Balozi wa Marekani Michael A. Battle: Kusema Tanzania haijafungamana, uhalisia haupo hivyo

Yote hayo tisa.

...na haihusiani na alichokisema.
=======
Tanzania haikuwa imefungamana na Nchi yeyote ile. Ikiwa ina maana hatushobokei East ama West, ubepari ama Ukomonisti...na lengo lilikuwa ni moja

'To exercise a modicum of sovereign Initiatives" rather than being swept by the cold war, geopolitical pressure and Ideological mambo jambo, vile vile, Tulihofia(Nchi za NAM) kupigwa na Nyuklia ikiwa tungesema 'tupo na marekani' au 'tupo na urusi' tena walikuwa na lisaa lao la propaganda likionyesha bomu la nyuklia litafika dakika yeyote ile. Nani aliyataka Ujinga wao?

Ikumbukwe NAM iliasisiwa miaka ya sitini wakati wakitishiana nyau "Bay of pigs Fiasco'

.....aliyemdanganya kwamba Watanzania tunafikiri nchi yetu kutokufungamana na nchi yeyote, tafsiri yake kuwa hatuna Ushirikiano ni nani? Kwani uwepo wetu NAM haukuwa ushirikiano na Nchi zingine?

Labda CHADEMA waliodai "Sasa nchi imefunguliwa"

Ilifungwa wapi?(rejea alichosema balozi)

Ameokota wapi huo Ujinga?
 
Wenzio ndani ya chama hawajui nini maana ya kufungamana na mashirikiano ni wengi na ni wajinga kuliko wewe. kitendo cha kusign treaties of agreements ina maana kuna kashirikiano kwenye baadhi ya mambo hasa ya kisera. Kwamba sera zenu zinafungamana au zinashabihiana kwa maana hiyo kuna mambo mnajadiliana kwa pamoja au kupokea maoni yao. Tatizo la wajinga wengu wakipewa ushauri hutumia nguvu kuzima hoja.
 
Mungu Wabariki Wazungu
 
Napendaga Wamarekani wanapopata ujasiri wa kutoa hoja kama hizi kuhusu Tanzania ambazo mashuleni tunaaminishwa na kukaririshwa. Hauwezi kusikia hoja hizi kutoka kwa Watanzania wenzetu, hata wasomi. Labda Lissu tu ndiyo huwa ana upeo na ujasiri huo.

Kuna mwaka fulani balozi wa Marekani aliwahi kuhoji, kama nakumbuka vizuri akasema, si kweli tunapojisifu kuwa Tanzania kama taifa haijawahi kumwaga damu. Ilikuwa ni hoja nzito kweli kweli. Nakumbuka Serikali ilituma malalamiko yake kuwa amekiuka kanuni na misingi ya diplomasia. Kwa anayekumbuka hili anikumbushe jina la huyo Balozi na alichosema maana naweza kuwa off kidogo.
 
Tanzania ni nchi huru halisi haiendeshwi kwa dhana, haichaguliwi rafiki wala haielekezwi nchi ya kushirikiana nayo full stop.

Tanzania ina malengo na mipango yake, Lakini pia inazo mbinu namna halisi ya kuyafikia malengo yake. Siyo dhana.

Balozi aachene na masuala ya dhana, ambayo ni sawa na ushirikina na ramli chonganishi tu, hayo ni mambo ya kijima 🐒
 
Unaonekana una mapenzi makubwa ma Marekani🤣🤣🤣
 
Mdogo mdogo tunabanwa vifuko vya mbegu....

LeLe huanzaga kama utani
 
Wanadhani kuwa wadau wa maendeleo wana haki ya kutoa maelekezo ni namna gani nchi ijiendeshe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…