Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Dhalimu na aliyejaa dhuluma - tuulize watu wa Bukoba.
Jiwe ni Kiongozi Muovu na Muongo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jiwe ni Kiongozi Muovu na Muongo.
hivi mkuu unatania au ni kwel kabisa kayasema na kuyatenda haya?!!!!!Nilimalizia kwa kusema kuwa, 'anaweza kuwa na sifa nyingine lakini tusiwe na uthibitisho wa moja kwa moja'.
Kwenye ukatili, nadhani ushahidi wa wazi upo. Kuwabomolea nyumba watu ambao hujui watalala wapi, kutumia michango ya wahanga wa tetemeko kwa mambo mengine na siyo ya kuwasaidia wahanga moja kwa moja.
Kukosa hekima, nakubaliana nawe. Kwenda kuwasimanga watu waliopatwa na tetemeko, eti ukimwi umeanzia kwao, vita ya amini ni wao, na sasa tetemeko kwao, n.k. Yale siyo maneno ya kiongozi mwenye hekima kwa watu wanaoomboleza. Asante kwa kuongeza hizi sifa nyingine zenye uthibitisho wa wazi.
Sent using Jamii Forums mobile app
kwa hiyo mpaka leo hujui kwa nini watu wema waling'ang'ana lissu akatibiwe nairobi badala ya daslam? hujui kwa nini mwanaccm mwenzio aligharamia mamilion ili mtu mwema Lissu akatibiwe nje ya nchi na si ndan ya nchi?Ndege za private za kukodi Tanzania mbona ziko kibao kwa nini akodi Kenya aache za watanzania ambazo ziko kibao
Mwenye picha atuwekee wengine hatujalionaLipo mkuu kuuubwa ameshika viganja vyote hivi Kama kweli...na green imeng'aaaaaaaaaaaa
Kuna watu wamevaa miwani ya mbao na kuweka pamba masikioni. Hawasikii wala kuona mbele ya JPMhivi mkuu unatania au ni kwel kabisa kayasema na kuyatenda haya?!!!!!
na kama ni kwel mkuu hivi kuna mtu atakayempa kura mtu aina hii kwel hata kama ni mwanaccm?!! ili nini hasa?
Yaani una ndugu malofa kweli kweli.Nimewaambia ndugu zangu kama 30 hivi kwamba wakichagua ccm wasije wakaniambia wana tatizo lolote nikalitatua. Na uzuri wamenielewa baada ya kuwapa darasa la nguvu.
Nashauri wagombea wa ccm waache kubeba watu kwa malori alafu tuweke uwiano nani anajaza watu kwa hoja na wasiwepo wasanii kwenye majukwaa
utakuwa haujamsoma mleta mada mpaka mwisho...ameeleza kwa ushahidi wa matukio yaliyofanyika, kifupi kamvua nguo yesu wa lugola!.Na wewe unaongea bila hata kutuonyesha kizibiti
Nami nililiona huko. Ina maana halipo sehemu nyingine?Namimi nimeliona shinyanga nikashangaaa sana
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Mh Rais anatisha aisee ile siku anacheza singeli Singida alivyonyanyukaa tuu high table wotee mbiooo naoo wakanyanyukaa kwa spidi ya umeme na kucheza nae.
Nikasema duhh hii shughuli pevuu
Mkuu, hata Bashiru na Polepole na bila kumsahau kada P. Mayalla wakilisoma bandiko hili, hawana utetezi kabisa!Duuh...aisee Mkuu kwa huo ushahidi na kwa namna ulivyojenga hoja zako, kupinga andiko lako kunahitaji utafiti wa muda mrefu sn.
Mkuu huyo si kiongozi kiongozi hawi hivi. Pia ni mwizi na fisadi.
Atakuwa amemaliza yake haina shidaIngekua ni enzi zile, ungeongeza na haya maneno " Pia ni dhalimu! Nduli"" ha ha ha ha! Very very interesting.
All in all, siku ya Magufuli kuondoka madarakani, ndipo atakapogundua sura halisi za wasaidizi wake wengi wanafiki na wachumia tumbo wengi walio mzunguka.
4/Ni diktetaNdugu yangu Bams, naona umesahau kuorodhesha sifa zake hizi...
- Ni kiongozi katili
- Ni kiongozi anayekurupuka
- Ni kiongozi asiye na hekima
Awe mnyenyekevu kwa kila kitu ili mpige dili vizuri.?
Kuna bango moja la mgombea wa kiti cha Urais, Mh. Magufuli linasema eti Magufuli ni mnyenyekevu!
Nilipoliona bango hili, nikashtuka sana. Nikajiuliza maswali mengi:
1) Ni Magufuli mwenyewe amehiari kuwepo kwa bango la namna hiyo?
2) Kuna watu fulani wameamua kutengeneza bango hilo, labda kwa kumdhihaki Magufuli?
3) Au Magufuli amewaeleza kuwa endapo akichaguliwa safari hii anataka awe mnyenyekevu?
