Banc ABC ni taasisi ya kitapeli?

Banc ABC ni taasisi ya kitapeli?

Kama Raisi alienda BOT akakuta masnema yale we unategemea nini.

Yaani hapa inabidi waziri wa Fedha afanye surprise siku moja aseme kwamba wananchi wenye malalamiko na hizi Bank akutane nao live,aiseee kuna Bank lazima zitafungwaa hasa hivi vitaasisi vidogo.
Maana kuna uhuni na ujanja kibaoo,kuanzia uongozi wa juu ukifika kwa maofisa mikopo ndio balaa kabisaaaa.
 
Hii inaitwa Super Riba,piga dili kwa wajinga.
Maaana nchi maskini siku zote ndio wajanja wanakuja kupiga pesa.

Ukisema wanakuambia kwamba wao ndio wakombozi wa umaskini na wamekuja kuondoa umaskini.
Hahahaha,

BOT huwa wanasimamia kitu gani?
 
Hi bwana Kulyunga.
Mi ni mtumishi wa banc ABC nmejisikia vibaya sana baada ya kusoma taarifa yako lakini ninajukumu lakuhakikisha unaiona bank yetu kama sio yakitapeli wala namna yeyote ile mbaya kwa jamii. Nahisi kutakuwa na tatizo la mawasiliano kati ya ww mteja afisa wa mikopo aliekujazia fomu na watu wa makao makuu. Nakuhaidi kukushugulikia na upate taarifa sahihi juu ya mkopo wako siku ya jumatatu. Chakufanya naomba nitumie majina yako matatu na check number yako. No yangu 0717696744. Tunaomba utusamehe kwa changamoto zote zilizotokea wakati wa mkopo wako.
 
Wamejipotezea credibility yao tayari. Kwenye kipindi hiki cha utandawazi ukimfanyia mteja kitu kidogo tu taarifa zinasambaa mara moja na kupoteza wateja. Review kutoka kwa wateja zinaongea sana kuliko kujitangaza.

Sijui ninani atakayewaamini kwa yanayosemwa huko. Watu wengi wanaofungua account au kuchukua mikopo mikubwa ya biashara huwa wanaangalia credibility ya bank kwanza.

Hawa watu wajirekebishe otherwise wataishia kufunga biashara watakapokosa wateja kabisa.
 
Why usimuombe afike ofisini kwako/ kwenu ili mmalizane, maana akikutumia hizo detail kwa sms naona as if unaanzisha urasmu mwingine, I thought jumatatu angekuwa anapata mshiko wake kumbe taarifa sahihi tu? Ukiangalia post za wadau inaonekana watumishi hii bank wote mmefanana tabia zenu na mienendo yenu. Ni mtizamo wangu tu.
 
Mi npo makao makuu DSM kama na yeye yupo hapa afike ofisin kwetu apate taarifa sahihi ila kama yupo mkoani nimeona no njia sahihi yakumpatia taarifa moja kwa moja.
 
Mi npo makao makuu DSM kama na yeye yupo hapa afike ofisin kwetu apate taarifa sahihi ila kama yupo mkoani nimeona no njia sahihi yakumpatia taarifa moja kwa moja.

Naomba pia utujibu maswali yetu
owner wa bank hii ni kina nani?
pale kariakoo kwenye tawi lenu kuna ABC hotel na ABC kitu gani sijui
ni kampuni moja?

zile pesa za Obama alizowapa muwakopeshe wajasiriamali..zilienda wapi?
 
Kutakuwa na tatizo katika mkopo wake so baada ya kufika ofisin ndo ntapata jib kama ni kupata pesa au kunatatizo alijue na ajue chakufanya
 
Hi bwana Kulyunga.
Mi ni mtumishi wa banc ABC nmejisikia vibaya sana baada ya kusoma taarifa yako lakini ninajukumu lakuhakikisha unaiona bank yetu kama sio yakitapeli wala namna yeyote ile mbaya kwa jamii. Nahisi kutakuwa na tatizo la mawasiliano kati ya ww mteja afisa wa mikopo aliekujazia fomu na watu wa makao makuu. Nakuhaidi kukushugulikia na upate taarifa sahihi juu ya mkopo wako siku ya jumatatu. Chakufanya naomba nitumie majina yako matatu na check number yako. No yangu 0717696744. Tunaomba utusamehe kwa changamoto zote zilizotokea wakati wa mkopo wako.

