Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Miaka 20 unalalamika?! Kwanza hufai kukopeshwa wewe. Hujui value for money kabisa.
Miaka 20 unakatwa 650,000 mana yake unaijua mzee. So kama income yako ni 1.2 ukitoa hio ni 5.5 miaka 20.
 
Wasalamu wakuu.
Baada ya hawa jamaa wa benki kuja kutoa semina hapa lindoni kwetu wakanishawishi kweli kweli kupata mkopo wa Kujenga.
Sasa last week nikawaibukia ofisini kwao nikawaambia nataka 40,000,000 nirudishe kwa miaka 20 kama walivosema wao.
Leo nikapigiwa simu kuwa niende nikasaini tayari process zishafanyika. Nilipofika kusoma nikaona kama nimechoka naomba nichukue nikasome taratibu kisha nitarejesha.
Hesabu iko hivi.
Mkopo: 40,000,000.
Riba: 18% (annually)
Monthly payment: 617,325.00
Hapa ukipiga hesabu for 20 year nitalipa
617,325.00 * 12 * 20= 148,158,000/=
Yaani almost 4 times ya hela nilokopa.
Nimeamua kuchoma huu mkataba nimempigia afisa mikopo kuwa sitoweza kusaini aendelee na shughuli zake.
Hapa ndo naelewa wale wanaonunua tofali kila mwezi kuweka kwenye kiwanja.
Bank hamnipati tena.
fuatilia historia ya mabenki duniani,yote yameanzishwa kuwanyonya na kuwakandamiza wanyonge,kwamba watakuja kukunyang`anya hata kile kidogo ulicho nacho
 
Vijana wana vituko sana, yaani hawajui kuwa hawa wafanya biashara wakubwa waliofanikiwa wengi huwa na mikopo mikubwa mikubwa kwenye taasisi nyingi za kifedha?
Hata ukienda Kenya utashangaa vijana wanarejesha mikopo kwa kiwango kikubwa kabisa bila tatizo,lkn Tanzania vijana kila siku wanalialia na ccm
 
kuna mzee wangu mmoja nilimuambia "ukienda kukopa benki milioni 10 alafu ukarudisha milioni 15 ni sawa sawa na wewe unashida alafu ukaenda benki ukawapa hizo milioni 5 bureee kabisa bila wao kutumia nguvu yeyote ile
kwa sababu ile riba yao ni sawa sawa na wewe umewapa hiyo pesa bureee bila wao kutumia nguvu.
kama unaweza kulipa milioni 5 ndani ya mwaka si ungedunduliza na kutunza taratibu tu pesa yako mpaka ifike milipni 5 kwa mwaka then unakuwa umeepuka kuwapa benk pesa ya bure (riba)
Hamjui Kutumia Mikopo. Labda Mnaa Nyota Ya Umasikini.
Vitu Vingine Havilazimishwi.
Acheni Wahindi Watajirike.
Yaani Uchukue Tsh 40M Ya Mtu Ukae Nayo Miaka 20. Unayo Tu:
Kuna:
- Inflation
- Taxation
- Duration
Halafu Unaona Pesa Hiyo Ya Marejesho Ni Kubwa Sana ??!!
 
Mahali hapo sijaelewa,
So mkopo unaoulipa kwa miaka 20 ulitamani urudishe shilingi ngapi katika hilo deni la milioni 40?
Hapo sijaelewa, milioni 40 riba 18%! Sasa mbona ikigawanywa kwa muda huo na hicho kiasi kinakuwa juu Sana? Na ndiyo mwenye mada amepagawa kama vile mimi
 
Nilikopaga bank 10ml aisee mpaka Leo nataabika mbaya hata mapenzi yamepungua nyumbani na wife kuishi kwa 230000 ndani ya mwezi sio mchezo aisee
Wenye mishahara midogo kama 500,000 hamtakiwi kukopa kabisa, kwq sababu watakukata pakubwa, lakini pia mkopo mdogo tu, unaweza chukua miaka mitano na kiendelea.

So, kwa waalimu kukopa ni kutafuta namna ya kuichukia kazi tu, maana utajiona unafanya kazi bure
 
Nilikopaga bank 10ml aisee mpaka Leo nataabika mbaya hata mapenzi yamepungua nyumbani na wife kuishi kwa 230000 ndani ya mwezi sio mchezo aisee
Kwahiyo 10M Ulivyochukua, Ukatupa Chooni.

Maana Hujaonesha Kama Imeongeza Chochote Kwenye Kipato Chako!
 
Hapo mkuu wewe ndio mwenyewe shida.

