Bara wabebe mzigo umeme Visiwani hadi lini?

Bara wabebe mzigo umeme Visiwani hadi lini?

Ouch, Mkuu Bin Maryam! Naruhusiwa kukosea ndiyo maana sikuupata uhandisi. Unachosema, Bin Maryam kinaelekea isipokuwa kwa kitu kimoja. Kama Ewura wanapanga bei ya kumuuzia msambazaji wa Zanzibar wangesema hivyo, ili bei atakayolipa mteja iwe baina yao na msambazaji wao. Hii itaondoa dhana kuwa Tanesco wanahusika na bei anayolipa mteja. Au Ewura nayo ni ya muungano kwa hiyo wanahusika kuwapangia bei wenzetu wa ZNZ? Mbona inaelekea nguvu zote wamemuelekezea Tanesco? Hilo la wezi lina ukweli, siwezi kupinga. Asante kwa kunielewesha.

Ninapoishi nipo mpakani mwa state mbili. Nikivuka state moja kwenda nyingine bei ya umeme ni tofauti kwa sababu ya wasambaji tofauti lakini wasambaji wote wanatoa umeme kutoka kwenye kinu kimoja.
 
wabara ni mazuzu na matapeli,kazi yao kufikiria jinsi ya kuiba na mikataba ya ajabu ajabu.
 
Mnajua hili la bei ya umeme ni kati ya miujiza ya muungano, bara imeweka amana kubwa ili muungano usivunjike, na visiwani wao wanataka muungano ufe hata kesho. Sasa basi, kutokana na hiyo rehani ya bara vitu vingi inabidi bara wakae kimya hata kama siyo haki kwani kinachofanyika ni kama wanajaribu kutoa pipi ili Visiwani nao wapunguze kelele za kuua muungano.

Ila siDE alivyosema kidogo kaniacha hoi, kama ni kweli je shiraka la umeme zenji wananunua huo umeme wa jumla bei gani?, kwani kama ni rahisi sana basi hata bara ilitakiwa Tanesco wasiweke faida kubwa hivyo, ila na watanzania wa bara nao waufaidi. - Kutokana na hayo ndiyo maana nahisi kuna kitu kimefichwa, sitashangaa ikija julikana kuwa kuna ruzuku inatolewa kufidia hizo gharama kule visiwani ili tu kuwanyamazisha.
 
Hii hoja is so weak!

Zenj wana tofauti gani na mji kama Moshi au Iringa ktk umeme?

You can argue better than this! Acha siasa ktk umeme!

Ukweli Visiwani wanalipia kidogo kwa kubwebwa na walala hoi Bara!

Kwanza garama kuleta tu umeme toka Kidatu/Kihansi to Zanzibar ni kubwa mara nyingi kwani unapiata baharini- which is another cost!

Ukweli ni kuwa Visiwani wanabebwa na kusaidiwa umeme na Bara!

Tupunguze ushabiki na siasa!

Gharama ya umeme wa KIDATU to ZANZIBAR haikutoka TANESCO wala BARA mkuu, ni ZANZIBAR yenyewe iliolipia gharama zote za kiufundi na vifaa kusafirisha umeme huu, na hitilafu zozote kwenye njia hii ZANZIBAR ndio inawajibika.
 
gharama za kuzalisha umeme ni ndogo sana,lakini
tatizo lipo katika utawala,gharama za adimnistratin ni kubwa sana.hawa ndio wanauwa shirika na kufanya bei ya umeme kuwa juu.
 
Gharama ya umeme wa KIDATU to ZANZIBAR haikutoka TANESCO wala BARA mkuu, ni ZANZIBAR yenyewe iliolipia gharama zote za kiufundi na vifaa kusafirisha umeme huu, na hitilafu

zozote kwenye njia hii ZANZIBAR ndio inawajibika.

Side

prove your claims!

Umeme toka Kidato to Zanzibar ni pesa nyingi- na uchumi Visiwani ni dhoofuu!! Wapi na wapi????

Je hawa Norway wanaleta umeme toka Tanga to Pemba- je hii ni pesa toka Zenj?

Zenj hata madaktari ndo mnawalipa 150,000 wakati bara ni 1,000,000. Je pesa mtapata wapi?

Be a realist! You can argue better!
 
SiDe umeingiza ushabiki tena. Ndiyo maana nasema haya masuala yakiendelea kufichwa kunasababibisha myth kama hizi. Tuelezwe nani alilipa deni la Zanzibar. Mchango wa Zanzibar kwenye Muungano uwekwe wazi na kiasi gani kinabebwa na bara. Kama zanzibar waliwahi kuukopesha Muungano nayo iwekwe wazi. Ingawa Bin Maryam amejitahidi kufahamisha, kama Zanzibar wanatoza chini ya gharama ya uzalishaji(isiyojumuisha usambazaji ambao unajumuisha wizi wa watu wa bara) basi kuna mtu anafidia tofauti hiyo. Hii nayo iwekwe wazi.
 
wakristo wana phrase yao inasema "bwana katoa ,bwana katwaa" ,sasa tanganyika si ndio bwana wa muungano anaecontrol uchumi wa zanzibar namna anavyotaka yeye.hiyo kupanga bei ya umeme hata hainisumbui sana maana huo uchumi wa zanzibar yeye ndio "anatoa na kutwaa". Hata akitupa bure basi bado atakuwa hajaondosha lawama za wazanzibari ambazo wao wanadai haki za msingi na sio faida ya kitu sahali kama umeme! umeme tu umewapandisha mizuka ,sijui kama mngekuwa katika situation ya kama zanzibar(nchi bila benki kuu,rais wa zanzibar kuchaguliwa bara,mawaziri wa zanzibar kukosa kutambulikana kimataifa,uhuru wa zanzibar kujiunga na mashirika ya misaada,zanzibar kukosa kujiwakilisha kimataifa n.k),si mngechanganyikiwa nyinyi?.nakuhakikishieni kwamba kesho zanzibar tukisema tupewe umeme bure au muungano uvunjwe ,basi tanganyika itahiari kutupa umeme bure, kwani umeme is nothing ,kilichofichikana katika muungano ndio something.
 
Tunasubiri waje wajibu wenyewe maana kila siku ni malalamiko tu.
bro. hapa hatulalamiki bali tunadai haki zetu! kama umehisi hii haki ya umeme wazenji wanakudhulumuni basi na wewe simama udai haki yako.mimi na wewe sote ni victims of the system, unapodhulumiwa simama na useme.
 
SiDe umeingiza ushabiki tena. Ndiyo maana nasema haya masuala yakiendelea kufichwa kunasababibisha myth kama hizi. Tuelezwe nani alilipa deni la Zanzibar. Mchango wa Zanzibar kwenye Muungano uwekwe wazi na kiasi gani kinabebwa na bara. Kama zanzibar waliwahi kuukopesha Muungano nayo iwekwe wazi. Ingawa Bin Maryam amejitahidi kufahamisha, kama Zanzibar wanatoza chini ya gharama ya uzalishaji(isiyojumuisha usambazaji ambao unajumuisha wizi wa watu wa bara) basi kuna mtu anafidia tofauti hiyo. Hii nayo iwekwe wazi.
nakubaliana na maneno ya bin maryam na side, na ukiyakutanisha unaona wanaongelea kitu kimoja. ni kweli wanachofanya tanesco ni kuiuzia unit za umeme zanzibar tu, gharama nyengine zote ni up to kidato na shirika la umeme zanzibar , pia shughuli za usambazaji na ugawaji na mengineyo.tukija upande wa tanzania bara, tanesco ndio everything kuhusiana na umeme usambazaji,utengezaji na gharama kadhaa wa kadhaa kama ugawaji na mengineyo.hivyo ukiangalia gharama inazopata tanesco bara na zile inazopata zanzibar hata hazilingani. kwahiyo msiseme mnaibeba zanzibar semeni tanesco ina majukumu mengi bara na kwa upande wa zanzibar ,zanzibar imeipunguzia tanesco baadhi ya gharama na usumbufu na majukumu yasio ya msingi.
 
Under age,
maneno yako kweli lakini brother ebu turudi nyuma kidogo hapa..
Ikiwa tanesco atakuwa na majukumu yote hayo kulikuwa na faida gani kuanzisha kampuni ya umeme Zanzibar? na itawezekana vipi wao kuendesha biashara ikiwa hawana expenses zozote kisha wao ndio wachukue faida.
Ni muhimu Tanesco waishie kuuza umeme kisha hilo shirika la Zanzibar ndilo litakalo amua bei ya umeme Zanzibar, wapi wapeleke na wapi waache na sio maamuzi ya tanesco tena ktk nyumba ya mtu. Kutokana na gharama za usambazaji mnaepuka ukiritimba wa Tanesco ama niseme bara kuingilia ugawaji wa umeme Zanzibar. Kisha mapato ya hilo shirika yanaingia ktk mfuko wa Zanziba badala ya tanesco ambapo makao yao makuu ni bara, wakifunga mahesabu ya mwaka kodi wanalipa bara.
Kwa hiyo mnanunua umeme kwa bei poa sana na kama yapo matatizo basi hilo shirika ndilo la kulishika shati.
 
nakubaliana na maneno ya bin maryam na side, na ukiyakutanisha unaona wanaongelea kitu kimoja. ni kweli wanachofanya tanesco ni kuiuzia unit za umeme zanzibar tu, gharama nyengine zote ni up to kidato na shirika la umeme zanzibar , pia shughuli za usambazaji na ugawaji na mengineyo.tukija upande wa tanzania bara, tanesco ndio everything kuhusiana na umeme usambazaji,utengezaji na gharama kadhaa wa kadhaa kama ugawaji na mengineyo.hivyo ukiangalia gharama inazopata tanesco bara na zile inazopata zanzibar hata hazilingani. kwahiyo msiseme mnaibeba zanzibar semeni tanesco ina majukumu mengi bara na kwa upande wa zanzibar ,zanzibar imeipunguzia tanesco baadhi ya gharama na usumbufu na majukumu yasio ya msingi.

Kidatu ni ya nani? Na wewe unaleta ushabiki. Gharama Tanesco wanayowaliuzia shirika la umeme znz ni chini ya gharama ya UZALISHAJI na haijumuishi gharama za usambazaji n.k. Sasa tofauti kati ya gharama ya uzalishaji na hiyo inayotozwa shirika la huko analipa nani? Naona unachanganya serikali ya muungano na serikali ya Tanzania bara. Mbona bara hawalalamiki pale ambapo mawaziri kutoka unguja wakiongoza wizara zisizo za muungano? Tatizo ni kwamba mmejenga hisia kuwa huu muungano unawafaidia bara tuu bila kuangalia matatizo ya huko kwenu. Tuseme muungano usiwepo hatima ya nchi yenu itakuwaje wakati hivi sasa mmekaliana kooni waunguja na pemba? Muungano usipokuwepo wale wapemba wa sharif shamba watakimbilia wapi? Leo mnatibiwa hospitali za bara wakati za kwenu mmezitelekeza. Au matumaini yenu ni kuwa huo muungano ukikatika hao ankal zenu wa muscat na o.i.c watakuja kuwabeba? Msitukane mkunga wakati....
 
Hata akitupa bure basi bado atakuwa hajaondosha lawama za wazanzibari ambazo wao wanadai haki za msingi na sio faida ya kitu sahali kama umeme! umeme tu umewapandisha mizuka ,sijui kama mngekuwa katika situation ya kama zanzibar(nchi bila benki kuu,rais wa zanzibar kuchaguliwa bara,mawaziri wa zanzibar kukosa kutambulikana kimataifa,uhuru wa zanzibar kujiunga na mashirika ya misaada,zanzibar kukosa kujiwakilisha kimataifa n.k),si mngechanganyikiwa nyinyi?.nakuhakikishieni kwamba kesho zanzibar tukisema tupewe umeme bure au muungano uvunjwe ,basi tanganyika itahiari kutupa umeme bure, kwani umeme is nothing ,kilichofichikana katika muungano ndio something.

Huu ndiyo ushabiki ninaouzungumzia. Mtakuja kuamka siku moja na kukuta kuwa hao watu wabara wamechoka na hawautaki muungano. Hicho kilichofichika ni nini hasa? Kuwa tumekuwa kimbilio lenu wakati wa matatizo? Kuanzia waliokimbia kuozwa kwa lazima, walioshutumiwa na mauaji ya rais wenu wa kwanza( kuepuka kangaroo courts za huko kwenu) n.k. Marais wenu hata wale wanaodaiwa kuwa hawana haja na muungano wameretire bara! Ni nini hasa unachodhani kitawafanya watu wabara wangang'anie muungano kwa kila hali? Msijidanganye, huu muungano ni wetu wote ( tumeoana, tumezaliana n.k.)na haina haja kuubeza upande mwingine ati ni mabwege. Tutajuta wote ukitutoka.
 
fundi mchundo. karibu jf. wale maveterani wa jf wana msemo wanasema "where we dare to talk open". mnapenda kutuletea haya maneno ya kwamba ukivunjika muungano wapemba na waunguja watagombana .4get abt that, fitina yaa uunguja na upemba tunaijua inapandikizwa na nani, so u better leave it. majuzi niliskia mikoa kadhaa ya bara inaongelea kujitenga ili iwe nchi. hukuliskia hili? sasa unalichukuliaje hili? ,na hapa hatuubezi muungano tunachotaka ni marekebisho ya muungano, siasa za kutishwa tishwa zimepitwa na wakati. nakubali hata tanganyika inapata baadhi ya matatizo katika muungano huu na ndio maana naamini kuurekebisha ni jambo la wajibu. by the way usije ukanitoa nje ya mada ,zipo mada kadhaa humu zinaongelea muungano sasa ni bora ukaenda ukazifufua zile.hapa ni umeme.
 
Under-Age! Mimi naelewa hii ni www kwa hiyo hakuna kinachonishangaza. Sina haja ya kulumbana juu ya Muungano na mtu yeyote. Kinachonitubua ni pale mnapo dare kusema kuwa hata tukiutaka bure umeme tutapewa kwa vile kuna SIRI ya muungano! Siri gani? Unaamini kweli wengi wa walio bara haswa(wakulima, wavuvi n.k) give a hoot about Muungano? Ni pale wanapopachikwa mizigo isiyo na maana na upande wa pili unawabeza kuwa wao ni wezi, wajinga waliozubaa ndiyo maana wanafanyiwa hivyo. Arguments za Bin Maryam na SiDe ziliniingia ingawa hazikuni'convince'. Wewe na mwenzio Katibu Tarafa ndio mlionifanya nifufue ambayo hayakustahili katika mada hii. Kwa haya nawaachia wengine waendeleze mada kama iko haja.
 
F. Mchundo:

Miezi michache iliyopita mwakilishi wa World Bank alitembelea Tanzania. Na katika mazungumzo yake alisema serikali ni lazima iache kutoa ruzuku ya umeme.

Sababu zinazotolewa na serikali kutoa ruzuku hizo ni kulenga watumiaji masikini.

Asilimia kumi inayotumia umeme Tanzania sio masikini. Na wale masikini ambao wanalipiwa ruzuku na serikali (90%) hawategemei kutumia umeme kwa zaidi ya miaka 20 inayokuja.

Kwa mtaji huu, mtanzania bara anayeona kuwa anabebeshwa mzigo wa kulipa ruzuku ni lazima aelewe kuwa yeye pia analipiwa ruzuku. Aliyosema mwakilishi wa benki kuu ya dunia yalitolewa kwenye magazeti lakini sikuoni forum yoyote iliyogusia mada hiyo. Na forum azikugusa kwa sababu wachangiaji wengi ni watumiaji wa umeme na ruzuku inawasaidia.

