Bandari ikiwa mikononi mwa wageni kwa asilimia 100, hatuwezi tena kudhibiti kinachoingia na kinachotoka kwa asilimia 100. Ni hatari kwa usalama wetu!

Bandari ikiwa mikononi mwa wageni kwa asilimia 100, hatuwezi tena kudhibiti kinachoingia na kinachotoka kwa asilimia 100. Ni hatari kwa usalama wetu!

Kwa mtu yeyote makini atatambua kwanini Watanzania tuna Hofu kubwa na Mkataba hasa kutokana usiri mkubwa lakini pia ushabiki mkubwa wakati unajadiliwa na Bunge la Jamhuri ambalo kimsingi ni la Chama Kimoja.
 
TUSIDANGANYANE!! TRA anasubiri aliyeingiza mzigo ajitokeze kwake na documents zake ndio TRA afanyie kazi!! TRA hawezi kujua kwenye meli kuna nini. Ukiletwa mzigo wa silaha kwa mfano, mpokeaji ni bandari, na TRA atafichwa ni nini hicho!! Anayeupokea mzigo physically ni bandari. TRA anategemea uaminifu wa bandari, na mwizi au mtu mwovu siku zote si mwaminifu!!

Jiulize, kama madawa ya kulevya yanaweza kuingia nchini wakati bandari iko mikononi mwetu kwa asilimia 100, je itakuwaje kama haitakuwa mikononi mwetu kwa asilimia 100!!. Lakini pia watu wetu wanahongeka sana tu!!

Unachokisema wewe ni sawa na mtu mwenye nyumba kubwa na ina vyumba vingi na vitu vingi, lakini mlango wa kuingilia akamkabidhi mgeni. Halafu unamwambia mgeni kitu chochote utakachoingiza au kutoa lazima umwonyeshe mtumishi wangu (TRA). Je unategemea siku akiamua kuingiza sumu ya kukuua wewe mwenye nyumba atamwonyesha mtumishi wako kuwa ameingiza sumu? Ni akili matope tu inayoweza kukabidhi mlango wa nyumba kwa mgeni, halafu ikaamini kuwa usalama utakuwapo!!. Hatuongelei kutoa bali tunaongelea KUTOROSHA!! Mtoroshaji ukimkabidhi mlango wa nyumba yako, utakuwa umemrahisishia sana kazi ya kutorosha vitu vya nyumbani kwako, na kuingiza nyumbani kwako vitu usivyovihitaji!!!​
kabla mzigo haujaingia tra anajulishwa na scner ipo chini ya TRA. MELI yoyote kabla haijaingia lazima mtu wa TRA waende kujiridhisha na uhamiaje waende kuwavongea passport ndio meli iingie berth . Manifet inasajiliwa kabla , na meli Inapita scanner. sio rahisi kama uwazavho
 
Wapi kwenye mkataba imeelezwa hivyo? Tupe hicho kifungu
Inaonesha hata huo mkataba hauujui bali unaunga kitu usichokijua. Ni sawa na mtu aliyekodi nyumba halafu mwingine akauliza kwani kuna kipengele kipi kwenye mkataba kinachosema utaitumia hiyo nyumba? Mkataba ni wa kukodisha bandari. Shughuli zote za bandari zitakuwa mikononi mwa mwekezaji!!
 
kabla mzigo haujaingia tra anajulishwa na scner ipo chini ya TRA. MELI yoyote kabla haijaingia lazima mtu wa TRA waende kujiridhisha na uhamiaje waende kuwavongea passport ndio meli iingie berth . Manifet inasajiliwa kabla , na meli Inapita scanner. sio rahisi kama uwazavho
Kama madudu yalikuwa yanaweza kufanyika bandarini wakati bandari iko chini ya serikali, je itakuwaje ikiwa chini ya waqgeni? Hao TRA sana sana wamewekwa kwenye nafasi ya kupokea rushwa kubwa za kimataifa.
 
DPWorld hawana shida tatizo ni kwa viongozi wetu kuweka maslahi yao binafsi mbele.
 
Wenzetu Rwanda ya Kagame wanaona mbali sana ndio maana wanaweka maslahi ya taifa mbele, hata hii reli itakapoisha, wakati sisi tunahangaika na malori wao ndio wataitumia zaidi kwa manufaa ya nchi yao na tukizubaa mizigo itakwenda Rwanda ndipo irudi tena Tanzania kwa kuwa hatuna viongozi wenye nia njema na taifa hili tutegemee Tanzania isiyo na mwenyewe kuwa kama Palestina hapo baadaye.
 
Hili liko wazi na tulishalidokeza na tukatoa mfano wa habari iliyoripotiwa Al jaazera namna wajanja walivyotorosha kiasi kikubwa cha dhahabu ya zimbabwe. Imagine unamweka mgeni getini, atatorosha hadi vijiko vya chai.
Kama hao hao waarabu waliweza kutosha wanyama hai wa porini kupitia uwanja wa ndege Kia,inakuwa vp tukiwakabidhi lango hili kuu la kuingia na kutoka walidhibiti wao. Jamani serikali tafakari hasara nyingi sana mnazoelezwa na wenye nchi Yao. Mnatufanya tuamini kabisa hili ni Dili mnacheza! Toss tafadhalini ndg zetu,msikubali haya mambo kufanyika kijinga namna hii. Wanawadharau hata nyie kitengo muhimu ktk nchi. Waonyesheni kwamba mnajua na mna uzalendo.
 
Sasa
MCHANGA WENYE MADINI ULIOKUWA UKITOROSHWA BANDARINI MIAKA NA MIAKA HADI KIPINDI CHA MAGUFULI JEE BANDARI ILIKUWA INASIMAMIWA NA WAWEKEZAJI??
kama fisi anaweza kumzidi ujanja mlinzi wako wa bucha akadokoa nyama, sasa ukimkabidhi bucha yenyewe itakuwaje?
 
Back
Top Bottom