Balozi Polepole jitokeze sasa tukuunge mkono kuwakataa wahuni

Balozi Polepole jitokeze sasa tukuunge mkono kuwakataa wahuni

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Kwa sababu Samia hajiamini ndani ya CCM.kuelekea 2025!

CCM-Samia wanatumia nguvu kubwa Sana ili kuhakikisha kwamba. Hakuna mwana CCM ambaye anaweza kupata ushawishi wa kisiasa ndani na nje ya CCM nchini zaidi yake Samia!

Hii yote ni kwa sababu Samia bado ana uchu wa madaraka kuliko kitu kingine chochote.
Na hajiamini ndani ya chama ambacho yeye binafsi ndiye mwenyekiti wake.

Huku akihanikizwa na genge la walamba Asali walioko nyuma yake, ambao kwa sasa wananufaika kwa 100% na urais wa Samia na uenyekiti wa Samia katika CCM.

Ninaposema hayo, ninamaanisha kuhusu mkakati unaoendelea sasa ndani ya CCM kwa kumsafishia njia Samia kuelekea 2025.

Ilianza kwa kuwaondoa watu wa JPM, kina Bashiru, Polepole na wengineo.

Polepole yeye akajaribu kufurukuta kwa kuunda Platform yake kupitia Programu yake ya Shule ya Uongozi kupitia Mitandao na Luninga, ikaonekana kama anaendelea kujikusanyia umaarufu.

Kilichofuatia ni kupelekwa nje ya nchi, Malawi, ambako ni balozi wa Tanzania mpaka sasa
(wale mliowahi kupitia uchimbaji dhahabu, mnafahamu maana ya kula "Malawi").

Bashiru yeye ameendelea kuwa kimya kwa muda wote, na ninadhani ni kwa sababu, wako wanaompenda ndani ya system ambao wanampa muongozo ili aendelee kuwa salama.

Haikuishia hapo. Kundi la pili ni Lukuvi na Kabudi, walichomolewa na kurudishwa Ikulu kusoma magazeti.
Hii ikiwa mbinu nyingine ya kuwaondoa kwenye utendaji ambao unaweza kuwajengea umaarufu kuelekea 2025.

Na pale walipo wako chini ya uangalizi maalumu,bila wao kulijua hilo. Ndio maana tunaona hata inafikia sasa Kabudi kupewa Muongozo wa kuja kusema mambo yasiyoeleweka kuhusu Makinikia.

Haijaishia hapo.... Samia bado hajaridhika, kwa kujua kwamba yeye bado hana mtandao ndani ya CCM kwa huku Bara, ameendeleza wimbi la pangua pangua huku akijaribu kujenga mtandao wake.

Tatizo ni kwamba anatumia njia ambayo sio sahihi....
kwa mfano sasa hivi kwenye uchaguzi ndani ya CCM, ameruhusu watendaji wa serikali walioko madarakani, kama wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ... wamechukua fomu na kugombea katika nafasi mbalimbali ndani ya chama.
Na baadhi yao wamefanikiwa.Mfano halisi ni Jerry Murro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ikungi-Singida.amegombea na kushinda.huku akiwa pia mkuu wa wilaya hiyohiyo aliyogombea.
Wengi wa hawa,wamegombea huku wakiwa na maelekezo rasmi, ili kuupata ujumbe wa kamati kuu ya CCM.
Lengo likiwa ni Samia kutengeneza mazingira kama alivyowahi kufanya Edward Lowassa kipindi kilichopita.

Ndio maana wale wakuu wa wilaya wastaafu wote waliojaribu kugombea wametupwa nje, kwa kuhofia kwamba huenda wasimuunge Samia mkono huko mbeleni.

Na ndio maana kumeibuka na lindi kibwa la UVCCM-Samia ambao wanakurupuka na kujikuta wakiyoa kauli tata na zenye kutishia watu hivi sasa.mfano wa karibuni ukiwa wa Tulia Akson Zipka wa Bunge la JMT.

Kuhusu Overshine!

Mfano hai wa karibuni, ni kutenguliwa kwa waziri Wa mambo ya nje Mama Liberata Muramura.

