mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kwa jiografia ya nchi yetu ilivyo, bandari ndio mlango mkubwa wa nchi yetu wa kuingilia na kutoka. Mlango huu ukimkabidhi mgeni kwa miaka 100, hatuwezi tena kudhibiti kwa ukamilifu kitakachokuwa kinaingia na kitakachokuwa kinatoka. Hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu. Silaha zinaweza kuingizwa nchini kinyemela na zikaishia katika mikono ya magaidi. Siyo siri kwamba nchi za mashariki ya kati ndiko chimbo kubwa sana la ugaidi duniani. Na siyo siri kuwa sehemu kubwa nya magaidi duniani hudai ni waumini wa dini fulani na huwa hawaoni haya kumtaja "mungu" wao na dini yao!
Lakini pia bandari ni mlango mkubwa sana wa kupitishia raslimali kutoka nchini kwenda nje. Hatutaweza kudhibiti nini kinatoka kwa uhakika kama mlango tumemkabidhi mgeni. Mali asili yetu itatoroshwa kwa sana tu!! Mama tunakupenda sana lakini katika hili tunasema HAPANA! Ukilazimisha historia itakuhukumu pamoja na uzao wako!!! Mama Mungu amekupa nyumba (nchi) nzuri yenye kila kitu, halafu unamkabidhi mlango mtu mgeni!!! Mama tunakuheshimu lakini katika hili UMWOGOPE MUNGU!! Dhamana tuliyokupa ni kubwa sana, usiitumie vibaya!! Ukilazimisha kama inavyoelekea naomba ukumbuke kuwa MACHOZI ya Watanzania yana nguvu sana MBELE ZA MUNGU WETU, lazima YATAKUANGUSHA.
Machozi lazima yatutoke, lakini haya machozi tutayatoa kwa MUNGU, tutashitaki kwa MUNGU. Kwa maana tunashuhudia nchi aliyotupa Mungu kama urithi wetu hapa duniani, inataka kuuzwa MBELE YA MACHO YETU MCHANA KWEUPE!! NINAAMINI MUNGU ATATUSIKIA.