Habari za majukum wakuu?
Naomba kufahamishwa ni taasisi zipi au Bank zipi zinatoa mikopo, hadi milioni mia moja,
Karibuni kwa michango yenu.
Benki zote kubwa na ndogo zinatoa hiyo 100M. Inategemea na wewe ikiwa unakopesheka.
Nasema kwamba unakopesheka kwa maana hii.
1. Unataka kuifanyia nini na una nini mpaka sasa kitakachowashwashi wakupatie hiyo mia.
2. Uzoefu wako katika kile kinachokusukuma kukopa
3. Haujwahi kukwepa kulipa deni katika taasisi za fedha
4. Una dhamana ya kudhamini huo mkopo ukishindwa kulipa inauzwa kufidia deni. Unaweza pia kuwa na mdhamini akaweka mali zake.
5. Anuani ya kazi yako na ya makazi pia.
Kwa kuanzia hakikisha hivo vigezo unavyo.
Sasa tembelea FINCA, NMB, CRDB, BARCLAYS, EXIM, KCB, AKIBA na benki zingine nyingi utapata huduma na gharama zao za mikopo (riba) zinatofautiana. Wapo wanakusubiri tu kukipatia hizo pesa ukikidhi vigezo.
ONYO: PESA YA MKOPO SI YA KUFANYIA STAREHE, UTADUWAZWA