Uchaguzi 2020 Balozi wa Marekani nchini Tanzania: Serikali ihakikishe usalama wa Viongozi wa Upinzani, iwaachie waliokamatwa na kurejesha mawasiliano kwa wananchi

Umekandamizwa nini wewe? Internet yetu ina muhusu nini yeye? Na mbona haulizi kama tunakula?
Shitukeni huyo balozi ni ibilisi kavaa ngozi ya kondoo
Tuko tayari kusaidiwa hata na shetani ili tu huyu mkoloni mweusi atoke
 
Ni rahisi sana kuona kibanzi kilichopo kwenye jicho la mwenzako lingali la kwako lina boriti.
Balozi hebu litetee Taifa lako la Marekani huko kusikoeleweka. Hapa Tanzania tuna amani, tunafanya kazi zetu na maisha yanaenda vizuri tu
 
Nichukue nafasi hii kusema yakwamba viongozi wa upinzani hawawekwi ndani sababu ya kuonewa bali ni pale wanapokiuka sheria za nchi kwani wasije wakahatarisha amani ya nchi yetu.
 
Hayo ni mawazo yako wewe pamoja na vijana wenzio wa Kwa ufipa mana ndivyo mlivyomezeshwa.
 
Katika harakati za ukombozi ni lazima raia kama nyie muwepo ili wakati Uhuru kamili unaporeviil upate joto ya jiwe vizuri.
 
Kabisa anajijengea tabia ya kuingilia siasa za Tanzania; huku anajifanya kiziwi kwa matamshi hatari yanayotolewa ya kuvunja amani na hao anaowatetea.

Serikali imeshawabembeleza USA vya kutosha ila wameonesha wazi hawana nia njema, ni muda wa kuamua tu wafanye wanalotaka ila hamna haja ya kuwaendekeza wajinga, wao wanataka itokee civil disobedience, mali za watu zichomwe moto nk., huu ujinga sio wa kuendekeza kabisa.
 
Hivi huyu baba hanaga kazi zingine? Kwa Kenya huwaga wanaside na serikali kukandamiza wapinzani kwa Tz wanaside na wapinzani dhidi ya serikali. Wamerekani wanafiki sana jamani
Anaweweseka anapoona Tanzania inaimarika kiuchumi na huku jemedari wetu Magufuli anazidi kubarikiwa na M/Mungu katika kulijenga Taifa letu Tanzania
 
Je fujo zilitengenezwa hazikutengenezwa?
Wanaodai kuibiwa na kukamata kura je ushahidi ulichomwa haukuchomwa?kama ni kweli ni kwanini uchome kama sio mchzo wa kuigiza
je mbowe,zitto,mdee,heche,lema wangepata ubunge wangesema walichokisema?
turudi kwa wananchi je miaka yote walienda kutengeneza vitambi vyao na kunywa faru john zao walishawahi kuwakumbuka wananchi?

Turudi juzi tu apo janga la corona kuna Mbunge gani kati ya hao hata alitoa fungu la posho yake hata kwa wananchi wa jimbo lake kwamba serikali ipitishe lockdown yeye atasupport wananchi wake kwa chakula ?

Embu fikiri upya tena alafu uje uandike sio huo urojo wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…