Mwaka 2000, 1Usd ilikuwa 600Tzs, Leo hii tunaongea 2400Tzs/1Usd. Kwa maana 40,000,000/=Tzs za mwaka 2000 Leo ni 4 x 40,000,000= 160,000,000/=Tzs.

Banks zinaangalia na namna Shilingi inavyopoteza thamani ndani ya kipindi cha mkopo.

Lakini vilevile nyumba hiyo after 20yrs hebu jaribu fikiri itakuwa na thamani ya kiasi gani?

Sikushauri ukope kwa ajili ya kujenga. Kopa kama tayari expert katika biashara. Vinginevyo unajipunguzia kipato chako bila kujua
 
Mkuu miaka 20 urudishe 60?. Mbona ningesaini hapo hapo

Ni benki gani hiyo inayoruhusu wateja wake kukopa kwa muda unaofikia miaka 20? Tufahamishane ili kama vipi wenye roho ngumu tukajilipue. Ninachofahamu benki nyingi kikomo chake kwa sasa ni miaka 6 mpaka 7!
 
Wasalamu wakuu.
Baada ya hawa jamaa wa benki kuja kutoa semina hapa lindoni kwetu wakanishawishi kweli kweli kupata mkopo wa Kujenga.
Sasa last week nikawaibukia ofisini kwao nikawaambia nataka 40,000,000 nirudishe kwa miaka 20 kama walivosema wao.
Leo nikapigiwa simu kuwa niende nikasaini tayari process zishafanyika. Nilipofika kusoma nikaona kama nimechoka naomba nichukue nikasome taratibu kisha nitarejesha.
Hesabu iko hivi.
Mkopo: 40,000,000.
Riba: 18% (annually)
Monthly payment: 617,325.00
Hapa ukipiga hesabu for 20 year nitalipa
617,325.00 * 12 * 20= 148,158,000/=
Yaani almost 4 times ya hela nilokopa.
Nimeamua kuchoma huu mkataba nimempigia afisa mikopo kuwa sitoweza kusaini aendelee na shughuli zake.
Hapa ndo naelewa wale wanaonunua tofali kila mwezi kuweka kwenye kiwanja.
Bank hamnipati tena.
Bank gani hiyo inakopesha miaka 20?
 
Kuna rafiki yangu ni mfanya biashara mkubwa kuna bank wamembembelezea pesa kinoma!
Kachukua mkopo wa milioni 100 kwa muda wa miezi 6,sasa cha kushangaza riba yake ni milioni 6 tu,wakati yeye pesa ameagiza contena ambalo hakosi faida ya milioni 20,ndani ya miezi sita shilingi itakuwa imezaa shilingi,Yaani anasema hadi miezi sita inakamilika atakuwa ashamaliza bank na mfukoni ana faida ya milioni 75,sasa utamwambia vipi mfanyabiashara asikope??
Bank wakiona ni mfanyabiashara mkubwa wanakupa pesa kwa riba Ndogo sana na bila masharti mengi tena kwa kukubembeleza!
Lakini wakiona huelewi chochote kuhusu biashara utapigwa riba hadi na za michepuko yako
 
Mhh Kwa miaka 20 kiwango mbona kidogo sana.
Tuchukue update hizo milion 40 uwekeze mfano kwenye biashara ya utengenezaji wa unga wa sembe.
Kukodi jengo 300000*12'=3600000
Mashine ununuzi =8000000
Kuingiza umeme=2000000
Mifuko grade1 ya kuanzia(2000)=1000000
Mpaka hapo jumla=14600000
Unabaki na 25400000
Toa 25000000 kipind cha mavuno nunua Mahindra utapata kg 40000
TUJE KWENYE UZALISHAJI
Ukijiwekea target kila siku usage tani kumi Kwa wastan wa faida ya 300000 Kwa tani kumi. Hapa bila pumba.
Ukifanya Kwa siku 20 Kwa mwezi,
20*300000= utaingiza 6000000 Kwa mwezi.
Kwa mwaka 12*6000000=720000000
Kwa miaka 20*72000000=1.44bil
1.44bil-147mil=?

TUJE KWENYE DECISIONS
Kwa maono yangu tatizo sio benki Bali maono ya mtu na exposure.
Nipe Mimi hizo nikupe 200mil Kwa miaka miwili Ila au nipe machinery za that amount hiyo nichague eneo la kufanyiwa biashara nikupe mara kumi ya capital yako ndani ya mwaka.
Hakika unakipaji cha Biashara kudos
 
Back
Top Bottom