Bangi Meru yawaponza OCD, OCCID, DSO. Rais Magufuli awaondoa | Amthibitisha James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya

Bangi Meru yawaponza OCD, OCCID, DSO. Rais Magufuli awaondoa | Amthibitisha James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Rais Magufuli wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule amewaagiza wakuu wa vyombo vya usalama nchini kuwaondoa Mkuu wa Polisi wilaya ya Meru na Mkuu wa Usalama wa Wilaya Meru kuondolewa maeneo yao ya kazi kutokana na kukithiri kwa zao la bangi bila kuchukuliwa hatua madhubuti.

Rais Magufuli amesema haya...

“Nimekuona jana au juzi ulikagua kijiji kwa kijiji na kukuta gunia za Bangi, sasa IGP nataka mkuu wa Polisi wa Meru aondolewe, DSO wa Meru aondoke, maana yake hawakutimiza wajibu wao, haiwezekani mtu atoke Dar aende akakamate Bangi Meru wakati wao wapo”

OCCID wote watoke, ikiwezekana washushwe cheo maana hatuwezi kwenda kwenye utaratibu huo. Na wewe wa Kitengo cha Madawa nakuthibitisha leo


Pia, Rais Magufuli amemthibitisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji, kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, leo Julai 06, 2020.

Huyu Kamishna wa Madawa ya Kulevya siwezi nikamuapisha hapahapa?, tengenezeni kiapo haraka mkimaliza nimuapishe sitaki kurudi tena hapa

james.jpg
Rais Magufuli akimuapisha James Wilbert kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini.
 
Wakati Rais Magufuli akiwa anawaapisha Wakuu wa Wilaya, Mikoa na Wakurugenzi wapya leo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, ameoneshwa kutoridhishwa na utendaji kazi wa vyombo vya usalama wilayani Arumeru.

Hii ni kufuatia Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Madawa ya Kulevya kutoka Makao Makuu Dodoma na kwenda Arumeru kuendesha msako wa kukamata dawa za kulevya aina ya Bangi, ambapo alifanikiwa kukamata shehena ya madawa hayo.

Hali imepelekea Rais kumuagiza IGP, kuwatumbua OCD na OCCID wa Arumeru kutokana na uzembe na kutoridhishwa na utendaji kazi wao. Pia Rais amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TISS, kumuondoa DSO wa Arumeru kwa uzembe huo.

Kufuatia baadhi ya wajumbe hao wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Arumeru kuondolewa, Meenyekiti wao ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jerry Muro ajiandae wakati wowote ule kwanzia sasa, anaweza akataumbuliwa.

Ukiona wenzako wananyolewa wewe tia maji!
 
Back
Top Bottom