Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukifanya 'Jambo' likampendeza 'Mkuu' naye akafurahi na kukutunuku 'Cheo Kikubwa' kama fadhila ya yale uliyoyafanya... Basi sisi wapenzi watazamaji tutarajie kuendelea kuona mengi yakitushangaza mojawapo ni kama hili.
Cheo cha Ubalozi ni sawa na kusema 'Rais Ugenini'.
MkuuKuna hali mbili au tatu kwenye makuzi
Kukua kimwili
Kukua kiakili
Kukua kimwili na kiakili
Kuna kukua kiroho pia lakini huku huambata na akili, huwezi kukua kiroho huku akili ikiwa ni ya kitoto
Makuzi ya kawaida ni kuwa na uwiano sawa wa kukua kimwili na kiakili.. Hapa kimwili namaanisha kiumri... Unaposikia fulani ana mambo ya kitoto tambua huyo umri umeenda lakini matendo yake kiakili ni sawa na ya mtoto wa umri fulani
Ama ukisikia ana mambo ya kikubwa yaani umrí ni mdogo lakini anayofanya yalipaswa kufanywa na mtu wa umri fulani kumzidi
Kuna shida kubwa huko kwenye vetting ya viongozi mbalimbali huko chama chawala..hasa viongozi hawa wa kisiasa.. Wengi hawateuliwi kutokana na weledi maarifa, ujuzi na umahiri bali huteuliwa kama asante ama kwa sababu fulani isiyo na tija kwa taifa
Nafasi zinazolalamikiwa sana kwa sasa ni nafasi za uwakilishi wa nchi mbalimbali cheo cha balozi.. Wateuliwa wengi hawajui ukubwa, umuhimu na weledi wa hii nafasi.. Wengi wao wanadhani balozi wa nchi ni sawa na balozi wa nyumba kumi
Balozi ni mwakilishi wa nchi pale alipo.. Ana mamlaka kamili na makubwa ya kusimama badala ya mkuu wa nchi..hivyo matendo yake, lugha yake, life style yake ni lazima iendane na nafasi anayoshikilia
Balozi mteule unaposhinda mitandaoni na kufanya vituko wanavyofanya wadogo zetu huko mitandaoni ni wazi kabisa huyo anakuwa hajitambui ama kakua kiumri na kimwili lakini sio kiakili....
Enzi za mwalimu kufanya vituko kama hivi ni automatically umejivua cheo husika hata kabla Mwalimu hajasema
Hebu ona hiki anachofanya huyu barozi wa walawi hapa ..!View attachment 2231544
Kuna mdau hapo juu kamshauri aachane na ubalozi arudi kwenye uanaharakati wake.. Hapo hatutakuwa na cha kusemaMkuu
Kuna kitu unapaswa kujiuliza hapo!!
Huyu ni mtu anaefurahia ushindi fulani na anashangilia uhusika wake kwenye huo ushindi!!
Nasikia jamaa ni mlokole
Ni kama anashangilia katiba mpya,na anajua jambo FULANI ambalo hata mama halijui KABISA!
TUSUBIRI
Namuona mlokole akipigiwa SALUTI!!
Kwanza kujirekodi ni tabia za mademu, haijarishi ni balozi au bodaboda.Kwanza kujirekodi ni tabia za mademu, haijarishi ni balozi au bodaboda.
Huyo mwendo ameshaumaliza, kama umeshafika Brantyre hapana tofauti na Turiani Morogoro, mwache aendelee kuzurura mjini hiyo nafasi aliyopewa Malawi ni adhabu anaumia sana kisaikolojia kutoka kumiliki shule ya uongozi mpaka sasa yeye ndio mwanafunzi anafundishwa uongozi anasumbuliwa na sonona.
Kama hujataka kumuelewa Polepole ni vigumu kumuelewa.Dah.[emoji23] labda nikwambie tu kwamba kila nafasi ya uongozi ina kanuni, masharti na vigezo vyake ..
Unahisi au una uhakika bwana mshana jr?Ataachaje kwa mfano
Fuatilia maisha yake kwanza ndio utamuelewa. Huyo alikuwepo kabla ya samia na magufuli kuwa marais. Ni international figure.Kwa sisi tuliopata bahata ya kusoma clinical psychology jamaa anaenda kupata mental health ill kwa kujiona yeye ni mkubwa sana kwenye hii (grandiose dellusion)....kila anapotembea,kila anachokifanya anaona kama nchi yote imemtizama....mimi naona ambacho huyu mtu mama samia angekifanya ili akili imrudi amnyang'anya hata ubarozi...arudi kwenye kazi yake ya uanaharakati na akijichanganya akaisema serikali vibaya apewe kesi ya ugaidi au ya uhujumu uchumi....
MkuuKuna mdau hapo juu kamshauri aachane na ubalozi arudi kwenye uanaharakati wake.. Hapo hatutakuwa na cha kusema
Mpaka kajipost anachecheza hivyo, siyo tena personal ni public life.Personal life mnaanza kuingilia, cha msingi kazi anafanya