Kuwa 'mnyenyekevu' au kwa kiingereza kuwa 'humble', tafsi yake:
Unyekenyekevu hutokana na neno kunyenyekea. Anayenyenyekea huitwa mnyenyekevu. Kama Magufuli ni mnyenyekevu, ni lazima tujiulize, huwa anamnyenyekea nani?
Kunyenyekea ni kujishusha. Kunyenyekea ni kuamini wewe si kitu mbele ya yule unayemnyenyekea. Kunyenyekea ni kuonesha kuwa ama wewe ni duni mbele ya yule unayemnyenyekea au zaidi ni kuwa upo sawa na yule unayemnyenyekea.
Kunyenyekea maana yake ni kuwa msikivu. Kunyenyekea ni kuwa tayari kupokea ushauri, maelekezo na matakwa ya unaowanyenyekea.
Sasa tujiulize, hivi kweli Rais Magufuli anazo hizi sifa? Bila ya kutafuta majibu toka kwa watu wengine, nina hakika Magufuli hatakuwa amependezwa na bango linalosema yeye ni mnyenyekevu maana mara kadhaa kwa kauli yake na kwa matendo yake amekataa kabisa kuitwa "mnyenyekevu".
Rais Magufuli amewahi kutamka yafuatayo:
1) Mimi sibadilishwi na yeyote, mimi jiwe. Maana yake yeye hapokei ushauri wala maelekezo kutoka kwa yeyote
2) Mimi ukinishauri, ndiyo umeharibu kabisa, maana sitafanya unachonishauri
3) Wewe Mpina ni kichaa mwenzangu, endelea hivyo hivyo
Mtu mnyenyekevu, ni mtu mwenye huruma, kwa sababu anaamini kuwa wale anaowanyenyekea wanastahili kuthaminiwa na kuheshimiwa utu wao.
Mara kadhaa Rais Magufuli amefisha utu wa watu wengine na kuwaonesha kuwa ni takataka mbele yake. Baadhi ya kauli na matendo yake:
1) Huyu Kabudi na Mpango, hawawaambii tu, nilikwishawaambia ni mapumbavu mara nyingi tu
2) Huko Marekani ulikokuwa ulikiwa unafanya upumbavu huu (aliambiwa mkurugenzi wa halmashauri ya Tunduru)
3) Kuna watu walikuwa wanaishi kama malaika, nitahakikisha wataishi kama mashetani (anapenda watu wateseke. Wala hakusema kuwa kuna watu wanaishi kama mashetani, nataka nao waishi kama malaika. Yeye anapenda watu wapate taabu)
4) Kwenye utawala wangu, tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote (maana yake anaweza kumwonea mtu kwa sababu tu ni tajiri. Yaani kuonesha kuwa yeye ni bora kuliko watu wote kiasi cha kuweza kumfanya mtu chochote bila ya kujali mtu huyo ana kosa au hana kosa)
5) Wa Mwanza msiwabomolee nyumba zao kwa sababu walinipa kura nyingi (kama hukumpa kura, ina maana ni halali kubomolewa nyumba yako. Haamini kuwa kuna mtu mwingine yeyote mwenye haki sawa na ya kwake ya kuweza kupigiwa kura)
6) Kamdai maji mbunge wako uliyemchagua au mume wako (alitamka Tunduma dhidi ya mama aliyemwambia wana tatizo la maji)
7) Ninyi mlichagua mbunge mpinzani ndiyo maana siwezi kuleta maendeleo (aliwaambia wananchi wa kule Lindi)
8) Tetemeko halikuletwa na Serikali wala CCM. Hakuna serikali inayowajengea nyumba wahanga wa matetemeko (aliwaambia wahanga wa tetemeko la ardhi)
9) Serikali haina shamba (aliwaambia wananchi waliomba chakula baada ya mazao yao kufa kwa ukame)
Magufuli anaamini kuwa wananchi wengine ni duni kuliko yeye, hawastahili kuwa viongozi, bali yeye na wale tu ambao yeye anawataka.
Ukimtazama Magufuli, matendo yake na kauli zake, bila ya ushabiki, ungeweza kumtafsiri kwa majumuisho yafuatayo:
1) Ni kiongozi mbabe
2) Ni kiongozi mwenye majivuno
3) Ni kiongozi anayejiamini kupita kiasi
4) Ni kiongozi mwenye dharau
5) Ni kiongozi asiyependa kusikiliza, kuelekezwa wala kushauriwa
6) Ni kiongozi asiye na huruma
7) Ni kiongozi asiyejali
Na kila moja katika hizi sifa 7, kuna au kauli au matendo yanayotoa uthibitisho. Anaweza kuwa na tabia nyingine pia lakini kunaweza kusiwepo na uthibitisho wa moja kwa moja.
Swali langu, hivi kusema Rais Magufuli ni "mnyenyekevu", walioandaa bango hili, wanamdhihaki, wanawadanganya wananchi, au limewekwa kwa lengo gani? Maana Rais Magufuli, kwa hakika ni kinyume kabisa cha Unyenyekevu, na wala hata yeye haipendi hiyo tabia ya unyenyekevu. Watanzania tuache unafiki, tumwelezee mtu katika uhalisia wake.