Mr ceragem
Senior Member
- Feb 22, 2015
- 109
- 65
Kwa muono wangu unga mzuri unaanzia kwenye ukoboaji. Mara nyingi naweza kusema ukiwa na mashine ya roller kuanzia tano na ukayabana vizuri mahindi ukija kwenye usagaji no ishu ya chekeche. Kwangu Mimi chekecheo nayotumia ni moja na robo,
Tukija kuwa supplier mkubwa kitu tusichojua Kwa mashine ya size 50 au 75 na mashine ya kukoboa ya roller tatu sitarajii kama utaweza timiza malengo kihaswa maana ili utengenezaji pesa inabid uzalishe Kwa wingi uuze bei ya wastan huku ukipunguza gharama za wafanyakazi.
Kwa ushauri chonga mashine ya kukoboa roller tano mota hp 50 mpya hata za kichina Ila za rpm 1440 na mashine oversize ya kusaga kama unaweza nunua plate mwenyewe kama inchi 12 tafuta fundi akutengenezee. Ukiwa na mashine imara hata ukija weka pulley mfano kwenye mota inch 12 Kwa inchi 3 Kwa mashine utanambia moto wake. Kuna watu nasikia wanafunga mpaka gearbox ili kupunguza ulaji umeme sijawahi kutana na technolojia.
🙏🙏🙏🙏
Nadhani hapo naposema kinu namaanisha kwenye kukoboa na kusaga ikiwa katika hali ya size zote ziwe 75, ila kwenye suala uliogusia la 50Hp ni zuri ila ulaji wa umeme nadhani utaweza kimbia labda kama unavyosea hivyo nija ya kutumia gearbox ambayo ndio maujanja hayo nayapata hapa
Ila pia suala la chekecheo nalo ni muhimu sana