Balozi Nchimbi asimamishwa Ndanda, ampigia simu Waziri TAMISEMI, nae apokea maelekezo ujenzi wa kituo cha afya

Balozi Nchimbi asimamishwa Ndanda, ampigia simu Waziri TAMISEMI, nae apokea maelekezo ujenzi wa kituo cha afya

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
BALOZI NCHIMBI ASIMAMISHWA NDANDA, AMPIGIA SIMU WAZIRI TAMISEMI, NAE APOKEA MAELEKEZO UJENZI WA KITUO CHA AFYA

▶️ Asisitiza wananchi kuendelea kulinda amani, utulivu na mshikamano nchini

▶️ Atoa wito kwa Serikali kuhakikisha wakulima wanakuwa salama na wafugaji pia kwani wanategemeana

Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, 28 Julai, 2024 akiwa njiani kuelekea Mtwara Mjini baada ya kuzungumza na Wananchi na Wanachama wa Masasi amesimamishwa na wananchi katika eneo la Kata ya Nganganga Jimbo la Ndanda wakitaka awasalimie na kuzungumza nao.

Akiwa hapo Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameendelea kuwasisitiza Watanzania kuhusu umuhimu wa umoja wa kitaifa kwa kutunza tunu ya amani iliyopo nchini, pamoja na kumpigia simu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akitaka kujua utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya, ambapo Waziri alipokea maelekezo na kuahidi kuwa ujenzi utaanza mwezi ujao baada tu ya mwaka wa fedha kuanza.

Katibu Mkuu wa CCM na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anaendelea na ziara ya mikoa miwili inayolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu.
 

Attachments

  • IMG-20240728-WA0216.jpg
    IMG-20240728-WA0216.jpg
    183 KB · Views: 2
  • IMG-20240728-WA0215.jpg
    IMG-20240728-WA0215.jpg
    745.8 KB · Views: 3
  • IMG-20240728-WA0214.jpg
    IMG-20240728-WA0214.jpg
    214.1 KB · Views: 2
  • IMG-20240728-WA0217.jpg
    IMG-20240728-WA0217.jpg
    178.4 KB · Views: 2
  • IMG-20240728-WA0218.jpg
    IMG-20240728-WA0218.jpg
    195.9 KB · Views: 5
  • IMG-20240728-WA0219.jpg
    IMG-20240728-WA0219.jpg
    215.9 KB · Views: 2
Kusimamisha..mb....o..o inawezekana..vinginevyo hakuna jipya hapo, hizo ni siasa za hadaa za CCM na zilishazoeleka mbona!
 
Hii nchi ina viongozi wajinga sn, eneo hilo kuna RC/RAS/RSO/DC/DAS/DED/DSO/Mbunge/diwani na watumishi wengine, wote hao hawajaona umuhimu wa kuwa na kituo cha Afya mpaka aone Katibu Mkuu wa CCM? Tuna serikali ya hovyo sn
 
Ded yupo, DC yupo, diwabi yupo, mbunge yupo. Hawakujua hakuna kituo cha afya eneo hilo??
Hadi waigiane simu?
Wanasubiri fungu la Pesa za Serikali hawataki kutumia Pesa za Halmashauri, mboni Nchengerwa kalizungumzia hilo Jana haujasikia?
 
Kusimamisha..mb....o..o inawezekana..vinginevyo hakuna jipya hapo, hizo ni siasa za hadaa za CCM na zilishazoeleka mbona!
Kwenye vitu serious utani weka pembeni kwenye msiba usilete utani wa ngumi utasababisha kutokee msiba mwingine Mzee we namna gani kuna shida gani hapo?
 
Back
Top Bottom