Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Miaka 20 unalalamika?! Kwanza hufai kukopeshwa wewe. Hujui value for money kabisa.
Miaka 20 unakatwa 650,000 mana yake unaijua mzee. So kama income yako ni 1.2 ukitoa hio ni 5.5 miaka 20.
 
fuatilia historia ya mabenki duniani,yote yameanzishwa kuwanyonya na kuwakandamiza wanyonge,kwamba watakuja kukunyang`anya hata kile kidogo ulicho nacho
 
Vijana wana vituko sana, yaani hawajui kuwa hawa wafanya biashara wakubwa waliofanikiwa wengi huwa na mikopo mikubwa mikubwa kwenye taasisi nyingi za kifedha?
Hata ukienda Kenya utashangaa vijana wanarejesha mikopo kwa kiwango kikubwa kabisa bila tatizo,lkn Tanzania vijana kila siku wanalialia na ccm
 
Hamjui Kutumia Mikopo. Labda Mnaa Nyota Ya Umasikini.
Vitu Vingine Havilazimishwi.
Acheni Wahindi Watajirike.
Yaani Uchukue Tsh 40M Ya Mtu Ukae Nayo Miaka 20. Unayo Tu:
Kuna:
- Inflation
- Taxation
- Duration
Halafu Unaona Pesa Hiyo Ya Marejesho Ni Kubwa Sana ??!!
 
Mahali hapo sijaelewa,
So mkopo unaoulipa kwa miaka 20 ulitamani urudishe shilingi ngapi katika hilo deni la milioni 40?
Hapo sijaelewa, milioni 40 riba 18%! Sasa mbona ikigawanywa kwa muda huo na hicho kiasi kinakuwa juu Sana? Na ndiyo mwenye mada amepagawa kama vile mimi
 
Nilikopaga bank 10ml aisee mpaka Leo nataabika mbaya hata mapenzi yamepungua nyumbani na wife kuishi kwa 230000 ndani ya mwezi sio mchezo aisee
Wenye mishahara midogo kama 500,000 hamtakiwi kukopa kabisa, kwq sababu watakukata pakubwa, lakini pia mkopo mdogo tu, unaweza chukua miaka mitano na kiendelea.

So, kwa waalimu kukopa ni kutafuta namna ya kuichukia kazi tu, maana utajiona unafanya kazi bure
 
Nilikopaga bank 10ml aisee mpaka Leo nataabika mbaya hata mapenzi yamepungua nyumbani na wife kuishi kwa 230000 ndani ya mwezi sio mchezo aisee
Kwahiyo 10M Ulivyochukua, Ukatupa Chooni.

Maana Hujaonesha Kama Imeongeza Chochote Kwenye Kipato Chako!
 
Hapo mkuu wewe ndio mwenyewe shida.

Mwaka 2000, 1Usd ilikuwa 600Tzs, Leo hii tunaongea 2400Tzs/1Usd. Kwa maana 40,000,000/=Tzs za mwaka 2000 Leo ni 4 x 40,000,000= 160,000,000/=Tzs.

Banks zinaangalia na namna Shilingi inavyopoteza thamani ndani ya kipindi cha mkopo.

Lakini vilevile nyumba hiyo after 20yrs hebu jaribu fikiri itakuwa na thamani ya kiasi gani?

Sikushauri ukope kwa ajili ya kujenga. Kopa kama tayari expert katika biashara. Vinginevyo unajipunguzia kipato chako bila kujua
 
Mkuu miaka 20 urudishe 60?. Mbona ningesaini hapo hapo

Ni benki gani hiyo inayoruhusu wateja wake kukopa kwa muda unaofikia miaka 20? Tufahamishane ili kama vipi wenye roho ngumu tukajilipue. Ninachofahamu benki nyingi kikomo chake kwa sasa ni miaka 6 mpaka 7!
 
Bank gani hiyo inakopesha miaka 20?
 
Kuna rafiki yangu ni mfanya biashara mkubwa kuna bank wamembembelezea pesa kinoma!
Kachukua mkopo wa milioni 100 kwa muda wa miezi 6,sasa cha kushangaza riba yake ni milioni 6 tu,wakati yeye pesa ameagiza contena ambalo hakosi faida ya milioni 20,ndani ya miezi sita shilingi itakuwa imezaa shilingi,Yaani anasema hadi miezi sita inakamilika atakuwa ashamaliza bank na mfukoni ana faida ya milioni 75,sasa utamwambia vipi mfanyabiashara asikope??
Bank wakiona ni mfanyabiashara mkubwa wanakupa pesa kwa riba Ndogo sana na bila masharti mengi tena kwa kukubembeleza!
Lakini wakiona huelewi chochote kuhusu biashara utapigwa riba hadi na za michepuko yako
 
Hakika unakipaji cha Biashara kudos
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…