Bangi haina madhara yoyote kama tunavyoaminishwa, iruhusiwe

Kaka yangu ameathiriwa na matumizi makubwa ya uvutaji wa bangi. Kaanza kuvuta bangi tangu mimi niko mdogo hadi sasa amezeeka maisha yake ni ovyo sana, hana mke ,hana mtoto, hana kwake ,yeye ni mtu wa kutangatanga kwa ndugu jamaa na marafiki.....mara leo yupo hapa kesho pale keshokutwa kule, haeleweki.

Pamoja na kuwa ni mtu mwema sana lakini ukikaa nae utagundua huyu mtu bangi imeshamuathiri, anavuta kama tumbaku vile, popote anasokota bangi lake analiwasha anavuta bila kujali.

Akishalivuta sasa! ana stories za maendeleo ya Dunia nzima. Anakwambia atatengeneza michongo ya hela atajenga nchi yake ambayo raia wake watakuwa ni watu wasio jiweza, walemavu, wazee, wajane, yatima na wanyonge. Atawalisha na kuhakikisha mahitaji yote muhimu wanayapata kwa gharama zake yeye.

Bangi sio aseeee
 
Kabisa chief
 
Ukipata Bangi kali nzuri stiki moja inatosha sana kuwa high

ukivuta zaidi ya hapo ni kujichosha mwili
 
Kuna koo kuvuta bangi ni mwiko

inawezekana huyo bro ako ni mmoja wao jaribu kufanya tafiti 🤔
 
Hayo ni ma
Tatizo yake tu
 
Wewe na yeye wote hamjaeleweka,

Maana hata wewe hujatupa data ya tafiti kuwa ni kivipi inasababisha ukichaa, Na ushahidi kuwa hao ndugu zako ukichaa wao ulisababishwa na bangi
 
Mnachanganya mambo sana, hapa inazungumziwa tiba ya bangi, lakini watu mnaingiza wavuta bangi thread haiwezi kuwa na maana wala kuelimisha bangi inatibu vipi.

Kuna watu wapo kwenye maumivu makali sana bangi ndio tiba sahihi kwa cronic pain hapa hatuzungumzi kuvuta bangi au wavuta bangi.
 
Nadhani wewe unataka kutengeneza maana yako,

Mtoa mada kaidadavua kwa namna anavyoifahamu bangi pamoja na faida zake...

Sasa kwanini useme wachangiaji wanachanganya mambo ?

Maditation ni tiba ? Kufukuza wachawi ni tiba ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…