Bank kutuma pesa kimakosa

Bank kutuma pesa kimakosa

Naomba wenye kujua wanijuze hili, kuna bank furani ilituma pesa kimakosa February 1 katika account yangu... na baada ya kuchukuwa statement ikaonekana na mshahara uliolipwa kutoka kaasisi furani. (Mimi sio muajiriwa wa taasisi yoyote).

Baada ya siku tatu wakanipigia simu kupitia mtu wa bank wakitaka niwarudishie pesa yao maana wakadai walifanya makosa ya kibank.. nikawarudishia pesa yao tena kwa kutuma kwenye account ambayo wao wallpa wakidai ndiyo ya mteja ambaye alipaswa kuwekewa pesa hiya.

Sasa nashangaa tena mwezi huu wametuma pesa kama ile ile.... nawaza je ni kweli wametuma kimakosa au kuna kamchezo wanakajua wao? Naomba mwenye kujua anijuze tafadhari.
Pesa ikitumwa kimakosa na Benki kuwasiliana na aliyetumiwa kimakosa ni jukumu la Benki kurekebisha/ kureverse hilo kosa. Kitendo cha wewe kupigiwa simu na kupewa akaunti sahihi ya kupeleka hizo pesa siyo sahihi, unaweza kuingia mtegoni kwa mchezo mchafu labda unaofanywa na huyo anayekupigia simu. Nenda kauone uongozi wa Tawi na waeleze hilo tatizo.
In Tanzania, if a bank mistakenly credits a customer's account and the customer withdraws those funds, the legal implications are as follows:


  1. Bank's Obligation to Protect Consumer Assets: Financial institutions are responsible for safeguarding consumers' assets against fraud, misappropriation, or misuse. If a loss occurs due to such issues, the institution must promptly refund the consumer, unless the consumer's negligence or fraud is proven.
  2. Customer's Responsibility: If a customer knowingly withdraws funds credited in error, this may be considered fraudulent behavior. The customer could be required to return the funds and may face legal action for misappropriation.
  3. Dispute Resolution Mechanism: Financial institutions are mandated to have mechanisms for handling consumer complaints and disputes. If a customer disputes the bank's claim regarding the erroneous credit, they should first utilize the bank's internal complaint resolution process. If unresolved, the matter can be escalated to the Bank of Tanzania's Complaints Resolution Desk.
  4. Regulatory Oversight: The Bank of Tanzania oversees financial institutions to ensure compliance with regulations, including the protection of consumer rights and the integrity of banking operations.

In summary, both the bank and the customer have specific obligations under Tanzanian law. The bank must protect consumer assets and address errors transparently, while the customer is expected to act in good faith and return funds not rightfully theirs. Legal consequences may ensue for customers who knowingly exploit such errors.
 
Nenda kwa branch manager, keep records za barua kuomba kufanywa marekebisho kuzuia tatizo.
Andika barua hardcopy au email kisha tunza sehemu salama.
Kuna siku unaweza kujikuta upo mikononi mwa vyombo vya sheria mfanyakazi hewa unaibia pesa taasisi fulani, au umepokea fedha ya ufisadi ukatakiwa urudishe au ukapewa kesi ya uhujumu uchumi.

Unaweza pia kupewa kesi ya kutakatisha fedha.
Kuna mtu anafanya makusudi.

TATIZO JF UONGO MWINGI, unaweza kukuta hii habari so ya kweli unapiteza muda kutoa ushauri.
Ahsante kwa ushauri mzuri sana, pia kilichotokea ni kweli kabisa.. maana kwa mara ya kwanza nilichukulia kawaida na kwa maelezo yao ya awali waliniambia account yangu na ya mteja wao zimetofautiana herufi moja tu.. kwaiyo nikaona kawaida ndio maana niliwarudishia bila kuwaza sana...sasa imanishtua jana jioni pesa inaingia tena.... na sijaigusa kwa chochote... nikaanza kutafuta kwanza ushauri njia salama ya kukomesha ilo tatizo ili nisijeingia kwenye shida nisiyoijua.
 
