Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Banki sio rafiki kwa Mfanyakazi/mtu wa kipato Kidogo

Kwa muono wangu unga mzuri unaanzia kwenye ukoboaji. Mara nyingi naweza kusema ukiwa na mashine ya roller kuanzia tano na ukayabana vizuri mahindi ukija kwenye usagaji no ishu ya chekeche. Kwangu Mimi chekecheo nayotumia ni moja na robo,
Tukija kuwa supplier mkubwa kitu tusichojua Kwa mashine ya size 50 au 75 na mashine ya kukoboa ya roller tatu sitarajii kama utaweza timiza malengo kihaswa maana ili utengenezaji pesa inabid uzalishe Kwa wingi uuze bei ya wastan huku ukipunguza gharama za wafanyakazi.
Kwa ushauri chonga mashine ya kukoboa roller tano mota hp 50 mpya hata za kichina Ila za rpm 1440 na mashine oversize ya kusaga kama unaweza nunua plate mwenyewe kama inchi 12 tafuta fundi akutengenezee. Ukiwa na mashine imara hata ukija weka pulley mfano kwenye mota inch 12 Kwa inchi 3 Kwa mashine utanambia moto wake. Kuna watu nasikia wanafunga mpaka gearbox ili kupunguza ulaji umeme sijawahi kutana na technolojia.

🙏🙏🙏🙏

Nadhani hapo naposema kinu namaanisha kwenye kukoboa na kusaga ikiwa katika hali ya size zote ziwe 75, ila kwenye suala uliogusia la 50Hp ni zuri ila ulaji wa umeme nadhani utaweza kimbia labda kama unavyosea hivyo nija ya kutumia gearbox ambayo ndio maujanja hayo nayapata hapa
Ila pia suala la chekecheo nalo ni muhimu sana
 
Inaonekana hii biashara ukitulia unaweza piga hela ya maana. Mtaji unaweza kuwa kama kiasi gani kwa mtu ambaye anaanza from scratch?

kwa watu kama sisi ambao twafanya rejareja yaani kukoboa na kusaga kwaajili ya wanamtaa/wanakijiji unatakiwa angalau uwe na kuanzia 8-12 milioni na inategemeana sana na suala la unajenga au unapanga, vile vile mjini au kijiji kwani kuingiza umeme bei ni tofauti kwa mfano kijijini umeme wa 3phase ni Tshs 177,000 ila mjini ni Tshs 900,000 hivi hata kujenga nyumba ya mashine kijijini na mjini ni mbingu na ardhi utofauti wa gharama
 
Ninachoelewa unaweza kukopa kwa Malengo.

Mkopo una faida zake ukitumika vyema na hasara kubwa ukitumika vibaya.

Mfano. Mkopo ni wa kukuza mtaji, na sio utumike kama mtaji, faida utakayopata kwenye biashara baada ya kuongeza mtaji ndio utatumika kufanya shughuli zingine kama kujenga nk
 
Pia mkuu Ze Farmer bihashara yeyote unapiga hela sema yatakiwa kuzingatia vigezo na masharti yake tu la sivyo wenzako watakuwa wanachanja mbuga wewe kilasiku ni mtu wa kuanzisha bihashara mpya na kuhiachia njiani hata mafanikio yake hutoyaona kamwe
 
🙏🙏🙏🙏

Nadhani hapo naposema kinu namaanisha kwenye kukoboa na kusaga ikiwa katika hali ya size zote ziwe 75, ila kwenye suala uliogusia la 50Hp ni zuri ila ulaji wa umeme nadhani utaweza kimbia labda kama unavyosea hivyo nija ya kutumia gearbox ambayo ndio maujanja hayo nayapata hapa
Ila pia suala la chekecheo nalo ni muhimu sana
Sawa nimekupata. Kwenye suala la mashine za kukoboa hatupimagi Kwa size hizo zenyewe zinapimwa Kwa roller zilizopo au njia rahisi ni idadi ya chekeche utazoweka. Kweli kama nia rejareja Kwa 50hp itakumaliza umeme. Kwa sababu hutakuwa unafanya KAZI muda mrefu 30hp inakufaa Kwa kusagia hata ukichukua roller nne Kwa kukobolea itaenda tu kupunguza suala zima la umeme. Ila nasisitiza unga mzuri unaanzia kwenye ukoboaji tu
 
