habari wadau wa JF? Mimi ni member mzuri wa jukwaa hili kwa kusoma na kupata mawazo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yananisaidia kama mjasiriamali mdogo kwa kiasi kikubwa.
Mbali na kuwa mjasiriamali lakini pia Mimi ni mtumishi wa umma katika kusukuma gurudumu hili la maisha ya kila siku.
Katika harakati zangu za mihangaiko niliomba mkopo wa mtumishi kutoka banc ABC ili inisaidie katika shughuli zangu mnamo November 06, na niliahidiwa kupata mkopo wangu baada ya Siku NNE hadi saba toka Siku ya maombi ya mkopo.. kinyume chake ni kwamba hadi Leo hii tar 24 nwezi DEC sijapata mkopo huo kama nilivyoahidiwa halafu kibaya makato ya mkopo yameshaanzwa kukatwa katika mshahara wangu.
nunefanya mawasiliano na afisa mikopo katika tawi nililoomva mkopo kanipa namba ya makao makuu lakini hakuna jibu la maana wanalonipa imefika hatua wote hawapokei simu yangu. Nimeanza kuhisi labda hawa watu ni matapeli au nimetapeliwa kwa namna Fulani..
kama kuna yeyote ana experience ya hawa jamaa hebu anijuze na mwenye kujua nifanye nini nipate haki yangu tafadhali nisaidieni jamani.
Mkuu kwa maelezo uliotoa naliona tatizo sehemu, natatizo lenyewe inawezekana kabisa unalifahamu au hulifahamuhulifaham. kama imefikua hatua ya were kukatwa basis jua mkopo wako ulishughulikiwa na kukamilika kwa wakati, pili tatizo lililopo ni kama ifuatavyo. Moja ,linawezekana lipo upande Wa afisa utumishi wako, hapa kuna vitu viwili vibavyoweza kufanya usipate hela yako kwa wakati ambavyo ni, kukosea kuingizwa kwa usahihi deductions/makato (yachunguze makato kama ni sawa) na kutoingizwa kwa usahihi total exposure/jumla ya mkopo wote. Ilikujua kama vyote hivi Viko sawa ni mpaka uende kwa afisa utumishi wako, jua hili benk haiwezi kukulipa kama hili haliko sawa kasababu itakula kwao.
Pili, afisa mikopo, kama na yeye hakuchukua taarifa taarifa sahihi za mteja kama za kibenk, yaani account ya mteja ambayo hela hiyo itapitia, majina ambayo yapo kwenye hiyo account ya mteja, check number ya mteja. Kama vitu hivi haviko sawa mteja atachelewa kulipwa mpaka virekebishwe.
Tatu, kwa mteja mwenyewe, ikiwa mteja kwa makusudi au kwa kughafirika, au kwa kutaka kupata hela haraka akatoa taarifa ambazo sio sahihi hatalipwa hatakama ameanza kukatwa au atachelewa kulipwa mpaka baadhi ya taarifa amvazo zinatiliwa shaka zirekebishwe.
Ushauri wangu kwako ni huu, kama kweli hujapata ushirikiano kuoka ka afisa Wa banc ABC muone Afisa utumishi wako tens yule ambae aliingiza hayo makato yako iliajirizishe kama yapi sahihi, halafu achukue Stahiki.
Pili lazima umlazimishe asisa wa mikopo akuambie hatma ya mkopo wako hasa ikuzingatiwa umeisha anza kukatwa na ni nini kimekwamisha wewe kutopata hela.
Tatu jitafakari wewe mwenyewe He taarifa ulizo to a zilikuwa sahihi?