Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji kukutana na M/kiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge la EU kutoa ufafanuzi dhidi ya taarifa za upotoshaji

Kwani hukumbuki wakati Mr Mzungu aliposhindwa uchaguzi & maandamano kubuma akaamua atimkie kwa Bob Amsterdam & mabeberu wengine???
Nakumbuka sana hio na ndio maana CCM mna kauli mbiu yenu isemayo baada ya Mungu ni Mzungu.
 
Anaenda kuaibika tu kwa sababu Kuna hoja nyingi tu zisizojibika
 
Bado mnataka misaada ya mabeberu?
 
Kutokana na unyeti wa hili suala, asiachiwe huyo balozi peke yake kulishughulikia. Iundwe timu ya wajumbe wasiopungua watatu chini ya balozi wetu Sweden, litamalizwa mapema sana.
 
Hata habari za mauaji ya mtwara mlikanusha hivi hivi, lakini jana tumeona kamanda sirro akiwa huko na IGP wa msumbiji natumesikia kauli zake kuhusu uvamizi unaoendelea.
 
Umeharibu uzi wako hapo ulipohusisha EU na Ufipa! Yaan bado mnahangaika na watu waliokataliwa na wananchi? Miafrika sijui nani katuloga jamani! Kha!!
 
Nimetumia bando langu kusikiliza mjadala wote ule.Ulikuwa mjadala wa kamati yao na kwa bahati tumepata muda wa kuusilikiliza.Siioni cha kwenda kujibu,kama ni uongo basi umeanzia katika wawakiishi wao na kuna Bwana mmoja alikuwa akirudia "our people at the ground".EU ina office hapa na 2018 tulifukuza mwakilishi wao,kwa hiyo tumekuwa katika mvutano nao ingawa kichinihini kwa miaka miwili.
Jambo la pili walitamka wazi kuwa kuna kipengele amabcho kama wanatakakuikatia misaada Tanzania wanatakiwa wakitumie lakini mjumbe yule akaeleza ya kuwa hatujafikia huko.
Kuna sehemu katika utawala huu ambapo panaleta matatizo na ni "KUKUBALI KUKOSEA".Ifike mahali tukubali kuwa katika jambo fulani tumekosea na tujirekebishe.
Ukali wa mweneyekiti ni kama ukali Ndugai akimkoromea Lema au Mdee,ni kawaida!!
 
Anadhani McAllister ni katibu mwenezi wa Chadema. Acha akutane nae akajichore.
Hii mijitu ya CCM bure kabisa........

Hivi wanadhani watawadanganya hao "mabeberu" wa Ulaya kama wanavyotudanganya sisi?

Nyinyi CCM mnajua wazi kuwa hapa nchini kila kitu mmebana, kuanzia Tume ya uchaguzi CCM, Polisi CCM, Wasimamizi wa Uchaguzi CCM, Mahakama CCM!

Hivi unadhani katika mfumo huo unaobana kiasi hicho, wapinzani watakatizia wapi hapo?
 
Uko na mdomo wa bure na kijismatifoni cha kuazima, sasa una uhuru wa kubwabwaja lolote. Au ndo Mr Mzungu & Bob Amsteedam aliwaleta kuvuruga uchaguzi???
Mkuu lakini Sirro amekiri watu kuuawa hasa Zanzibar kwenue uchaguzi sasa sijajua tafsiri hasa ya neno 'amani na salama'
 
Mbona ni kawaida kwa MWIZI yeyote.. hata akikutwa na manyoya, minofu na kichwa, mwizi huendelea kubisha kuwa hakuiba.
Mc Allister na wenzake siyo wajinga
 
Kama ni uongo anakutana naye ili wafanyenini?
 
Balozi ndiyo wajibu wake wa kidiplomasia msimfundishe kazi wacha aonane na Mwenyekiti. Katika uzi wangu uliopita humu nilieleza umuhimu wa kipindi hiki kufanya kazi yao kiweledi kupangua hoja na tuhuma zinazochafua nchi yetu.
 
Viongozi wa dini,ccm. Vyombo vya habari, ccm. watumishi wa umma, ccm. Wasanii, ccm. wanafiki wote pamoja na maprof wa jalalani, ccm. wajingawajinga wote, ccm. Nk, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…