Bandari, ardhi, misitu na maliasili zetu, ni Mali ya URITHI, hazitauzwa wala kukodishwa kwa wageni, kataa wahuni

Bandari, ardhi, misitu na maliasili zetu, ni Mali ya URITHI, hazitauzwa wala kukodishwa kwa wageni, kataa wahuni

Haihitaji Watanzania wote kujua IGA ndio irekebishwe. Kuna Makundi ya kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa. Vinatosha.
IGA ni kanuni tu zilizoingia bungeni ndio maana hata baada ya kuvuja na kuifikia jamii bado DP World walitulia tu kwani walijua hakuna siri yoyote inayoweza kuandikwa kwenye IGA.

Commercial Agreements zilizosainiwa pale ikulu Dodoma ndio nyaraka za kibiashara ambazo ni za siri, haziwezi kwa namna yoyote ile kuvujishwa kwenye jamii.

Iwapo IGA imekuwa ni sababu ya mtu mmoja kufungwa jela, hizi commercial agreements zikivuja serikali itamnyonga mhusika atakayevujisha.

IGA haikuwa na makosa kama tunavyodanganyana mitandaoni, na ilikuwa ni lazima HGA ziwe na tofauti na mkataba uliopita bungeni kwani huko ndio kila kitu kimeandikwa kwa kina.
 
Kwenye #3: Sio kweli kwamba mvua zimenyesha nchi nzima. Hivi nyie watu wa Dar mkoje? Mvua zikinyesha Dar mnaona imenyesha nchi nzima? Na hizo mvua zimenyesha kwa muda gani? Mabwawa yanategemea catchment areas. Catchment area ya Bwawa la Mtera bado haijapata mvua kabisa. Ni Wilaya za Mbarali, Makete, Wanging'ombe na Iringa kwa sehemu. Hizo wilaya bado hazijapata mvua kabisa. Ni kukame kabisa. Bwawa la Mtera ndilo Bwawa la HEP kubwa kuliko mengine only to be second to JNHPP Mungu akiijalia.
TMA: Watanzania tujihadhari na uwezekano wa kuwapo mvua za ernino. Mvua ni mchi nzima inaonyesha, acha uongo tangu Oct.

Biteko: 65% ya umeme unaozalishwa, hautumii gas!!

Kuna mtambo mmoja umeharibika, mwaka wa pili sasa haujatengenezwa.

Ilithibitika pia kuwa maji yalifunguliwa kwenye Bwawa la mtera Ili kuhujumu umeme wa maji.
 
Tafuta video ya kusainiwa kwa mikataba ya bandarini kule ikulu Dodoma, mkurugenzi wa TPA kajibu hoja zako zote.

Kumbuka kuwa DPW wanakodisha hawajauziwa, sawa na TICTS walivyokuwa pale kwa miaka 22, sawa na Swissport walivyokaa uwanja wa ndege tangu miaka ya 1994.

IGA ilipitishwa bungeni haiwezi kufutwa.

Kujenga tujenge sisi Kwa mkopo, halafu kukusanya mapato akabidhiwe mwarabu?

Amewekeza sh ngapi?

Hao wahuni hawatakiwi nchini kwetu.
 
Salaam, Shalom!!

Kuna uteuzi ulifanyika siku ya kusaini mkataba BATILI wa kukodisha URITHI wetu, Bandari Kwa wageni.

Uteuzi huo umekuja na wimbi la Matukio ya kutengeneza wenye Nia ya kutusahaulisha wanaukoo juu ya kilichofanyika.

Jambo muhimu juu ya nini Hasa kilisainiwa kwenye mkataba Ule kimebaki kuwa Siri, Viongozi wetu wa kiimani wamejaribu mara kadhaa kuomba mikataba hiyo Ili waisome na kujiridhisha ikiwa Issues zilizokuwa zikipigiwa kelele zimefanyiwa KAZI au la!!

Hadi sasa, hatujapata majibu, media zimechukuliwa na upepo wa uteuzi na maigizo ya kijana wa chama Fulani.