Naomba wenye kujua wanijuze hili, kuna bank furani ilituma pesa kimakosa February 1 katika account yangu... na baada ya kuchukuwa statement ikaonekana na mshahara uliolipwa kutoka kaasisi furani. (Mimi sio muajiriwa wa taasisi yoyote).

Baada ya siku tatu wakanipigia simu kupitia mtu wa bank wakitaka niwarudishie pesa yao maana wakadai walifanya makosa ya kibank.. nikawarudishia pesa yao tena kwa kutuma kwenye account ambayo wao wallpa wakidai ndiyo ya mteja ambaye alipaswa kuwekewa pesa hiya.

Sasa nashangaa tena mwezi huu wametuma pesa kama ile ile.... nawaza je ni kweli wametuma kimakosa au kuna kamchezo wanakajua wao? Naomba mwenye kujua anijuze tafadhari.
Kuna upigaji hapo huenda wanakutumia wewe bila kujua
 
Wewe warudishie tu mkuu. No matter what usiingie kwenye mtego. Haiku cost kitu kuwarudishia. Ila itaku cost usipowarudishia.

Kingine mkuu usibadili r na l. Una r kali sana!
Hapa kuna jambo. Hawa watu watakuwa wanapiga ela wanaipitisha kwake kama malipo halafu yeye anaito huenda anaituma kwa mmoja wao. Hapa hakuna makosa. Inabidi achukue hatua zaidi
 
mkuu ndio safari ya jela kimasihara hiyo..kuna watu wanafanya money laundering kupitia ww na kwa vile umesema ni malipo ya mshahara ina maana wahasibu huko wametengeneza payrol fake ya wafanyakazi hewa wakishaweka hela kwenu wanarudi kuzidai uzitume kwenye account tofauti..ukute hata huyo anaekupigia simu wala sio mtumishi wa benki au ni mshirika wao na pengine benk haina habari ya kinachoendelea..hao jamaa siku wakikamatwa upelelezi wa polisi utawafikisha hadi kwako kwani uchunguzi utaonesha na ww ni mtuhumiwa utaunganishwa kwenye kesi ya wizi na kutakatisha pesa hiyo ni miaka 30 jela.! ulifanya kosa la hatari kuituma hela tayari ushauziwa kesi..muamala wowote unaoingia kwenye account yako usiurudishe ww ni hatari wawasiliane na benki..huo muamala wa pili ukaushie tu ila nenda karipoti benk hiyo account inayokutumia fedha na hata kosa ulilofanya mara ya kwanza waambie benk pia kama inawezekana wa iblock hiyo account isiweze tuma hela tena kwenye account yako la sivyo ni suala la mda tu utenda jela kwa kesi usiyoijua si unajua msoto wa mahakama zetu kalenda zao mpaka uchomoke uwe umesota sana.!
 
Thanks, na kwanini wanipe account nyingine ndio niitumie kurudisha pesa yao..? Kwanini wao wenyewe wasitoe iyo pesa wakatuma wanakotaka kutuma?
Umekuwa mshirika kwenye uharifu. Kwa kifupi wametumia akaunti yako kuiba pesa mahali, kwa kuwa hili linahitaji muda na uchunguzi, mpaka ufanyike na kugundulika watakuwa wameisha tajirika wakati wewe mwenye akaunti ukiingia matatani.
 
Hili suala ni kweli
Hata mm limenitokea mwaka juzi nilipokea mara mbili kutoka benk moja
Na wiki iliyopita nimepokea kutoka benk nyengine
Tofauti yangu na mtoa mada mm hazioneshi ni za nn
Mara ya kwanza nilipigiwa cm,baada ya ushauri wa mtu wa benk,nikaambiwa nisilipe hadi bank iliyotuma watazirudisha kwao wenyewe kupitia mfumo
Kitendo cha kuwalipa waliogiga cm haitakiwi,kwa sababu watenda kusema hawajapokea,nikaziacha mpaka nikazitumia sikupigiwa cm tena
Za juzi pia nimeziacha na mpaka leo hii sijapigiwa cm yyt
Na sina acc katika benk hizi,wananitumia kwenye cm yangu tu,ila ujumbe unakuja ni kutoka bank
 
Wewe warudishie tu mkuu. No matter what usiingie kwenye mtego. Haiku cost kitu kuwarudishia. Ila itaku cost usipowarudishia.

