Banda la kuku 250

Banda la kuku 250

tuwe wakweli

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
223
Reaction score
59
Heshima kwenu wadau.
Nina banda ambalo urefu ni mita 10 na upana ni mita 3.Malengo yangu ni kufuga kuku wa kienyeji 250 wa mayai nikitarget kupata at least tray 7 per day.
Swali,1:je ukubwa wa banda hilo unakidhi haja?
2:Kip niboreshe kutimiza ndoto? THANX
 
kabla sijakushauri zaidi ningependa kujua unataka kufuga kwa namna gani hao kuku mkuu?
ufugaji huria, wa ndani au ndani-nje ?
 
kwa ufugaji wa ndani (intensive system), kitaalam inatakiwa kuku wanne au watano kwa kila mita moja ya mraba.
eneo (area) la banda lako ni 3m x 10m =30m sqr. ukizidisha kwa 5, (30x5) utagundua unatakiwa kuwaweka kuku 150 humo.
kadri unavowaweka wengi kupita uwezo wa banda (overcrowding) ndivo unavowahatarisha kuambukizana magonjwa hasa yanayoenezwa kwa njia ya hewa.
kwa ujumla zingatia usafi, ukavu na kuwe na mzunguko wa kutosha wa hewa. Naamini waweza amua cha kufanya mkuu
 
Ubarikiwe sana mkuu maana umenifungua
 
ndio walewale ... mkuu kwa mfano unataka kufuga nje, yaani kuku wanalala bandani usiku mchana wanashinda nje ya banda, kuku wangapi wanashauriwa kwa square metre? Ahsante mkuu.
 
Last edited by a moderator:

kwa nje inakua 4m sqr kwa kuku mmoja. (una exchange tu figures), waweza vuka zaidi ya hapo maana kwa ufugaji huria/wa nje hewa ya kutosha ni obvious ipo. kitu muhimu kuzingatia ni usalama wa hao kuku, pawe mbali kidogo na makazi (wasije haribu mali za majirani), chakula kiwepo hilo eneo (wadudu, mabaki ya mazao, majani n.k) ili wawe wanajiokotea (scavenging), kua makini na wale wanaotaga (wasitage porini au kwa majirani). Asante.
 
Mkuu nahisi umechanganya kdg,umesema 4 sqm kwa kuku mmoja? ebu njoo tena
 
sijachanganya mkuu, ufugaji wa nje unahitaji eneo kubwa kiasi, kuku mmoja anatakiwa kutawala eneo la mita 4 za mraba katika uzururaji wake. Kwa lolote, kuwa huru kuuliza / ku'share. Asante
 
ahsanteni sana wanajf mimi ninahitaji kuingia katika biashara hii ya ufugaji wa kuku hasa hawa wa kienyeji nimekamilisha kila litu ikiwemo kutengeneza banda na utaalam wa kisasa ila kwa bahati sijapata pa kununua hao kuku wa kienyeji wenye uhakika kwa hapa DAR ES SALAAM.
naomba kwa yeyote wenye kujua wapi wanapatikana kuku hawa ani PM tuweze kuwasiliana
NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU WOTE.😛oa
 
Riwa alimaanisha kama humo bandani wakiamua walale tu idadi itaongezeka au ni walewale kuku watano kwa sqr mita 1?
 
Back
Top Bottom