Kisa halisi hakijulikani wazi, lakini kutokana na kauli yake mwenyekiti wa CCM mama Samia Suluhu Hassan.

Ni kwamba alizidi nje ya mipaka yake kikazi(kwamba alivuka red line)
Tafsiri hii inatokana na yeye kutokuwa kwenye msafara wa Samia nchini Msumbiji, alikopaswa kuwepo kulingana na procol halisi.

Badala yake yeye akawa Marekani, ambako alikuwepo makamu wa Rais kwa wakati huo, akihudhuria mkutano mkuu wa UN. (Kule alipaswa kuwepo naibu waziri, samamba na makamu wa rais.).

Na kibaya zaidi. Mulamula akaibukia white house akialikwa kwa Dinner pamoja na rais wa nchi hiyo Joe Biden.

Na isitoshe Mulamula akapiga picha ya pamoja na Rais huyo wakiwa na mkewe.

Ikumbukwe pia Mulamula aliwahi kualikwa na familia ya Rais mstaafu wa nchi hiyo Barak Obama.

Na pia alipiga picha kama hiyo.

Sasa kwa jinsi Mama alivyo na hofu ya kuwa outshined....
Kilichoendelea ndio hiki tulichokiona juzi kwa yaliyompata Mulamula,huku likitolewa angalizo na kwa wengine kwamba wasijaribu kuvuka mipaka.

Hata upinzani hajaachwa Salama......

Tumeona kilichompata Joseph Mbatia mwenyekiti wa NCCR -MAGEUZI .

Ameadhibiwa kwa kile kilichoitwa na mfumo kama kumkosea mama adabu kwa kukataa kumuita Samia "mama" na badala yake akaendelea kumuita "dada".

Ukizingatia kwamba amekuwa na uswahiba na CCM kwa muda mrefu, hadi kupelekea kuwahi kupewa ubunge wa viti maalumu huko nyuma, ikiwemo na ubunge wa EALA kwa dada yake Mbatia pia.

My Take!

Kwa sababu ni wazi kabisa kwamba mama Samia na CCM kwa ujumla, wametokea kuififisha nyota ya maendeleo ya nchi, ambayo yalianza kuonekana wazi mbele ya watanzania.

Wameturudisha nyuma miaka 10 iliyopita.

Wanaendelea kukopa mikopo inayotuzalishia TOZO.

Wanaelekea kuturudisha kwenye Richmond Empire!

Na kwa sababu Upinzani nao umekuwa sehemu ya walamba asali.

Leo hii Zitto Kabwe na genge msoga,wamerudi na kuwa kitu kimoja.

Chadema imekaa kama wanagawana fito badala ya kujenga chama chao.

Wengine wamebaki kufanya mikutano ya matusi huko Club houses,bila kuwa na hoja zenye mashiko na njia mbadala wa jinsi ya kulikwamua taifa hili lilipo.
Huku wakifundisha somo la historia ya mashambulizi dhidi yao.
Badala ya kutoa sera zenye ushawishi kwa mwananchi ili wajikite kujenga chama chao kuanzia mashinani.na hatimae kujizolea wafuasi zaidi.kuelekea 2025.

Wenye busara kama mwenyekiti Mbowe wamepatwa vigugumizi ghafla.

Ni Wakati Sasa wa wana CCM wenye uthubutu kama Komredi wa ukweli.

Ndugu Humphrey Polepole,ambaye wengi ndani ya CCM wameona uthubutu wako.

Njoo usimamie unachokiamini,na hautakuwa peke yako.

Watu wameichoka CCM hii ya mateka, wanahitaji mbadala, lakini hawauoni kwa sasa!
Mungu atakuwa nawe Muda Wote.

With Many More Blessings Ahead of You.
View attachment 2381174
View attachment 2381175View attachment 2381179
 
Awamu hii huwa nataype nikitetemeka maana ukikosoa tu unaweza jikuta mahali pabaya mno. Na mleta mada umetoa mifano hai.
 
Kwa sababu Samia hajiamini ndani ya CCM.kuelekea 2025!
CCM-Samia wanatumia nguvu kubwa Sana ili kuhakikisha kwamba. Hakuna mwana CCM ambaye anaweza kupata ushawishi wawa kisiasa ndani na nje ya CCM nchini zaidi yake Samia!

