TANZIA Balozi Paul Milyango Rupia amefariki dunia nchini Afrika Kusini

Hamid Rubawa

Member
Joined
May 23, 2018
Posts
72
Reaction score
211
Nimehuzunishwa na kifo cha Balozi Paul Milyango Rupia Aliyekuwa na umri wa miaka 84. Mauti yalimkuta Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Paul alikuwa miongoni mwa wanadiplomasia wabobezi wa Tanzania na alikuwa muungwana. Kifo chake kimetupokonya busara na bashasha zake.

20220916_113042.jpg

Rupia.jpg

Balozi Paul Rupia (Kulia) akitunukiwa Nishani na Rais Kikwete(Mstaafu)

=======

Katibu Mkuu Kiongozi wa tano, Balozi Paul Rupia amefariki dunia leo asubuhi nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 86.

Taarifa ya kifo chake imetolewa leo Septemba 16 kwa Mwananchi na mtu wa karibu na familia hiyo, Mzee wa Atikali ambaye naye alipewa taarifa hiyo na mtoto wa marehemu, Peter.

Mbali na wadhifa wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Rupia amekuwa ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje kuanzia mwaka 1963 na baadaye alikuwa balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwamo Uingereza na baadaye balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Pia, aliwahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Dar es Salaam.

Balozi Rupia aliyezaliwa Januari 7, 1936 katika hospitali ya Nkolandoto mkoani Shinyanga ni mtoto wa mpigania uhuru, mfanyabiashara na mwanasiasa, John Rupia.

Kwa nyakati tofauti, (Baba yake) John Rupia amekuwa mwaasisi wa chama cha TAA (Tanganyika African Association), TANU, (Tanganyika African National Union) na AA (African Association (AA) na alishiriki katika baraza maarufu la wazee wa TANU wakati huo akiwa pamoja na kina Mzee Mwinyikambi, Tambaza, Mshume, Chamwenyewe, Haidar Mwinyimvua na Rajab Diwani.

Na walipotoka TAA na kuanzisha TANU, John Rupia alipewa nafasi ya kuwa Makamu Mwenyekiti chini ya uongozi wa Julius Nyerere, akiwa na kadi namba 7.

Baba yake balozi Rupia (John Rupia) anatajwa kuwa ndiye aliyekuwa mfadhili namba moja kwa kukiendesha na kukikuza chama cha TANU kwa kujitolea kulipa mishahara na posho.

Pia, kwa sehemu kubwa aligharamia safari ya Mwalimu Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa kuelezea dunia kwamba Watanganyika walikuwa tayari kujitawala.

Baba yake balozi Rupia ndiye alimnunulia suti za kuvaa safarini na kumpa fedha za kujikimu Mwalimu Nyerere katika safari yake nchini Marekani.

Balozi Rupia ameacha mjane Rose Rupia na watoto Peter, Suzan, Pauline na Simon.

Makatibu wakuu kiongozi waliopita

Dunstan A. Omary 1962- 1964

Joseph A. Namata 1964-1967

Dickson A. Nkembo 1967-1974

Timothy Apiyo 1974-1986

Paul M. Rupia 1986-1995

Martene Y.C Lumbanga 1995-2006

Philimon L. Luhanjo 2006-2011

Ombeni Sefue 2012-2016 [3]

John William Kijazi 2016-2021

Bashiru Ally 2021-2021

Hussein Athuman Kattanga 2021

Chanzo: Mwananchi
 
Nimehuzunishwa na kifo cha Balozi Paul Milyango Rupia Aliyekuwa na umri wa miaka 84. Mauti yalimkuta Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Paul alikuwa miongoni mwa wanadiplomasia wabobezi wa Tanzania na alikuwa muungwana. Kifo chake kimetupokonya busara na bashasha zake.

View attachment 2358641

Amefanana na mwalimu wangu wa civics, tayari ni marehemu
 
Nimehuzunishwa na kifo cha Balozi Paul Milyango Rupia Aliyekuwa na umri wa miaka 84. Mauti yalimkuta Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Paul alikuwa miongoni mwa wanadiplomasia wabobezi wa Tanzania na alikuwa muungwana. Kifo chake kimetupokonya busara na bashasha zake.

View attachment 2358641

View attachment 2358668
Balozi Paul Rupia (Kulia) akitunukiwa Nishani na Rais Kikwete(Mstaafu)

=======

Katibu Mkuu Kiongozi wa tano, Balozi Paul Rupia amefariki dunia leo asubuhi nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 86.

Taarifa ya kifo chake imetolewa leo Septemba 16 kwa Mwananchi na mtu wa karibu na familia hiyo, Mzee wa Atikali ambaye naye alipewa taarifa hiyo na mtoto wa marehemu, Peter.

Mbali na wadhifa wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Rupia amekuwa ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje kuanzia mwaka 1963 na baadaye alikuwa balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwamo Uingereza na baadaye balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Pia, aliwahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Dar es Salaam.

Balozi Rupia aliyezaliwa Januari 7, 1936 katika hospitali ya Nkolandoto mkoani Shinyanga ni mtoto wa mpigania uhuru, mfanyabiashara na mwanasiasa, John Rupia.

Kwa nyakati tofauti, (Baba yake) John Rupia amekuwa mwaasisi wa chama cha TAA (Tanganyika African Association), TANU, (Tanganyika African National Union) na AA (African Association (AA) na alishiriki katika baraza maarufu la wazee wa TANU wakati huo akiwa pamoja na kina Mzee Mwinyikambi, Tambaza, Mshume, Chamwenyewe, Haidar Mwinyimvua na Rajab Diwani.

Na walipotoka TAA na kuanzisha TANU, John Rupia alipewa nafasi ya kuwa Makamu Mwenyekiti chini ya uongozi wa Julius Nyerere, akiwa na kadi namba 7.

Baba yake balozi Rupia (John Rupia) anatajwa kuwa ndiye aliyekuwa mfadhili namba moja kwa kukiendesha na kukikuza chama cha TANU kwa kujitolea kulipa mishahara na posho.

Pia, kwa sehemu kubwa aligharamia safari ya Mwalimu Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa kuelezea dunia kwamba Watanganyika walikuwa tayari kujitawala.

Baba yake balozi Rupia ndiye alimnunulia suti za kuvaa safarini na kumpa fedha za kujikimu Mwalimu Nyerere katika safari yake nchini Marekani.

Balozi Rupia ameacha mjane Rose Rupia na watoto Peter, Suzan, Pauline na Simon.

Makatibu wakuu kiongozi waliopita

Dunstan A. Omary 1962- 1964

Joseph A. Namata 1964-1967

Dickson A. Nkembo 1967-1974

Timothy Apiyo 1974-1986

Paul M. Rupia 1986-1995

Martene Y.C Lumbanga 1995-2006

Philimon L. Luhanjo 2006-2011

Ombeni Sefue 2012-2016 [3]

John William Kijazi 2016-2021

Bashiru Ally 2021-2021

Hussein Athuman Kattanga 2021

Chanzo: Mwananchi
Pole kwa familia...
 
Familia yake moja ipo hapa mikocheni B karb na clouds redio
 
Back
Top Bottom