Pili, nilijifunza kuwa kuna hoja nzito na za kisayansi za kutetea matumizi ya bangi; na kwa upande mwingine wa shilingi, hoja nyingi za kupinga bangi hazina mashiko katika sayansi ya tiba.
Ndiyo maana sikushangaa pale Bunge (la chini) la Uruguay (Congress) lilipopitisha muswaada kuhalalisha bangi; na naamini Bunge la juu (Senate) pia litaafiki ifikapo Oktoba, mwaka huu.
Uruguay itakuwa imeungana na majimbo ya Washington na Colorado ya Marekani yaliyotangulia kuhalalisha bangi kama kiburudisho kwa watu wazima. Pia, majimbo 17 ya Marekani yamelegeza sheria dhidi ya bangi kwa kuruhusu kutumika kama dawa.
Msuba, hashish, hemp, marijuana, cannabis, reefer, hash, pot, sigara pori ni machache kati ya majina mbadala (a.k.a) ya mmea bangi, unaosadikika asili yake ni Asia ya Kati na umekuwa ukitumika kwa miaka kati ya 3,000 5,000 iliyopita.
[FONT=Verdana, Geneva, Arial, Bitstream Vera Sans, DejaVu Sans, Meiryo, Hiragino Kaku Gothic Pro, MS PGothic, Osaka, sans-serif]hii nime nukuu na kuja na hoja zangu[/FONT]