Ukipita maeneo ya lango kuu la nchi yetu maeneo ya bandari hali sio hali, yaani ni shughuli mwanzo mwisho pamoja na mamlaka husika kufanya kazi usiku na mchana, meli ni nyingi hakuna mfano,yaani bandari yetu iko bize balaa, chombo kinaingia, huku kuna kingine kinatoka kingine kinapakia mzigo kingine kinashusha.
In short bandari yetu iko bizee balaa meli ni nyingi nyingi. Ndio maana ni vigumu kuwaona wale jamaa ambao miaka miwili iliyopita walikuwa wanaleta takwimu za meli hapa kila siku.
Mpaka ninaingia mitamboni hapa kuna vyombo kadhaa vinapkuwa cargo vikiwemo EURO SPIRIT na COSCO SHIPPING na kwa mbaaaalii naziona meli kadhaa zikiwa parking zinasubiri foleni.
Kweli maendeleo hayana chama, Mungu ibariki Tanzania.