Usitoe number za siri, au utambuliasho wako wowote ule kupitia njia ya mtandao. Ogopa matapeli...
 
Kiongozi wangu kila mtumishi anakitengo chake so kwa kitengo changu mi nadili mikopo kwa watumishi wa serikali. Majina ya abc hotel na back yametokea kufanana tuu lakini havina uhusiano wowote katika umiliki
 
Ungeongezea kwa kusema mmiliki wa banc ABC ni Atlas Mara, kampuni ya yule jamaa tapeli aliyefukuzwa barclays kwa kuyumbisha LIBOR kutokana na udanganyifu. Banc ABC inafanya vizuri sana nadhani nchi mbili tu; Botswana na Zimbabwe.
Kwa Tanzania performance yake ni mbaya mno, losses kila mwaka. Kwenye balancesheet ndio kwishney kabisa, maana mikopo mibovu ( Non Performing Loans) ipo juu sana.
Kuna kipindi cha nyumba benki hii ilikuwa mufilisi (yaani Techically Insolvent).

Naona Atlas Mara wamekomaa hawataki kufunga biashara Tanzania. Lakini kwa mwendo huu wasipofanya restructuring ya management ikiwa ni pamoja na kufukuza baadhi yenu basi wamekwisha.

Mfano mdogo tu ni kwako utajitambulishaje mitandaoni kiboya boya namna hiyo? Hamna kitengo cha marketing and PR? Hao ndio ilitakiwa watokee kwenye social media ku- neutralise negativity zote zinazorushwa na wahanga wa huduma zenu.
 
Usitoe number za siri, au utambuliasho wako wowote ule kupitia njia ya mtandao. Ogopa matapeli...
Na inaonekana anaitwa william mkumbo ni nibrahisi kulitumia jina na Namba mfanano
 
habari wadau wa JF? Mimi ni member mzuri wa jukwaa hili kwa kusoma na kupata mawazo mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yananisaidia kama mjasiriamali mdogo kwa kiasi kikubwa.

Mbali na kuwa mjasiriamali lakini pia Mimi ni mtumishi wa umma katika kusukuma gurudumu hili la maisha ya kila siku.

Katika harakati zangu za mihangaiko niliomba mkopo wa mtumishi kutoka banc ABC ili inisaidie katika shughuli zangu mnamo November 06, na niliahidiwa kupata mkopo wangu baada ya Siku NNE hadi saba toka Siku ya maombi ya mkopo.. kinyume chake ni kwamba hadi Leo hii tar 24 nwezi DEC sijapata mkopo huo kama nilivyoahidiwa halafu kibaya makato ya mkopo yameshaanzwa kukatwa katika mshahara wangu.

nunefanya mawasiliano na afisa mikopo katika tawi nililoomva mkopo kanipa namba ya makao makuu lakini hakuna jibu la maana wanalonipa imefika hatua wote hawapokei simu yangu. Nimeanza kuhisi labda hawa watu ni matapeli au nimetapeliwa kwa namna Fulani..

kama kuna yeyote ana experience ya hawa jamaa hebu anijuze na mwenye kujua nifanye nini nipate haki yangu tafadhali nisaidieni jamani.

Ni vema Watanzania tukaanza kuzitumia mahakama zetu ipasavyo! Tuache kulalamikia mitandaoni!

NB: peleka mahakamani hao!
 
Wamejipotezea credibility yao tayari. Kwenye kipindi hiki cha utandawazi ukimfanyia mteja kitu kidogo tu taarifa zinasambaa mara moja na kupoteza wateja. Review kutoka kwa wateja zinaongea sana kuliko kujitangaza.

Sijui ninani atakayewaamini kwa yanayosemwa huko. Watu wengi wanaofungua account au kuchukua mikopo mikubwa ya biashara huwa wanaangalia credibility ya bank kwanza.

Hawa watu wajirekebishe otherwise wataishia kufunga biashara watakapokosa wateja kabisa.

Nasubiri huyu amalize hili na ABC na mie nilete la Advanced Bank.Maana ni zaidi ya ujuavyo.

