tuwe wakweli
JF-Expert Member
- Feb 15, 2014
- 223
- 59
kabla sijakushauri zaidi ningependa kujua unataka kufuga kwa namna gani hao kuku mkuu?
ufugaji huria, wa ndani au ndani-nje ?
kwa ufugaji wa ndani (intensive system), kitaalam inatakiwa kuku wanne au watano kwa kila mita moja ya mraba.
eneo (area) la banda lako ni 3m x 10m =30m sqr. ukizidisha kwa 5, (30x5) utagundua unatakiwa kuwaweka kuku 150 humo.
kadri unavowaweka wengi kupita uwezo wa banda (overcrowding) ndivo unavowahatarisha kuambukizana magonjwa hasa yanayoenezwa kwa njia ya hewa.
kwa ujumla zingatia usafi, ukavu na kuwe na mzunguko wa kutosha wa hewa. Naamini waweza amua cha kufanya mkuu
ndio walewale ... mkuu kwa mfano unataka kufuga nje, yaani kuku wanalala bandani usiku mchana wanashinda nje ya banda, kuku wangapi wanashauriwa kwa square metre? Ahsante mkuu.
kwa nje inakua 4m sqr kwa kuku mmoja. (una exchange tu figures), waweza vuka zaidi ya hapo maana kwa ufugaji huria/wa nje hewa ya kutosha ni obvious ipo. kitu muhimu kuzingatia ni usalama wa hao kuku, pawe mbali kidogo na makazi (wasije haribu mali za majirani), chakula kiwepo hilo eneo (wadudu, mabaki ya mazao, majani n.k) ili wawe wanajiokotea (scavenging), kua makini na wale wanaotaga (wasitage porini au kwa majirani). Asante.
Mkuu nahisi umechanganya kdg,umesema 4 sqm kwa kuku mmoja? ebu njoo tena
Ubarikiwe sana mkuu maana umenifungua