Kingine mkuu usibadili r na l. Una r kali sana!
Ana 'r' kali sana zinazoumiza masikio🤣🤣🤣
 
Mkuu kula pesa hyo na Wala usitishwe na kiberenge yeyote,

Hukumpigia simu yeyote kumwomba pesa wala kumpa acc aweke pesa.
Kula pesa Kaa kimya.
 
Rudish
Naomba wenye kujua wanijuze hili, kuna bank furani ilituma pesa kimakosa February 1 katika account yangu... na baada ya kuchukuwa statement ikaonekana na mshahara uliolipwa kutoka kaasisi furani. (Mimi sio muajiriwa wa taasisi yoyote).

Baada ya siku tatu wakanipigia simu kupitia mtu wa bank wakitaka niwarudishie pesa yao maana wakadai walifanya makosa ya kibank.. nikawarudishia pesa yao tena kwa kutuma kwenye account ambayo wao wallpa wakidai ndiyo ya mteja ambaye alipaswa kuwekewa pesa hiya.

Sasa nashangaa tena mwezi huu wametuma pesa kama ile ile.... nawaza je ni kweli wametuma kimakosa au kuna kamchezo wanakajua wao? Naomba mwenye kujua anijuze tafadhari.
a ndugu hizo helà hazijawahi mwacha mtu salama kakaa

Nov 6 saa 05pm. Niko na jirani Yangu pub Moja hiki kisanga wewee

Akasikia msg..kuangalia akakuta imetumwa mil 4.5 kwenye simu yake akaniita PEMBEN

NKAMWAMBIA mpigie mhusika mwambie Niko pub ninywe ngapi narudisha helà zako


Akaniona fala akawahi kawe AKATOA helà

Ukweli sikuacha kuzitumia maana nimejua wajibu wangu nimemwelekeza kama kaamua woi

Akanipa lakimoja

Akanihesabia 4.2. Br kaniwekee home kwako
Hiki kilak 2 tukiwashe woiii NKAMWAMBIA ajwa

Nkawahi home nkazificha.. nkarudi pub tukaagiza mbuzi PEMBEN kukaa Shiba nkamshauri kaka nipe nizidhek niwe nalipa bill wanakuletea hamad akanipa...nusu saa tukaanza kunywa
Sasa sisi wanywabia kwa akili tunajua kesho..NKASEMA hapa tukianza beer zinaishia nkamshauri tuweke konyagi akasema m nani nipinge kaka..nkaita konyagai mbili nkakaribisha wah flan lamba mzigo kaka anakunywa anakunywaa anakunywaaaa weweeee NKAONA ananza kukoroma

Nikaomba dada niandikie billi Saini akanletea nkabaki NAYO...kijana AKAOMBA iitwe bajaji aende home nkampeleka AKASHUKURU sana

Asbh akaamka. Akapigaa kakaaa upoo wapii dah wameniibiaa Salio lote naamka asbh HATA 500 hazipo mfukoni NKAMWAMBIA pole sana m nilitoka baadae nkarudi nkakukuta hoi

Kijana AKAOMBA kwenye mil 4.2 nichukue lak 2 na NDIE nitakuwa nalipa NKAMWAMBIA ajwa

Tukaenjoy kama wiki nzima na Ile helà m na br tu

Wiki inayofwata akaweka mil 2 kwa wanae WA shule nikabaki na mil 2

Wiki yaa tatu nkamshauri twende ukanunue vitabu vya wanao vya mwakani wote watatu..tukanunue na madaftari yao yotee wote watatu...
Tukanunue soksi viatu vyaoa pair NNE NNE wote watatu akanikumbatia dah br unanipenda unapoenda sana wanao