Kujenga chumba kimoja hapa dar es salaam kuanzia msingi mpaka kwenye madirisha ni hela ndogo sana ,ufundi laki 3 ,tofali moja shilingi 1000 zidisha 300 ,bati mbili 50000 na mbao za elfu 30 maisha yanaenda utaendeleza vyumba vingine ukiwa humohumo kwenye pagale lako
 
Yaani ndugu wakupe 2.5M mkuu bilashaka unatokea familia zakina MO wewe....kwa ukiri yako angeenda Bank kama ndugu wanaweza mpa.
Atakua alijichanganya mkuu msamehe au maybe wakishua hao hawajui watu wanatokea iwalanje alafu yeye ndio kafika mjini kuna ukoo mzima umefurahi katusua
 
Wasalamu wakuu.
Baada ya hawa jamaa wa benki kuja kutoa semina hapa lindoni kwetu wakanishawishi kweli kweli kupata mkopo wa Kujenga.
Sasa last week nikawaibukia ofisini kwao nikawaambia nataka 40,000,000 nirudishe kwa miaka 20 kama walivosema wao.
Leo nikapigiwa simu kuwa niende nikasaini tayari process zishafanyika. Nilipofika kusoma nikaona kama nimechoka naomba nichukue nikasome taratibu kisha nitarejesha.
Hesabu iko hivi.
Mkopo: 40,000,000.
Riba: 18% (annually)
Monthly payment: 617,325.00
Hapa ukipiga hesabu for 20 year nitalipa
617,325.00 * 12 * 20= 148,158,000/=
Yaani almost 4 times ya hela nilokopa.
Nimeamua kuchoma huu mkataba nimempigia afisa mikopo kuwa sitoweza kusaini aendelee na shughuli zake.
Hapa ndo naelewa wale wanaonunua tofali kila mwezi kuweka kwenye kiwanja.
Bank hamnipati tena.

Riba za mabenki bado ziko juu sana. Sukuhu ya kupunguza machungu ya Mkopo ni kupunguza muda wa marejesho kwa maana ya kwamba kadri muda wa marejesho unapokuwa mkubwa vivyo hivyo utakapojikuta uanarudisha hela nyingi. Mfano ungekuwa na uwezo wa kuurudusha mkopo huo kwa kipindi cha mwaka mmoja (Miezi 12) basi ungerudisha kiai cha shiingi 44,006,396.59 ambapo kiasi cha shiling 4,006,396.59 kikiwa ni riba ya mkopo wote.
 
kwa watu kama sisi ambao twafanya rejareja yaani kukoboa na kusaga kwaajili ya wanamtaa/wanakijiji unatakiwa angalau uwe na kuanzia 8-12 milioni na inategemeana sana na suala la unajenga au unapanga, vile vile mjini au kijiji kwani kuingiza umeme bei ni tofauti kwa mfano kijijini umeme wa 3phase ni Tshs 177,000 ila mjini ni Tshs 900,000 hivi hata kujenga nyumba ya mashine kijijini na mjini ni mbingu na ardhi utofauti wa gharama
Sawa mkuu subiri nifanye upembuzi wa kina. Shida itakuwa kwenye usimamizi mana mi ni mguj na nyia kutokana na hii shughuli nafanya
 
Riba za mabenki bado ziko juu sana. Sukuhu ya kupunguza machungu ya Mkopo ni kupunguza muda wa marejesho kwa maana ya kwamba kadri muda wa marejesho unapokuwa mkubwa vivyo hivyo utakapojikuta uanarudisha hela nyingi. Mfano ungekuwa na uwezo wa kuurudusha mkopo huo kwa kipindi cha mwaka mmoja (Miezi 12) basi ungerudisha kiai cha shiingi 44,006,396.59 ambapo kiasi cha shiling 4,006,396.59 kikiwa ni riba ya mkopo wote.
Basically sikuwa na nia ya kukopa. Jaa walikuja kazini na kututia upepo mpaka nikajaa mazima. Jamaa anauliza toka umeanza kupanga unamuda gani namwambia 4 years. So hapo on average 4*12*350,000 (kodi) =16,800,000 landlord katafuna. Nikahamasika kumbe ndo naenda motoni
 
Sawa mkuu subiri nifanye upembuzi wa kina. Shida itakuwa kwenye usimamizi mana mi ni mguj na nyia kutokana na hii shughuli nafanya
Ishu sio usimamizi kuna watu kibao unaweza pata wakakufanyia vizuri ili mradi uwe commited na kusiwe na undugulization
 
