Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni kweli jogoo wengi sana kwa makoo 10 jogoo moja linatosha
kawaida ratio ya makoo kwa jogoo ni 7:1
Waungwana kwa wale wenye uzoefu naomba muongozo tafadhali. Nataka kujenga banda kama hilo hapo chini lenye ukubwa wa (5X20). Hivyo nilitaka kujua gharama za ujenzi na vifaa zenye kukaribiana na uhalisia. Shamba lipo Msata njia ya Bagamoyo. Nataka nijenge mapema iwezekavyo kuanzia sasa, tafadhali nishauri!
![]()
Hilo banda ni kubwa sana" Wataalam watakuja.
Ahsante nilishapata msaada kutoka kwa wenye uzoefu na hivi vitu humu humu JF. Wamenipa na breakdown yake yote na wapi nitapata hivyo vifaa vya ujenzi.
Majogoo dzain kama mengi weka jogoo kulingana na idadi ya tetra, jogoo moja wastani wa tetea kumi, majogoo yakiwa mengi tatizo yatakuwa yanacompete kurutubisha mwisho wa siku yataaffect uzalishaji
Kiuhalisia unajua hvyo coz jogoo moja linatakiwa kupanda wastani wa Terra nami kiutaalamu, unapoweka mungu huishia kugombana then urutubishaji unakuwa mdogo, na kama jogoo atawekewa Tetea wengi atashindwa kuwamudu wote
Kwa maana hio ulishajenga hilo banda??
Mkuu bado ila tathmini ya mwanzo imeshafanywa maana kuna mambo zaidi ya kulijenga tu; Uelekeo wa banda, mkwanja vilevile lazima tuupange tusije nikayaingia maji halafu nikashindwa kuyaoga na mengine machache lakini tukianza tu lazima nitoe uzi wa mrejesho kuanzia kusafisha shamba mpaka mfugo unaingia bandani.
Mkuu bado ila tathmini ya mwanzo imeshafanywa maana kuna mambo zaidi ya kulijenga tu; Uelekeo wa banda, mkwanja vilevile lazima tuupange tusije nikayaingia maji halafu nikashindwa kuyaoga na mengine machache lakini tukianza tu lazima nitoe uzi wa mrejesho kuanzia kusafisha shamba mpaka mfugo unaingia bandani.
Mkuu Apolinary umeshafanikiwa kwenye mradi wa kuku? Nami napenda kufuga, naomba nikutembelee/ziara ya mafunzo ili nami nipate ujuzi. Naishi Dar kikazi,ila makazi hasa ni Arusha. Hongera kwa ubunifu.Kwa sasa niko arusha ila ufugaji ninaufanya moshi vijijini kibosho mkuu.