Hii yote ni kwa sababu Samia bado ana uchu wa madaraka kuliko kitu kingine chochote.
Na hajiamini ndani

Huku akihanikizwa na genge la walamba Asali walioko nyuma yake, ambao kwa sasa wananufaika kwa 100% na urais wa Samia na uenyekiti wa Samia katika CCM.

Ninaposema hayo, ninamaanisha kuhusu mkakati unaoendelea sasa ndani ya CCM kwa kumsafishia njia Samia kuelekea 2025.

Ilianza kwa kuwaondoa watu wa JPM, kina Bashiru, Polepole na wengineo.

Polepole yeye akajaribu kufurukuta kwa kuunda Platform yake kupitia Programu yake ya Shule ya Uongozi kupitia Mitandao na Luninga, ikaonekana kama anaendelea kujikusanyia umaarufu.

Kilichofuatia ni kupelekwa nje ya nchi, Malawi, ambako ni balozi wa Tanzania mpaka sasa
(wale mliowahi kupitia uchimbaji dhahabu, mnafahamu maana ya kula "Malawi").

Bashiru yeye ameendelea kuwa kimya kwa muda wote, na ninadhani ni kwa sababu, wako wanaompenda ndani ya system ambao wanampa muongozo ili aendelee kuwa salama.

Haikuishia hapo. Kundi la pili ni Lukuvi na Kabudi, walichomolewa na kurudishwa Ikulu kusoma magazeti.

Huku wakiwa chini ya uangalizi maalumu. Ndio maana tunaona hata inafikia Kabudi kupewa Muongozo wa kuja kusema mambo yasiyoeleweka kuhusu Makinikia.

Haijaishia hapo. Samia bado hajaridhika, kwa kujua kwamba yeye bado hana mtandao ndani ya CCM kwa huku Bara, ameendeleza wimbi la pangua pangua huku akijaribu kujenga mtandao wake.

Tatizo ni kwamba anatumia njia ambayo sio sahihi, kwa mfano sasa hivi kwenye uchaguzi ndani ya CCM, ameruhusu watendaji wa serikali walioko madarakani, kama wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ... wamechukua fomu na kugombea katika nafasi mbalimbali ndani ya chama.

Lakini wengi wakiwa na maelekezo rasmi ili kuupata ujumbe wa kamati kuu ya CCM.
Lengo likiwa ni Samia kutengeneza mazingira kama alivyowahi kufanya Edward Lowassa kipindi kilichopita.

Ndio maana wale wakuu wa wilaya wastaafu wote waliojaribu kugombea wametupwa nje, kwa kuhofia kwamba huenda wasimuunge Samia mkono huko mbeleni.

Mfano hai wa karibuni, ni kutenguliwa kwa waziri Wa mambo ya nje Mama Liberata Muramura.

Kisa halisi hakijulikani wazi, lakini kutokana na kauli yake mwenyekiti wa CCM mama Samia Suluhu Hassan.

Ni kwamba alizidi nje ya mipaka yake kikazi(kwamba alivuka red line)
Tafsiri hii inatokana na yeye kutokuwa kwenye msafara wa Samia nchini Msumbiji, alikopaswa kuwepo kulingana na procol halisi.

Badala yake yeye akawa Marekani, ambako alikuwepo makamu wa Rais kwa wakati huo, akihudhuria mkutano mkuu wa UN. (Kule alipaswa kuwepo naibu waziri, samamba na makamu wa rais.).

Na kibaya zaidi. Mulamula akaibukia white house akialikwa kwa Dinner pamoja na rais wa nchi hiyo Joe Biden.

Na isitoshe Mulamula akapiga picha ya pamoja na Rais huyo wakiwa na mkewe.

Ikumbukwe pia Mulamula aliwahi kualikwa na familia ya Rais mstaafu wa nchi hiyo Barak Obama.

Na pia alipiga picha kama hiyo.

