Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Shehena inayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa kasi, kutoka tani milioni 16.27 mwaka 2020/21 hadi tani milioni 27.7 mwaka 2024/25, na kufikia tani milioni 33.7 mwaka 2025/26 rekodi mpya. Hii ni ongezeko la takribani 107% ndani ya kipindi hicho, likiashiria kuimarika kwa ufanisi wa bandari, biashara na nafasi ya Dar es Salaam kama lango muhimu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani.