Kwanza naunga mkono kauli ya RC mstaafu wa Mwanza kuwa "watu wanywe bia maana bia ni uchumi" Lakini pamoja na hilo siku za karibuni kumeibuka mfululizo wa bar ukanda wa mbezi beach ya chini hali inayopelekea mtaa kukosa utulivu hii imepelekea hata baadhi ya wasanii kuhama mjini sinza na kufata viwanja Mbezi beach.
Ongezeko la bar linaweza kuleta vitendo vya uhalifu, mapaka, madawa ya kulevya na kuharibu sifa ya mtaa. Bar zenyewe zinajaa watoto wa shule za kata wanyoa viduku na vidangaji vya kutoka uswahilini Kawe. Ukiondoa Oysterbay na Masaki mtaa unaofuatia kwa ustaarabu na makazi yenye utulivu ni Mbezi beach ila tunapoelekea sasa utakuwa mtaa wa fujo. Mwanzoni zilianza kumbi za sherehe, sasa hivi bar nani anajua kitakachofuatia?
Mipango miji tupeni jicho pande hizi kuna mitaa itunzwe na kuheshimiwa kama makazi mfano Mbezi beach, Mikocheni, Mbweni na Ununio na mitaa mingine ibaki ya starehe kama Sinza, kinondoni, Tabata n.k.
Baadhi ya bar hizo ni:
Rainbow
Juliana
Kidimbwi
Na nyingine nyingi siwezi taja zote wino utaisha.