Bandari ya Dar Es Saalam yazidi kuweka rekodi mpya ya Shehena

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911


Shehena inayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa kasi, kutoka tani milioni 16.27 mwaka 2020/21 hadi tani milioni 27.7 mwaka 2024/25, na kufikia tani milioni 33.7 mwaka 2025/26 rekodi mpya. Hii ni ongezeko la takribani 107% ndani ya kipindi hicho, likiashiria kuimarika kwa ufanisi wa bandari, biashara na nafasi ya Dar es Salaam kama lango muhimu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani.
 
well done serikali sikivu ya CCM chini ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan 🤝
 
Wazee wasiolipa kodi huku wakiendelea kuwanyonya waumini wao kwa gharama kubwa za huduma ,naona wanalia muda huu . wanapewa ruzuku , na kodi hawalipi ila wakitoa huduma ni pesa ndefu .
 
Wale waliokuwa wanasema bandari imeuzwa wako wapi
 
Tuambie mapato yameongezeka kutoka TZS ngapi Hadi ngapi. Na lazima yawe 107%plus vinginevyo tunalishwa matango pori
 
Kwa akili za kisisiemu, bila dp world bandari ya Dar ingebaki na uwezo uleule miaka nenda rudi.
 
Chai 🚮
 
Wale waliokuwa wanasema bandari imeuzwa wako wapi
Kuongezeka kwa shehena mmeleta takwimu Sawa, leteni na takwimu za kiasi gani, mapato kimeingia serikalini tuone kama hamjauza hiyo bandari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…