Kumbukumbu zangu za mwisho ni kuwa Zanzibar ilikuwa inanunua umeme kwa dollar kutoka katika shirika lililopo katika jamuhuri ya muungano.

Think about this: Shirika la usambaji Zanzibar linunue umeme kutoka Tanesco kwa dollar alafu liuze umeme kwa kutumia Shillingi ya Tanzania na baadaye libadilishe shillingi ya Tanzania katika dollar na kulipa gharama ya ununuaji wa umeme.

Sasa hivi makampuni mengi ya uzalishaji ya marekani yanapeleka uzalishaji nje ya nchi. Uzalishaji unapelekwa nje ya nchi sio kutafuta malighafi badi kupunguza gharama zinazotokana kulipa wafanyakazi marupurupu makubwa. Gharama ya Infrastructure (mitambo na mambo mengine) na uendeshaji wake sio mkubwa sana.

Hivyo gharama za kuendesha mashirika mengi zipo kwenye Miundo ya mashirika ya umma kama Tanesco ni hasara tupu. Kuna wafanya kazi wengi na ngazi za uongozi zinazoongezea shirika matumizi makubwa. Mameneja wa shirika lazima awe na nyumba Upanga au Osterbay. Na mikoani pia mameneja wanaishi kama wakuu wa mikoa.

Mimi ni mtanganyika ninayeamini siasa za kibepari na masoko huria japokuwa sina pesa. Pamoja na imani zangu hizo bado naona umuhimu wa nchi za kiafrika kuungana. Na hili kuondoa migogoro ya muungano; serikali ziache kufanya umachinga wa kuwa na mashirika ya biashara.

Kwa mfano, pamoja na kuwa na maendeleo ya kiteknologia duniani, shirika la simu Tanzania lilishindwa kusambaza simu. Directory ya simu ya Tanzania nzima ni sawa directory ya wilaya moja iliyopo URUSI (na hapo bado naipendelea Tanzania). Na kama majukumu ya kusambaza simu za mkononi yangekuwa chini ya serikali yetu, uwezekano mkubwa ni kuwa wenye simu hizo ni wangekuwa wachache sana.
 
Bin Maryam, World Bank na wataalamu wengine waliishauri serikali ya Malawi iondoe ruzuku kwenye kilimo nao wakafanya hivyo. Kilichofuata ni njaa kali na kudorora kwa zao la mahindi. Mwaka jana serikali ya Malawi iliamua kurudisha ruzuku pamoja na pingamizi za hao wakali. Mwaka huu Malawi wanawauzia Zimbabwe mahindi! Hao asilimia kumi wanaozungumzia wengi wao wanatumia umeme kuwashia taa na kuangalia televisheni kama wanayo. Hawa si matajiri. Nenda huko posh areas za masaki na utakuta wanaoitwa vigogo wanapikia maharage kwa mkaa au jiko la mchina. Huo si utajiri. Tangazo la hivi karibuni la EWURA linasema kuwa shirika la umeme la zanzibar linauza umeme chini ya bei ya uzalishaji na wao wamebaki kushangaa. Shirika la umeme znz limekuwa mmoja wa wadeni sugu wa Tanesco hadi hapo serikali ya Muungano ilipowanusuru. sasa hilo la dola limetoka wapi? Kinachofanyika ni shirika kuuza umeme kwa bei ambayo si sustainable wakijua kama walivyosema wengine waliochangia mwisho wa yote serikali ya muungano itabeba mzigo maana hawana jinsi. Hakuna economics hapa. Naheshimu msimamo wako wa kutetea ubepari lakini ni lazima tuangalie athari zake. Nchi ambazo zina highest standard of living ziko Scandinavia na wao sehemu nyeti zote wanazicontrol. Hakuna untamed capitalism kule. Sisi tumekurupuka kuukumbatia bilakuangalia athari zake. Ndiyo maana tuko hapa tulipo.
 
