Akaunti ya dollar zina gharama tofauti na za Tshs. Makato ya kila mwezi yanatofautiana benki moja na nyingine lakini ni kati ya usd 10 hadi 30.
Pia ukienda kutoa pesa unakatwa kulingana na kiasi unachotoa. Pia ukiweka pesa endapo ni zile ndogo ndogo kama usd 1, 5, 10 au 20, unakatwa gharama za kuweka hizo pesa kwa akaunti yako.
Tukirudi kwenye swali lako, nenda equity hawana makato ya kila mwezi na kufungua akaunti ni mara moja ukiwa na vitu wanavyohitaji. Kitambulisho cha taifaau cha kupigia kura.
Japo na wenyewe wanakero zao ndogondogo lakini kwa akaunti ya USD wako vizuri. Zingatia hautapewa ATM kadi, vinginevyo wawe wameshaanza kutoa hivi karibuni.