Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia amerudishwa nyumbani kwa tuhuma za Upotevu wa Fedha Ubalozini

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia amerudishwa nyumbani kwa tuhuma za Upotevu wa Fedha Ubalozini

Nimemsikia Mh Rais leo alipokua anapokea ripoti ya CAG na TAKUKURU huko chamwino Dodoma akisema amemrudisha nyumbani balozi wa Tanzania nchini Ethiopia kupisha uchunguzi wa upotevu mkubwa wa fedha

Utafiti unaonyesha balozi huyu ni mama Naimi Hamza Azizi

Na suala hili lilianza kuchunguzwa tangu mwaka jana kama inyosemeka hapa chini
View attachment 1400286
Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia mikononi mwa Takukuru

Friday November 15 2019


Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania imekabidhiwa jalada na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki la uchunguzi la upotevu na matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Advertisement

Dar es Salaam. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jalada la kulifanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe amekabidhi jalada hilo leo Ijumaa Novemba 15, 2019 kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo katika ofisi ndogo za wizara jijiji Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja kutokana na jitihada za Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Uchunguzi huo unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Kuhusu kiwango cha fedha kilichopotea Katibu Mkuu, Dk Mnyepe amesema kitajulikana mara baada ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walilokabidhi.
Kisa tu mrembo, mteule wa JK/Membe...and Cuz She refused to bend over For the FOOLS of the current regime

Pole Dada Balozi
Balozi_Naimi_Azizi.jpg
 
Duh!.
Tukianzia kwa Aziz Ally
Kuna Dossa Aziz muasisi wa TANU alikutana na majanga.
Akaja Hamza Azizi wa polisi akakutana na majanga.
Akaja Capt. Azizi wa ATC naye yakamkuta ya kumkuta
Kuna mrembo mmoja wa familia ya Aziz naye ana yake.
Sasa Balozi Aziz!.

NB. Inawezekana ni majina tuu kufanana lakini hao Aziz wakawa ni familia tofauti na sio familia moja, lakini wakiwa ni familia moja, waandishi wa IJ inabidi wawatembelee.

Mzee wetu Maalim Mohamed Said bingwa wetu wa historia za waasisi, jee kina Aziz hao ni nasaba moja?. Tupe kisa cha Aziz Ali na Dossa Aziz watu wa kuunganisha dots tuunganishe kama yanayowatokea kina Azizi ni karma au ni ya walimwengu tuu, maana Balozi naye ni mashallah, udhaifu wa watu wetu tunaujua!, kisije kuwa ni kisa kama cha yule mama jicho gololi wa TIC au yule baby face wa SSRA.

P
Lile shetani linnyonya damu halishindwi kudai mzigo! Na hasa kama.mama mwenyewe ni white!
 
Leo Raisi Magufuli kasema huyo balozi alikwapua hela za ujenzi wa ofisi ya ubalozi hadi serikali ikanyanganywa kiwanja na serikali ya Ethiopia

Mamá kibaka huyo
 
Back
Top Bottom