TUKAENDA SEHEMU tukapiga beer tatu akataka ya NNE nkampa HAPO namm nimejipanga kununua na vya wanangu wote wako wawili

Kaka AKAOMBA Naomba ukanunue tu wako form three na four dah .natoka nkaenda elite pale njia ya KWENDA massana

Nkaagiza vitabu vya form two vyote nkaagiza Tena form two vya wanangu

Nkaagiza vya form three ......wanafunzi wawili wangu na wake

Nkaagiza vya form four mtoto MMOJA wake

Nkanunua compass kama zote begizao watoto watano...

Nkanunua daftari makwaya 4 /
11 watoto watano nkalipa

Nkaenda dukani nkanunua soksi pair sita kila mtoto x 5

Bahati PEMBEN kuna MADUKA ya viatu nkanunua pair tatu kwa wanangu wote wake sikuweza sikuwa na namba za viatu

Nkaenda home NKATOA vyangu NKACHUKUA vyake nkarudi bar nkamwonyesha resit nkampa ahifadhi NKAMWAMBIA zimebaki kadhaa akasema bal tunza ..no p

Tukwaita pikipik wakapeleka kwake vitu tutaendelea na mvinyo ukweli kwenye helà mi sinywi beer nakunywa wine nzito red

Siku inayofwata akaja home nkamwonyesha bal AKASHUKURU nkampa akamwita wife akampa laki akaitwa wanangu akawapa 50 wawili
Baba nkaapewa laki Tena HAPO na bal nimehifadhi za kutosha
Akachukua bal akaondoka jion kama kawa akawa ananiita analipa yeye kwa sasa

Niko airport napigiwa naambiwa....kakayako jirani yako kakamatwa eeh..nn we si ULIKUWA unatumia nae kamtoe ..mmh nkafikia home nkaelezewa jamaa ANAKULA monde iKAJA land cruiser ikasimama kwa mbali wakatoa simu ZAO Nje wanazisimamisha baadae WAKARUDISha NDAN cruiser ikawa inasogea kumbe jamaa Wana mtruck gafla walipofika pub wakapiga kuangalia Yuko pale ama maeneo Yale


Kupiga kijana kapokea akasalimiwaa vizuri jamaa wakaenda kupaki wakatoka MMOJA MMOJA KWENDA Pub wakagiza maji soda na mwingine akagiza wine akanywa wakiendelea kunywa wakianza kuuliza unaitwa bwana Brian ndio ..Brian yyyu ndio za kwakoo nzuri..jamaa akamuuliza unanikumbuka hapana ulisoma shule flan ndio nilisoma pamoja...ooh karibu sana

Yaliyofwata ..NDUGU TUNAOMBA ukatusaidie kidogo KUNA pesa ilitumwa simsuyako gafla ikatolewa

BAADA ya kutolewa ukaazima simu eeeh sawa si sawa n sawa s..kwanza tunaka kujua iliobakia sh ngapi akasema mil 1.2 akaombwa azikabidhi akaenda najamaanwakazichukua akakabidhi

NXTY wakaenda nae kituon woi nkazima na mm simu nkasafiri Moshi

BAADA ya wiki nkambiwa NDUGU WAMELIPA mil 2 na wamhaidi kumlipa kiasi flan kila wiki

Jamaa Yuko MTAANI..akaniylizia akambiwa mdogo wako kaenda Moshi hahahaaaa mbona apatikan
Nkachat na wife line ya watu vipi huko akasema AMeTOKA njoo

Nkawasha simu nkampigia akajibu kakaa mahabusu Haina wenyewe nn kaka pole sana sana YAAN siku unachukuliwa nimefiwa NKAONDOKA na special hire usiku...akanielezea kaka tumenjoy helà za watuu zimentokea puani aisee pole sana mkuu

Toka sikuhio nikiona helà siielewi woii narudisha kabisa na BAADA e natumiwa ya ahsante
 
Back
Top Bottom