Banza Stone ana hali mbaya

Banza Stone ana hali mbaya

Sanaa ya bongo nzito,ukitaka kuwa maskini maarufu basi fanya sanaa Tz,huyu jamaa tangu atangaze kuwa siku zake za kuishi si nyingi sikumsikia tena ila Dunia ni mapito ipo siku...

Mkuu una maanisha sanaa gani au ni hii hii anayofanya Diamond, AY, Ally kiba, Mzee Yusuph, Ally choki?
 
Wabongo walivyo wanafiki sasa, japo hatuombei itokee, akifariki ndio utasikia redioni nyimbo zake zitapigwa na kurudiwarudiwa kutwa na wauzaji wa cd watauza sana, na msibani wasanii watajiliza sana na kujifanya wamezimia, utaona miguo imevaliwa mieusii na mamiwani meusi makubwa, kila msanii atakayehojiwa na tv atakuwa na kitambaa cha kufuta machozi na kujifanya wana uchungu mno! Hebu msaidieni Banza leo sio mngijee afe mtafute sifa.

Maneno kuntu haya....
 
Radio Tumaini hawapindishi maneno nilisikia jana kina Gaudence wakielezea hiyo story 96.5 FM.
 
Wabongo walivyo wanafiki sasa, japo hatuombei itokee, akifariki ndio utasikia redioni nyimbo zake zitapigwa na kurudiwarudiwa kutwa na wauzaji wa cd watauza sana, na msibani wasanii watajiliza sana na kujifanya wamezimia, utaona miguo imevaliwa mieusii na mamiwani meusi makubwa, kila msanii atakayehojiwa na tv atakuwa na kitambaa cha kufuta machozi na kujifanya wana uchungu mno! Hebu msaidieni Banza leo sio mngijee afe mtafute sifa.
wamsaidie nini?hela au?teja habebeki,ukimpa hela anannua unga!angekuwa anaumwa ugonjwa natural tungesema sawa asaidiwe,sasa we unataka kumuingilia mtu kwenye starehe yake ya ulevi?!!!
 
wamsaidie nini?hela au?teja habebeki,ukimpa hela anannua unga!angekuwa anaumwa ugonjwa natural tungesema sawa asaidiwe,sasa we unataka kumuingilia mtu kwenye starehe yake ya ulevi?!!!

Sawa kama imeshindikana kumuokoa,basi msijetumia msiba wake kama dili.
 
Diouf alienda kumshtaki Banza kwa Asha Baraka kwamba anawafundisha Aisha na wenzake wawili wa kike,nao ni wacheza show. Banza hiyo kitu akakataa,Diof alikuwa hataki hao mademu wavute nao. Ingawa na yeye alikuwa anatumia. Diouf sasa hivi yuko England,kamfata mama watoto wake.

Baada ya gari kuwaka, Aisha akawa anaenda pale kinondoni anawaomba mapusher wamfungie getto na mzigo apone!
Jamaa wanamhesabia dk kadhaa kisha wanazama ndn wanakula mtungo!
 
hamna cha ukuntu hapo,..jitu zima linajua madhara ya unga utalisaidaje!ni sawa na mimi niende kona bar niopoe changudoa nipige peku halafu walaumiwe rafiki zangu.!!!!

Mbona ray c kasaidiwa au yy ilikua sio drug
 
Mbona ray c kasaidiwa au yy ilikua sio drug

kwa hiyo wote tuvute unga tukitegemea ikulu itatupeleka rehab!mshaurini banza ajiwekee papuchi na macho ya kurembua wapambe wa pale magogoni watamkutanisha na mwajiri namba moja.
 
Asha atakua na tatizo kwenye kumanage wasanii wake...kwanini wanaathirikia kupita kiasi na unga na bangi wakiwa chini yake. Madinda, chokoraa; diof, banza nk. Anasubiri wafe agharamie mazishi? Hawa wasanii wamemtajirisha sana anatakiwa awafanyie zaidi ya kuwatumia tiketi!

Hizi lawama nyingine jamani hebu tuwe na busara walau kidogo....hao kina Ray c, Lord Eyes, Chidi, TID, Daz Baba na wengine wengi nao walipita/wapo kwa Asha ?

Pili..wewe kama mwana jamii nini mchango wako kuzuia hayo....bado hujachelewa, hebu nenda pale Twanga, tafuta wasanii wote wanaotumia unga, kaa nao chini waambie madhara ya kufanya hivyo, na sidhani kama Asha atakufukuza, kisha watafute kina Chidi na wenzake nao uwaelimishe vivyo hivyo.

Hizo za kusema yule ndio anahusika hazisaidii hata siku moja ndugu.
 
kwani mama akipika ugali sharti si uliwe au usiliwe sembe zinatoka kwa mama watoto wanacho kifanya ni kubwia wengine pia ni punda wanabebeshwa haya kalaga baho
 
Mnampa dhambi bure Asha Baraka!Banza anaumwa kifua long time na hata mama mtoto wake Joyce aka mama Haji alishatangulia (RIP)
 
kwani mama akipika ugali sharti si uliwe au usiliwe sembe zinatoka kwa mama watoto wanacho kifanya ni kubwia wengine pia ni punda wanabebeshwa haya kalaga baho

Huu mfano umenifurahisha sana, nimekumbuka enzi za utoto tulivyokuwa tukimyaimu mama yale maziwa ya unga. Akitoka dakika moja tu tayari tumetia hasara. Bila kujali mfuko wa suruali au bukta ni msafi kiasi gani basi maziwa yatajazwa humo ni balaa.
 
Mwajiri wake mpya kauchuna tu kila wiki end tuko naye Meeda pub akituchezesha mtindo wa kizigo.
Ama kweli kachokwa na safari yake imeiva. Atusalimie Aisha Madinda tu.
 
Habari.

Mwenye update kuhusu nguli huyu wa muziki wa dansi atupe.
 
Back
Top Bottom