Kuna Wanaosema huwezi kukuza mtaji bila Kukopa #tushikelipi sasa
 
kuna mzee wangu mmoja nilimuambia "ukienda kukopa benki milioni 10 alafu ukarudisha milioni 15 ni sawa sawa na wewe unashida alafu ukaenda benki ukawapa hizo milioni 5 bureee kabisa bila wao kutumia nguvu yeyote ile

kwa sababu ile riba yao ni sawa sawa na wewe umewapa hiyo pesa bureee bila wao kutumia nguvu.

kama unaweza kulipa milioni 5 ndani ya mwaka si ungedunduliza na kutunza taratibu tu pesa yako mpaka ifike milipni 5 kwa mwaka then unakuwa umeepuka kuwapa benk pesa ya bure (riba)
Ulikua unataka upewe bure...Ndo maana wakaiita interest rate
 
Wasalamu wakuu.
Baada ya hawa jamaa wa benki kuja kutoa semina hapa lindoni kwetu wakanishawishi kweli kweli kupata mkopo wa Kujenga.
Sasa last week nikawaibukia ofisini kwao nikawaambia nataka 40,000,000 nirudishe kwa miaka 20 kama walivosema wao.
Leo nikapigiwa simu kuwa niende nikasaini tayari process zishafanyika. Nilipofika kusoma nikaona kama nimechoka naomba nichukue nikasome taratibu kisha nitarejesha.
Hesabu iko hivi.
Mkopo: 40,000,000.
Riba: 18% (annually)
Monthly payment: 617,325.00
Hapa ukipiga hesabu for 20 year nitalipa
617,325.00 * 12 * 20= 148,158,000/=
Yaani almost 4 times ya hela nilokopa.
Nimeamua kuchoma huu mkataba nimempigia afisa mikopo kuwa sitoweza kusaini aendelee na shughuli zake.
Hapa ndo naelewa wale wanaonunua tofali kila mwezi kuweka kwenye kiwanja.
Bank hamnipati tena.
Ndo Mortgage hiyo
 
Mikopo ina manufaa sana kama ni ya kukuzia mtaji. Mkopo kwa ajili ya jambo lingine lisilo la kibiashara ni maumivu aisee.
 
Kuna rafiki yangu ni mfanya biashara mkubwa kuna bank wamembembelezea pesa kinoma!
Kachukua mkopo wa milioni 100 kwa muda wa miezi 6,sasa cha kushangaza riba yake ni milioni 6 tu,wakati yeye pesa ameagiza contena ambalo hakosi faida ya milioni 20,ndani ya miezi sita shilingi itakuwa imezaa shilingi,Yaani anasema hadi miezi sita inakamilika atakuwa ashamaliza bank na mfukoni ana faida ya milioni 75,sasa utamwambia vipi mfanyabiashara asikope??
Bank wakiona ni mfanyabiashara mkubwa wanakupa pesa kwa riba Ndogo sana na bila masharti mengi tena kwa kukubembeleza!
Lakini wakiona huelewi chochote kuhusu biashara utapigwa riba hadi na za michepuko yako
Nimekuelewa nadhani
 
Kwahiyo 10M Ulivyochukua, Ukatupa Chooni.

Maana Hujaonesha Kama Imeongeza Chochote Kwenye Kipato Chako!
Hawa ndo wale wanakopa na kwenda kujenga mapagale mkuu.. Unategemea ataishije kwa hyo miaka mitano? Lazima achukie kazi. Tofauti kabisa na yule aliye fanya mchanganuo mzuri, halafu akawekeza zile pesa. Baada ya muda mfupi akaanza kupata faida.
 
kuna mzee wangu mmoja nilimuambia "ukienda kukopa benki milioni 10 alafu ukarudisha milioni 15 ni sawa sawa na wewe unashida alafu ukaenda benki ukawapa hizo milioni 5 bureee kabisa bila wao kutumia nguvu yeyote ile

kwa sababu ile riba yao ni sawa sawa na wewe umewapa hiyo pesa bureee bila wao kutumia nguvu.

kama unaweza kulipa milioni 5 ndani ya mwaka si ungedunduliza na kutunza taratibu tu pesa yako mpaka ifike milipni 5 kwa mwaka then unakuwa umeepuka kuwapa benk pesa ya bure (riba)
Yqonekana hujawahi fanya biashara wewe..

Hiyo saving mpaka ifike 5m ingekuwa rahisi si kila mtu angesave....

Unaijua maana ya riba???
Na kwa nini kuna riba??
 
Back
Top Bottom