Bandari ya Tanga kinara wa uchumi Mkoa wa Tanga

Bandari ya Tanga kinara wa uchumi Mkoa wa Tanga

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Selemani Kakoso, Wamefanya ziara Mkoa wa Tanga kukagua Miradi ya Miundombinu inayoendelea Mkoa wa Tanga

IMG-20250313-WA0026(1).jpg
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya

Akiongea wakati wa Ukaribisho, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian, amesema Bandari ya Tanga imechaachua Moa Tanga. Amesema Bilioni 429.1 zilizowekezwa kwenye Bandari ya Tanga, kumeongeza Ufanisi katika Bandari ya Tanga. Kwani muda wa kuondoa Mzigo katika bandari ya Tanga umetoka Siku sita hadi Siku mbili ikizidi sana ni Tatu huku Idadi za Meli zinazoleta Mizigo zikiongezeka.

"Ziara yako imekuja kipindi ambacho Rais Samia amefikisha miaka minne ya Uongozi. Mkoa wa Tanga ni kati ya Wanufaika wakubwa wa Miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutekelezwa. Uwekezaji wa Bilioni 429.1 umezaa matunda makubwa sana kwa sababu imebadilisha Taswira ya Tanga. Hivi sasa Meli zinafika kwenye fukwe za Bahari na Mapato yameongezeka. Amesema Balozi Batilda.

"Mapato katika bandari ya Tanga yameongeza. Kabla ya Uwekezaji 2019 jadi 2020 tulikuwa tunapata Mapato tulikuwa tunapata Bilioni 17.2 na baada ya Uwekezi 2023 hadi 2024 tunapata bilioni 45.69. Hata shehena imeongezeka kutoka tani laki 470 baada ya Uwekezaji Mkubwa na Maboresho tumeanza kupokeza zaidi ya Tani Milioni laki moja laki moja na Sitini. Meli zimeongezeka kutoka 118 hadi 307. Hata muda wa kutoa Mzigo umetoka siku sita hadi siku 3." Ameongeza Balozi Batilda Burian.

Balozi Batilda ameendelea kuipongeza Serikali kupitia TANROADS kwa Uwekezi wa barabara

Balozi Batilda amesema Timu ya Katimu Mkuu Wizara ya Uchukuzi ilifika ili kuangalia uwezekano wa kuhakikisha Reli ya Tanga inaunganishwa Korogwe na Reli ya Kaskazini pia kuna inaunganishwa Ruvu na Reli ya SGR kwani Bandari ya Tanga inategemea sana Wafanyabiashara wa Congo. Uwekezaji wa Tanga unachachua uchumi.

Tanga inaenda kuwa sehemu ya Mafuta gafi kutoka Uganda. Balozi Burian amesema Rais aliekeza pia Mafuta ya Kaskazini yaweze kuwa yanapitia Bandari ya Tanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Miundombinu Mheshimiwa Selemani Kakoso, ameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa Uwekezaji Mkubwa katika Bandari ya Tanga.

IMG-20250313-WA0024(1).jpg
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya kushoto akiwa na Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile

Amesema Ziara ya Kamati nzima itatembelea Uwanja wa ndege wa Tanga, Reli ya SGR, Mradi wa Bandari, barabara ya kutoka Tanga kwenda Pangani itakayounganisha Mkoa wa Pwani kupita Bagamoyo hafi Dar es Salaam na Mradi wa Kivuko Pangani.

"Tunayo Miradi ya Barabara, Mkoa wa Tanga ni eneo la kimkakati la kiuchumi. Mheshimiwa Rais Samia ametengeneza Diplomasia ya kiuchumi kati ya Nchi yetu na Nchi jirani ya Uganda na kuna Bomba la mafuta ambalo linakuja maeneo haya. Bado tunahitaji Uanganishaji wa Bandari yetu ya Tanga ikiwepo Uwepo wa Reli ambayo itasafirisha Mizigo pamoja na Barabara ya Kimkakati ya kutoka Tanga Handeni, Kiberashi hadi Singida". Amesema Selemani Kakoso.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya kwa upande wa Uwanja wa Ndege upo hatua za Mwisho za manunuzi mradi wa ujenzi iweze kuanza. Na Mradi mwingi ni Mradi wa Barabara ya Tanga Pangani, Daraja na Pangani na Kivuko cha Pangani na barabara ya Afrika Mashariki kutoka Tanga hadi Mtwara

Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile ameishukuru Kamati kwa kutembelea Miradi inayoendelea chini ya Wizara ya Uchukuzi. Amesema Ujenzi na Urejeshaji wa reli ya Kaskazini itaongeza Uchumi wa Tanga.

Ziara ya Kamati ya Miundombinu Mkoa wa Tanga itakuwa ya Siku Mbili na baada ya hapo Itaenda Dar es Salaam.

ZIARA YA BANDARINI TANGA ILIVYOKUWA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imesema imeridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Bandari ya Tanga hasa baada ya maboresho makubwa ya miundombinu yaliyofanywa na Serikali Bandarini hapo.
IMG-20250315-WA0022.jpg

Kauli hiyo ya Kamati imetolewa tarehe 13 Machi,2025 na Mwenyekiti wake Mhe. Moshi Kakoso (Mb) baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea na kukagua miradi ya maboresho na miundombinu ya Sekta ya Uchukuzi katika Mkoa wa Tanga.

“Tunatoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Rais, Wizara ya Uchukuzi na TPA kwa maboresho makubwa ya miundombinu yaliyofanyika katika Bandari ya Tanga. Bandari sasa ufanisi unaonekana na mapato yameongezeka, hakika tumeridhishwa”. Amesema Mhe. Kakoso.

Mhe. Kakoso pia amesema kamati yake itaendelea kuisaidia TPA ili kutimiza maono ya Mhe. Rais na kufikia malengo yao na Serikali kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile (Mb) ameishukuru Kamati kwa ziara yao iliyowawezesha kujionea kazi kubwa inayofanywa na Serikali Katika Sekta ya Uchukuzi. Aidha Mhe. Naibu Waziri Kihenzile ameihakikishia Kamati hiyo kuwa maoni, ushauri na maelekezo waliyoyatoa yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha Mkoa wa Tanga unafunguka zaidi kiuchumi kupitia maboresho yanayoendelea kufanywa Miundombinu ya Uchukuzi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.Plasduce Mbossa, amesema kukamilika kwa awamu mbili za maboresho ya Bandari ya Tanga kwa gharama ya shilingi Bilioni 429.1 kumekuwa chachu ya maendeleo na
ufunguo kwa ushoroba wa Kaskazini.
IMG-20250315-WA0026.jpg

“Manufaa mtambuka ya Bandari ya Tanga yatapelekea maeneo yanayozunguka bandari kufunguka kiuchumi hivyo ushirikiano na wadau wote ikiwemo Kamati yako Mheshimiwa Mwenyekiti ni muhimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa”. Amesema Bw. Mbossa.

Pia Bw. Mbossa ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya miundombinu kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa TPA ili Mamlaka iweze kutekeleza mipango ya kuboresha miundombinu ya Bandari na kuwa chachu ya Maendeleo ya Uchumi wa Taifa. Aidha amesema TPA inathamini ushirikiano inaoupata kutoka Serikalini, Bunge na Wadau wote wa Sekta ya Bandari na itaendelea kusimamia bandari ya Tanga ili iendelee kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.

 
Back
Top Bottom