Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Siku ya leo ni siku muhimu sana kwa nchi za Afrika ya Kati yaani Msumbiji, Malawi, Zambia na Zimbabwe kwani nchi hizi zitaanza kupitisha mizigo yake kwa kutumia reli fupi ya Nacala kuzifikia nchi hizi, je tutarajie nini kwenye bandari yetu ya Dar es Salaam?
CCM ni kikwazo kwa maendeleo ya Tanzania, watakaobisha na wabishe. Tulipopata Uhuru Tanganyika ilikuwa na reli ya Mtwara Nachingwea ambayo kwa ujinga wetu tuliing'oa badala ya kuiboresha.
Kuiboresha reli hii ilikuwa ni kuifanya izitumikie nchi za Malawi kupitia ziwa Nyasa na na Zambia kupitia Kyela ambayo ni jirani ya Zambia kuliko Dar es Salaam, na mbaya zaidi ni nchi kushindwa kuitumia kikamilifu reli ya Tazara kwa kusafirisha mizigo ya Zambia na Malawi, badala yake kujikita eti kuondoa msongamano wa malori ya Tunduma! Hii ndiyo Tanzania inayothamini machawa kwa kuwaona ndio maendeleo ya nchi.
Mwisho kwa wale msiolijua hili, Kigamboni kuna bomba la mafuta kama linalojengwa kwenda Uganda isipokuwa hili linachukua mafuta toka Dar es Salaam kwenda Zambia, watanzania machawa nendeni Mbagala linapopita muone kama juu ya hilo bomba kuna fursa yoyote, linapita Kitunda, Kisarawe, Chalinze, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe, juu ya bomba hilo hakuna fursa zozote na tumeshindwa kulitumia bomba hilo kikamilifu kwa kupeleka mafuta Zambia badala yake tunatumia malori yanayotutia hasara kwa matengenezo ya barabara yasiyoisha pia kusafirisha kiasi kidogo cha mafuta.
Rais Chakwera, Nyusi na Hakainde.