Tunataka kujua yafuatayo;

1. Je IGA ilifutwa au Bado IPO?

2. HGA zilipelekwa bungeni Ili kuangaliwa UPYA ikiwa zimekidhi SHERIA zetu kama nchi juu ya ulinzi wa Raslimali zetu?

3. Kwanini mgao wa umeme unaendelea ilhali mvua zimenyesha kubwa Nchi nzima?

4. Kwanini Mawaziri walioguswa na tuhuma mbalimbali mf Nishati, ujenzi, Fedha nknk hawajaondoshwa Hadi sasa?

5. Pesa zilozoibwa sawasawa na Ripoti ya CAG katika Halmashauri mbalimbali, zimesharudishwa kiasi Gani Hadi sasa?

6. Je ni sawa Rais kuendelea kuteua wahusika wa Tume ya Uchaguzi, I wapi Tume huru ya Uchaguzi?

7. Kwanini uchaguzi wa MITAA 2024 usisogezwe mbele 2025 Ili isimamiwe na Tume huru ya Uchaguzi na kupunguza gharama ya mara mbili?

Ndugu watanzani, tusikubali kuhamishwa kujadili issues muhimu , kamwe tusikubali kutekwa na maigizo ya chama chakavu kinachowaza uchaguzi bila kusema kimewatumikia wananchi Kwa kiwango Gani!!

Ni hayo Kwa sasa.

Karibuni.
Huo urithi wenu unamsaidia nani hasa?
 
Kukodisha bandari zetu kinyume na matakwa ya wananchi,

Matokeo yake mtayaona kwenye uchaguzi ujao,

Hamtatoboa.
Porojo za kujifariji 😁😁

Sio tuu Bandari tumekuwa tunakodisha kuanzia Madini Hadi mabenki na matokeo yalipatikana.
 
Porojo za kujifariji 😁😁

Sio tuu Bandari tumekuwa tunakodisha kuanzia Madini Hadi mabenki na matokeo yalipatikana.
Mmekua mkikodisha madini sio!!!

Kweli huku upstairs, Kuna walakini!!!
 
Muwe mnataja tuu mnaogopa nini kuna watu wengine uelewa wao mdogo hadi umtajie kuwa ni msoga gang.
Hii nchi inachezewa na familia zisizozidi 10 na mwasisi wa uchafu huu ni yule mzee mfitinishaji wa pale njiapanda, huyo ndiye kawafundisha viongozi wengine kuanza kuiuza nchi kidogokidogo
 
Tuliambiwa mwarabu atamwaga pesa kama njugu kutokana na maokoto ya bandarini, lakini tumemsikia madelu akisema atakopa trilioni 6 kujazilisha bajeti ya mwaka ujao, what a contradiction?
 
Tuliambiwa mwarabu atamwaga pesa kama njugu kutokana na maokoto ya bandarini, lakini tumemsikia madelu akisema atakopa trilioni 6 kujazilisha bajeti ya mwaka ujao, what a contradiction?
HOJA Yako nzuri, naomba niongeze kwenye swali namba 8 hapo juu tafadhali🙏
 
Tuliambiwa mwarabu atamwaga pesa kama njugu kutokana na maokoto ya bandarini, lakini tumemsikia madelu akisema atakopa trilioni 6 kujazilisha bajeti ya mwaka ujao, what a contradiction?
Kumbe ndomana maigizo yanaendelea Ili tusihoji mambo muhimu!!
 
Tulitarajia DP World awe mwarobaini, kumbe kukopa bado kuko palepale na mwananchi bado anakamuliwa tozo.
IPO haja tudai mikataba ya HJA uwekwe wazi Ili tujue nini ni nini!!
 
Wana mtandao wa wasiojulikana
Usiogope. Usiogope, Usiogope.

HOFU ni DHAMBI.

Mungu pekee ndo wa kumwogopa na kumtetemekea, wengine ni WA kiwaheshimu tu.
 
Majizi na Matapeli yameanza kujidhatiti huko kwenye miradi ya Hewa ya Kaa...Carbon emissions Projects
 
Kujenga tujenge sisi Kwa mkopo, halafu kukusanya mapato akabidhiwe mwarabu?

Amewekeza sh ngapi?

Hao wahuni hawatakiwi nchini kwetu.
Uelewa wetu juu ya namna bandari inavyofanya kazi katika dunia ya 2020- ni wa kutakiwa kuendelezwa.

Tuna akili zile zile za Tool Port wakati Rais Samia anawazia bandari ya mfumo wa Landlord Port.

Paul Kagame alipomkejeli Kikwete akimwambia kwamba anaweza kuiendesha Tanzania kwa kutumia bandari tu, alikuwa na maono haya aliyoamua kuyafanyia kazi Rais Samia mwaka huu, tumpongeze kwa kutazama mbali sio kuishia kukejeli vitu ambavyo hatuvifahamu.
 
Back
Top Bottom