Na sio hao tu,hivi vi bank vinatatizo na matatizo makubwa saana,na sio siri wanatumia uelewa duni wa Watanzania ili kupiga
 
Naomba pia utujibu maswali yetu
owner wa bank hii ni kina nani?
pale kariakoo kwenye tawi lenu kuna ABC hotel na ABC kitu gani sijui
ni kampuni moja?

zile pesa za Obama alizowapa muwakopeshe wajasiriamali..zilienda wapi?

Hahahaha,

Ila mkuu vi bank vingi Owners ni watu wa Nje kama sikosei Advanced Bank Owner ni Wageni.

Na inawezekana kuna vigogo wana hisa chini ya mwamvuli.
 
Ni vema Watanzania tukaanza kuzitumia mahakama zetu ipasavyo! Tuache kulalamikia mitandaoni!

NB: peleka mahakamani hao!

Share za wakubwa mkuu.,
Kabla ya kwenda Mahakamani kuna kitengo BOT cha kushughulikia matatizo baina ya mteja na bank husika,ila wao nao ndio yale yale ya Magufuli kuwaotea.Watakuambia kwamba kwanza waandikie Bank yako barua ya malalamiko,hahaha,then ikipta zaidi ya mwezi hujashughulikiwa ndio wao uwajulishe.
Cha kuchekesha sasa,ukiwaandikia BOT kwamba muda mliosema umeisha,wanakuambia Banki yako imekujibu,unakuta Bank hizi ndogo zenye matatizo haya nao wanajua kucheza na akili za Kitengo hiki cha BOT,ukipeleka barua wanakuji tunaishughulikia,ikikaribia muda wanakurusha kutoka hatua moja kwenda nyingine ili wakuzingue.
Ukirudia BOT unaambiwa tunayo copy na tatizo lako Bank husika inalishughulikia,inaweza kufika hadi mwaka halijatatulia,so BOT sio siri hawana msaada wowote kwa wateja wadogo wenye kufanyiwa uonevu na hizi Banks.

Kuna madudu kibaooooo,maofisa mikopo ndio usisemeee.

Hapa issue ni Waziri wa fedha kutoa Tangazo kwenye vyombo vya habari ili wananchi wachangie na watoe maoni yao juu ya utendaji wa hivi vi bank,aisee yaani kuna vingine vitaumbuka.
Kwa ufupi matatizo ya Kibank kwa mfumo huo sio bahati mbaya,ila ni makusudi.
Yaani mtu unaweza kwenda pale bank na wanatabia ya kukariri sura,basi ukifika tu kila mmoja anakubadilikia.
Mie walinipa kali kuna siku mtu alikuwa na matatizo basi waliona anawazingua muda mwingi,Pale advance Bank wakampambanisha mteja na jamaa eti Ni senior staff,tena mswahili ila alikuwa anapiga English tupuu,halafu secretary anatafsiri,sasa kumbe yule mama kiingereza kimo ila akajifanya kachokaa hajui kitu.Na kusema kwamba yule ni mswahili ila wanataka kujifanya wananipagia staffs wapya kila siku ili kuy buy time.
 
Aissee kweli Ukistaajabu ya Advance Bank utayaona ya ABC Bank.

Hivi vi bank Waziri mpya avifuatilie,aisee kuna utendaji wa kihuni sijawahi kuona.
Sijui nani anavibeba.Maana haya BOT wanajua na dawati lao ukiwaandikia wanakuimbisha vile vile,sijui mpaka malalamiko yako yafike mwezi naa sijui miezi ndio wao wakusaidie.

Ujanja mwingiii,sasa wale wasiojua ndio wanapigwa vibaya,maafisa wa vibank hivi wengi wasanii kupita maelezo,full ujanja ujanja,maneno mengiiiii,sometimes mikwala kwa wale wasio na ufaham

Aisee chief kumbe advance bank nayo ni full uswahili?
 
Jina zuri ila waswahili na utapeli mwingi.

Kusanya nyaraka muhimu nenda kawafungulie kesi mahakamani.

Wakulipe fidia si chini ya 50M.

Namshangaa hata mimi ! hii ni kesi imenyooka kabisa. Tena waachie wakukate tu hata kwa miezi sita.
 
Back
Top Bottom