Bando za data Vodacom zinaisha kwa kasi ya ajabu, tatizo ni nini?

Labda Kuna app inarun background. Jaribu kuchunguza simu yako kwa umakini
 
Mitandao ya simu tumeamua kuwa vyura viziwi. Mtalalamika hapa, mtaishia hapa, na kesho mtarudi hapa kuendelea kuperuzi huku sisi tukizidi kuwaibia. Hakuna la kutufanya.
 
Kuanzia jana usiku na leo kutwa nzima hili jambo limetokea kwenye halotel, nimeunga MB 245, nikaingia sofa score kuangalia matokeo ya michezo mbali mbali, dakika 10 MB zikaisha. Zijaperuzi app nyingine yoyote. Nawapotezea kwanza naenda tigo.
 
Saa zngne ukute sio hata bando ni background apps ambazo bdo zinarun so lazma data iende muwe mnafanya uchunguzi kabla yakulalamika
Mimi zote zipo off hebu acha ujuaji, wanatuibia
 
Hata zilizopo hazifanyikazi
 
Hii hali nilijua kwangu tu hasa jana na Leo voda n majambazi yasiyo tumia silaha
 
Nilifikiria ni mimi peke yangu kumbe hata wengine mna experience the same ,naona labda sababu waziri NI Mpya kwenye wizara Kwa hivyo wanataka advantage ,yaani nilikuwa nikiweka mb zangu Kwa matumizi yangu yakawaida hata siku tano sasa hivi kidogo unatumiwa massage Kwamba umefikia 75% ya matumizi yako hii sio Sawa kabisa naomba service provider chonde chonde mliangalie hili Kwa jicho la tatu tunawamini naomba msituangushe.
 
Duu bora wewe umetumia lugha laini labda watakusikiliza
 
Nenda sehemu ya setting, kisha nenda applications kisha kagua kila app nenda walipoandika data usage zima background data kwa kila app

Sometimes unapoeka bando kuna app zinafyanza data hata kama hujaigusa kwaiyo wewe utasema wamekutapeli kumbe ni mafaili yako tu

Kuna siku nilikuwa nacheki euro kupitia simu nikaweka bando 1GB aisee ile kuplay dk3 bando limeisha nikaenda kuchungulia kwenye data usage ile app ya michezo imefyonza 800mb

Kwaiyo hatuzulumiwi na mitandao ila application nyingi zinafyonza mbs
 
Wizi mkubwa sana yaani per day unashangaa 1G inakata kimasihara dawa kususa huu mtandao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…