Balozi wa Zambia nchini Afrika Kusini afukuzwa kazi baada ya kuamuru Wafanyakazi wake wa Kiume wamnyoe nywele sehemu za siri

Balozi wa Zambia nchini Afrika Kusini afukuzwa kazi baada ya kuamuru Wafanyakazi wake wa Kiume wamnyoe nywele sehemu za siri

Inaelezwa kuwa Balozi huyo alitoa maagizo hayo ambayo siyo ya kidiplomasia kwa Wafanyakazi wake wa kiume licha ya wafanyakazi hao kukataa na nakueleza kuwa siyo sehemu ya majukumu yao ya kuwanyoa Mabalozi hasa sehemu zao za siri.
Wangekuwa wabongo, wangeomba wawe wanamnyoa kila siku
 
Labda ana kitambi hawezi kujifikia
Unajua Dar ukianzisha huduma ya kuondoa private hair kimzahamzaha unapata wateja na inaweza kuwa salon maarufu hadi watu wakashangaa!

Muhimu kila gender iwe na vyumba tofauti kama ilivyo vyoo na wahudumiwe na gender zao. Ni ubunifu tu halafu baada ya muda wengine wataiga na mwiko unakuwa umevunjwa inakuwa normal business kama nyingine.

I tell you; 30 yrs ago hakuna aliyetarajia leo wanawake wangekuwa wanatembea na skin tight barabarani; but it has become normal!

Joanah, cocastic, Jaji Mfawidhi, Nifah wazo hilo japo mwanzo mgumu.
 
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amemfukuza kazi Balozi wa Nchi hiyo nchini Afrika Kusini, Mazuba Monze kwa utovu wa nidhamu baada ya Balozi huyo kudaiwa kuwapa majukumu yasiyo yao Wafanyakazi wake wa kiume kwa kuwaagiza wamnyoe nywele zilizo kwenye sehemu zake za siri.

Vyombo mbalimbali vya habari vya Zambia vimeripoti kuwa Wafanyakazi hao walikataa kumnyoa Mama huyo sehemu za siri wakisema kuwa kazi hiyo sio tu haihusiani na masuala ya kidiplomasia lakini haikuwa sehemu ya majukumu yao ya kitaalamu waliyopangiwa kuyatekeleza kwenye Balozi hiyo iliyopo Pretoria wakisema hawajakwenda Afrika Kusini kumnyoa Balozi nywele zake sehemu za siri bali kulitumikia Taifa la Zambia.

Balozi huyo baada ya kukataliwa kunyolewa na Wafanyakazi hao aliwafukuza kazi Ubalozi akisema wameshindwa kutii agizo lake jambo lililopelekea Wafanyakazi hao kukata rufaa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakilalamikia kuonewa na baada ya uchunguzi kuonesha kweli walionewa Rais Hakainde Hichilema amechukua uamuzi wa kumfukuza kazi mara moja Balozi.

Katika hatua nyingine Raia mmoja mwenye asili ya Zambia ambaye anaishi Afrika Kusini amejitokeza na kusema madai dhidi ya Balozi Monze yametiwa chumvi au kutungwa na Wapinzani wake waliopanga kumchafua akisema kuna kampeni lizinduliwa dhidi ya Balozi huyo ikihusisha ripoti za uongo na uzushi ambao hatimaye ulisababisha kufukuzwa kwake.
 
Unajua Dar ukianzisha huduma ya kuondoa private hair kimzahamzaha unapata wateja na inaweza kuwa salon maarufu hadi watu wakashangaa...
Hili la jinzi,skin tight,vipensi kwa wanawake linanikwaza sana,maana ilikua laana hii juzi tu hapa,leo maofisini, barabarani wanawake ni tight na jinzi tu!!
 
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amemfukuza kazi Balozi wa Nchi hiyo nchini Afrika Kusini, Mazuba Monze kwa utovu wa nidhamu baada ya Balozi huyo kudaiwa kuwapa majukumu yasiyo yao Wafanyakazi wake wa kiume kwa kuwaagiza wamnyoe nywele zilizo kwenye sehemu zake za siri....
Mmmmm! Watu wanafanya makosa makubwa hawafukuzwi? Je imethibitika?
 
Back
Top Bottom