Balozi wa Tanzania nchini Namibia (Kipilimba): Rais Magufuli yuko mzima anachapa kazi

Kwani balozi ndiye amekuwa msemaji mkuu wa serikali? "I smell a very big rat on the whole issue".
Ndio. Balozi ni msemaji wa Serikali yetu huko anakotuwakilisha. Na amesema kwa sababu amehojiwa.
Sijui hapa Bongo waandishi wetu wamejipangaje
Mimi naona kwenye Katiba mpya tuweke kipengele;
Rais lazima aonekane angalau mara 1 ndani ya wiki 2 kama hana cha kufanya nje angalau atoke akamsalimie Mlinzi wa Geti Kuu la kuingilia Ikulu. Pia kiwepo kipengele kuhusu AFYA. Tutaarifiwe kila siku afya ya Rais wetu aajiriwe mtu wa kutoa taarifa hata kama ataenda chooni na tumbo limemchafuka au vimeonekna vidamu tuambiwe.. Isipokuwa tu damu za kawaida kama Rais atakuwa mwanamke na hajaingia kwenye menopause. Yaani ikitokea ameukwaa STD toka kwa side chick wake lazima tuambiwe. Kwa kweli afya ya mkuu ni mali binafsi ya kila Raia.
 
Reactions: Mj1
Yaani balozi Namibia ndo atoe taarifa, huku waziri wa mambo ya nje yupo, msemaji wa serikali yupo, mkurugenzi wa habari Ikulu yupo, kuna kitu hakipo sawa Tanzania.
Yaani nashangaa kwa kweli................Au labda yuko nchini huko kikazi ndio maana balozi anatuhabarisha.
 
Ohooo kumbe alikuwa anawaharisha wananchi wa huko. Ahsante Mkuu
 
Ukiachilia mbali na mambo ya AFYA mfumo wa utoaji wa taarifa kuna tatizo ndani ya serikali watu wanatatizo la kusema ukweli hasa tanzania. Badala ya kusema corona ina badalishwa kuwa tatizo la upumuaji beleshi kijiji kubwa tofauti na wakenya kitu kina tamkwa kwa kwa kificho kiasi kwamba majibu hayajitoshelezi kiasi kwamba watu wanahoji hawapati majibu ya kujitosheleza wakihoji wanakamatwa na kuwekwa kizuizini je dawa mtu ajitokeze ili kuvunja mizizi ya uvumi ulipo.
 
Nairobi, Kenya

Where is President Magufuli as he goes missing from the public? | INSIDE POLITICS WITH BEN KITILI

Source: KTN News Kenya
 
14 March 2021

NCCR-MAGEUZI YAJITOSA SAKATA LA RAIS MAGUFULI

CHAMA cha upinzani nchini Tanzania – NCCR-Mageuzi – kimekoleza moto katika mjadala unaohusu mahali alipo Rais John Pombe Magufuli. Martha Chiomba, katibu mkuu wa chama hicho, amewaambia waandishi wa habari, leo Jumapili, tarehe 14 Machi2021, makao makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala, jijini Dar es Salaam, kwamba wananchi wanataka kujua, “mahali aliko rais wao kipenzi.”

Kwa niaba ya wanachama wa NCCR- Mageuzi na wananchi wengine, Matha amesema, “wananchi wanataja Rais Magufuli ajitokeze hadharani, ili kumaliza shauku yao, kuhusu mahali aliko rais wao.”

Akisitiza hoja yake, Matha ametumia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inayozungumzia uhuru wa maoni na haki kwa wananchi kupewa taarifa, wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli zao.
Source : MwanaHALISI TV
 
FAKE NEWS as usual.
 
Asante mkuu
 
Acha njaa; Kaa kimya usije kujiaibisha!!
 
Kipilimba ni balozi wa mchongo , Tangu lini balozi akawa msemaji wa serikali ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…