Banda la kuku lipo tayari. Kuku wepi wanalipa?

Banda la kuku lipo tayari. Kuku wepi wanalipa?

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Salaam wakuu.

Nipo Moshi Mkoani Kilimanjaro. Ninaplan ya kuanza ufugaji wa kuku.

Nimejenga banda la matofali ya kuchoma lenye urefu wa mita 9 kwa mita 4 na kimo cha mita 2.3. Limeezekwa kwa mabati na ukuta nusu wa mbele nimeweka wavu mgumu kwa ajili ya ventilation.

Limesakafiwa vzr na kuzibwa sehemu zote za wazi juu ya paa na maeneo mengine ili kutoruhusu wadudu /viumbe wengine kupenya.

Nimezingushia fensi (iliyowazi juu) kwa mbele yenye urefu wa mita 5 na upanda wa mita 4.

Kwakifupi banda limeshakamilika na limegharimu TZS 1.3 Milioni.

Naombeni ushauri wa aina gani ya kuku naweza kufuga ili nipate faida nzuri.

Mwanzoni nilikuwa na wazo la kufuga kuku wa kienyeji na nitakuwa natotoresha vifaranga kwa incubator yangu yenye uwezo wa kuchukua mayai 200.

Naombeni ushauri ndugu zangu.
 
Yani umejenga banda hujui aina ya kuku unaotaka kufuga hauna tofauti na yule dikteta wa chato aliyenunua ndege bila kujua atazipeleka wapi matokeo yake zimelala tu pale airport
 
Nimejenga zuri la kuaccomodate kuku aina zote. Siyo vibaya kuomba ushauri.
Yani umejenga banda hujui aina ya kuku unaotaka kufuga hauna tofauti na yule dikteta wa chato aliyenunua ndege bila kujua atazipeleka wapi matokeo yake zimelala tu pale airport
 
Yani umejenga banda hujui aina ya kuku unaotaka kufuga hauna tofauti na yule dikteta wa chato aliyenunua ndege bila kujua atazipeleka wapi matokeo yake zimelala tu pale airport
Leo Airbus A 220-300 itatua saa 8 mchana JNIA Dsm.
 
Salaam wakuu.

Nipo Moshi Mkoani Kilimanjaro. Ninaplan ya kuanza ufugaji wa kuku.

Nimejenga banda la matofali ya kuchoma lenye urefu wa mita 9 kwa mita 4 na kimo cha mita 2.3. Limeezekwa kwa mabati na ukuta nusu wa mbele nimeweka wavu mgumu kwa ajili ya ventilation.

Limesakafiwa vzr na kuzibwa sehemu zote za wazi juu ya paa na maeneo mengine ili kutoruhusu wadudu /viumbe wengine kupenya.

Nimezingushia fensi (iliyowazi juu) kwa mbele yenye urefu wa mita 5 na upanda wa mita 4.

Kwakifupi banda limeshakamilika na limegharimu TZS 1.3 Milioni.

Naombeni ushauri wa aina gani ya kuku naweza kufuga ili nipate faida nzuri.

Mwanzoni nilikuwa na wazo la kufuga kuku wa kienyeji na nitakuwa natotoresha vifaranga kwa incubator yangu yenye uwezo wa kuchukua mayai 200.

Naombeni ushauri ndugu zangu.
Aina ya kuku inategemeana na mambo mengi...
Malengo yako ya muda mfupi au mrefu
Wateja wako wanatumia Sana kuku Aina gani
Soko lako ni mayai au nyama, nyama ya kienyeji au chotara au kizungu? Mayai ya kizungu au kienyeji au chotara?
Kuna mikoa hapa Tanzania soko la broiler ni dogo Sana hivyo ukitegemea soko la ndani huna budi kufuga kuku wa kienyeji au chotara kama hitaji kubwa ni kuku wa nyama.
Kuku chotara wana faida mara mbili, mayai na nyama pia uzao endelevu kama utatotolesha mayai kwa njia ya incubator au ukawachanganya na wa kienyeji watakaokuwa wanalalia kuendeleza kizazi, hapo nazungumzia sustainable ufugaji wa kuku...fikiria chotara zaidi maana wana faida zaidi ya nyama na mayai
Ukifuga layers yaani kuku wa mayai specifically maana yake utategemea kupata mayai pekee baada ya kuku hao kuanza kutaga takribani miezi sita tangu azaliwe...kuku hawa wa mayai wanataga vizuri hivyo ukiwafuga Mia wakianza kutaga hutopata mayai zaidi ya idadi Yao isipokuwa pungufu ya idadi Yao kwa sababu tofauti tofauti, wakikoma kutaga ukaamua uwauze kama nyama hutouza bei kubwa kutokana na mauombo Yao na soko Lao hivyo utakuwa umefaidika kwa kuuza mayai...sasa jibu unalo mahali ulipo kipi kitakufaa.
Kuku wa nyama au broilers ni zao la muda mfupi takribani wiki tano unaanza kuwauza na bei Yao haizidi au haifiki kabisa elfu kumi kwa kila kuku ndani ya huo muda, ni biashara ya haraka changamoto soko mahali ulipo linasomekaje maana kuna mikoa nje ya Dar hawa kuku hawana soko kabisaaaaaa.
Kuku wa kienyeji pia ukikusanya mbegu nzuri nzuri bado wana soko mikoa karibia yote ya nchi hii, ukiwaboreshea mazingira utapata faida ya nyama na mayai yaliyo na bei ya juu kuliko kuku wengine.
Kuku Aina zote wana changamoto za magonjwa mfanano...zingatia kanuni Bora za ufugaji
Kwa pamoja ukitoa faida ya mazao ya kuku kama mayai na nyama pia kuna fursa ya kuuza vifaranga ikiwa wafuga kuku wanaozaliana like chotara na kienyeji, layers na broilers wako limited to their number.
Pia mbolea ya kuku ni faida nyingine tena iwapo utaitumia mwenyewe kwenye kilimo au ukaiuza kwa wananzengo....

Karibu Sana kwenye field isiyo na stress za TRA, TFDA, TBS, and the like, hapa unapambana na afisa kilimo na mifugo tu akiwa mshikaji wako wa karibu kujifunza na kushare uzoefu, ukilisaka soko la ndani na nje Safi kabisa ukiwa vema wanunuzi watakusaka weye tu hauteseki na mgambo.
Kila la heri
 
Back
Top Bottom