Sasa kwa jinsi Mama alivyo na hofu ya kuwa outshined....
Kilichoendelea ndio hiki tulichokiona juzi kwa yaliyompata Mulamula,huku likitolewa angalizo na kwa wengine kwamba wasijaribu kuvuka mipaka.

Hata upinzani hajaachwa Salama......

Tumeona kilichompata Joseph Mbatia mwenyekiti wa NCCR -MAGEUZI .

Ameadhibiwa kwa kile kilichoitwa na mfumo kama kumkosea mama adabu kwa kukataa kumuita Samia "mama" na badala yake akaendelea kumuita "dada".

Ukizingatia kwamba amekuwa na uswahiba na CCM kwa muda mrefu, hadi kupelekea kuwahi kupewa ubunge wa viti maalumu huko nyuma, ikiwemo na ubunge wa EALA kwa dada yake Mbatia pia.

My Take!

Kwa sababu ni wazi kabisa kwamba mama Samia na CCM kwa ujumla, wametokea kuififisha nyota ya maendeleo ya nchi, ambayo yalianza kuonekana wazi mbele ya watanzania.

Wameturudisha nyuma miaka 10 iliyopita.

Wanaendelea kukopa mikopo inayotuzalishia TOZO.

Wanaelekea kuturudisha kwenye Richmond Empire!

Na kwa sababu Upinzani nao umekuwa sehemu ya walamba asali.

Leo hii Zitto Kabwe na genge msoga,wamerudi na kuwa kitu kimoja.

Chadema imekaa kama wanagawana fito.

Wenye busara kama mwenyekiti Mbowe wamepatwa vigugumizi.

Ni Wakati Sasa wa wana CCM wenye uthubutu kama Komredi wa ukweli.

Ndugu Humphrey Polepole,ambaye wengi ndani ya CCM wameona uthubutu wako.

Njoo usimamie unachokiamini,na hautakuwa peke yako.

Watu wameichoka CCM hii ya mateka, wanahitaji mbadala, lakini hawauoni kwa sasa!
Mungu atakuwa nawe Muda Wote.

With Many More Blessings Ahead of You.
cha kwanza hakunaga siasa ya kweli afrika kila mtu yupo kwa ajilr ya masihari yake.
 
Kwa kuwa walamba asali wanamshawishi agombee tena uchaguzi ujao,basi ikitokea amegombea na kivuli kama enzi zetu za mfumo wa chama kimoja basi sisi tutachagua kivuli.
 
Muache Samia nae awe dikteta sasa, awanyooshe hayo masalia ya Jiwe

Viva SSH
Na kwa sababu Wenye vyeti fake kama wewe,ndio mmetufikisha hapa.
Lazima kiongozi yeyote mpenda maendeleo angeanza ku deal na nyinyi kwanza
Pole kwa yaliyokukuta.Ila nina imani siku moja na wewe utakufa na mtakutana na Magufuli(R.I.P).huko aliko ili mmalizane mbele ya Mungu mwenyezi.
 
Kwa kuwa walamba asali wanamshawishi agombee tena uchaguzi ujao,basi ikitokea amegombea na kivuli kama enzi zetu za mfumo wa chama kimoja basi sisi tutachagua kivuli.
Mimi pia.!
 
Huyo unayemsema mwenyewe mbona ni muhuni ?

Aanze kuacha uhuni kwanza ndio aende kuupinga uhuni.
Ule ni ujana tu.tunaposema uhuni ni msamiati unaolenga mbali zaidi ya uhuni unaoufahamu au kuudhania wewe!
Tunaongelea uhuni wa kisiasa kama unaofanywa na CCM-Samia kwa sasa ndani ya chama chao.
 
Mwanzo akiwa hajaanza kuingia 18 za kikwete....alikuwa vizuri,lakini tangu alipokubali kuwa remote controled.....shida ikaanzia hapo.
Sorry mkuu nje ya mada, hicho kichwa na aina hiyo ya nywele zamani nikiwa shule nilipenda sana kuwakong'ota makonzi halafu nakimbia...

Nilikua nikiona tu mtu mwenye kisogo cha hivyo na kipilipili basi moyo hunisisimka na kutamani kutia makwenzi tuuu afu huyooo nateleza...
 
Back
Top Bottom