Bin Maryam,
heshima yako mkuu, hapa umesema maneno ya maana sana na kuna kitu kimoja ambacho kutokana na hotuba za rais wetu JK nimekuwa na wasiwasi zaidi jinsi tunavyopanga ueundeshaji wa biashara hizi za huduma.
Kwanza kabisa binafsi naamini kuwa Ujenzi wa infrastructure ni kazi ya serikali sio mashirika binafsi hapa nikiwa na maana uzalishaji Umeme ama nguvu za mawasiliano ni jukumu la serikali kuhakikisha vifaa hivyo vipi na ktk hali ya juu vikimilikiwa na serikali. Yawezekana uendeshaji wake uwkawekwa under contract kwa kampuni binafsi lakini isiwe mali ya kampuni hiyo. Kisha tunapofikia swala la usambazaji ndipo makampuni binafsi yanapoingia na itakuwa vizuri ikiwa halmashauri za miji zitahusika zaidi.
Kwa hiyo shirika la Umma kama Tanesco linatakiwa kubakia shirika la kuzalisha umeme badala ya kushika yote ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme tena ajabu wakinunua umeme toka shirika binafsi (IPTL)..Hapo tumefanya kinyume kabisa cha uendeshaji wa shughuli hizi za huduma kwani hao IPTL ndio walitakiwa kuwa shirika la Umma nafasi ya Tanesco ndio maana leo tunashindwa kabisa kurekebisha hasara wanazoingia Tanesco. Hii yote ni ktk kuogopa kuwa shirika binafsi likianza ku deal na wananchi moja kwa moja kutakuwa hakuna tena mpango wa ruzuku kwa wananchi. Kosa kubwa tulilolifanya ni kuweka miundo mbinu yetu chini ya mashirika binafsi kisha tukaweka shirika la Umma kusambaza huduma hizo... matokeo yake vurugu tupu.
 
Bin Maryam, World Bank na wataalamu wengine waliishauri serikali ya Malawi iondoe ruzuku kwenye kilimo nao wakafanya hivyo. Kilichofuata ni njaa kali na kudorora kwa zao la mahindi. Mwaka jana serikali ya Malawi iliamua kurudisha ruzuku pamoja na pingamizi za hao wakali. Mwaka huu Malawi wanawauzia Zimbabwe mahindi! Hao asilimia kumi wanaozungumzia wengi wao wanatumia umeme kuwashia taa na kuangalia televisheni kama wanayo. Hawa si matajiri. Nenda huko posh areas za masaki na utakuta wanaoitwa vigogo wanapikia maharage kwa mkaa au jiko la mchina. Huo si utajiri. Tangazo la hivi karibuni la EWURA linasema kuwa shirika la umeme la zanzibar linauza umeme chini ya bei ya uzalishaji na wao wamebaki kushangaa. Shirika la umeme znz limekuwa mmoja wa wadeni sugu wa Tanesco hadi hapo serikali ya Muungano ilipowanusuru. sasa hilo la dola limetoka wapi? Kinachofanyika ni shirika kuuza umeme kwa bei ambayo si sustainable wakijua kama walivyosema wengine waliochangia mwisho wa yote serikali ya muungano itabeba mzigo maana hawana jinsi. Hakuna economics hapa. Naheshimu msimamo wako wa kutetea ubepari lakini ni lazima tuangalie athari zake. Nchi ambazo zina highest standard of living ziko Scandinavia na wao sehemu nyeti zote wanazicontrol. Hakuna untamed capitalism kule. Sisi tumekurupuka kuukumbatia bilakuangalia athari zake. Ndiyo maana tuko hapa tulipo.

Kufuata siasa ya Ujamaa haifanyi serikali kuwa wamachinga. Unatoa mifano miwili ambayo unajigonga mwenyewe. Wakulima wa Malawi ni wadogo wadogo kama hile asilimia 90% ya watanzania yenye kutofaidika na ruzuku ya umeme. Na mfano wako wa Malawi, umeonyesha kuwa ruzuku kwa walengwa inatoa mafanikio. Na hiyo ndio point ya Benk ya dunia. Sio kila wakati Benki ya dunia inafanya makosa, na kwa upande wa umeme Tanzania ilikuwa 110% kwenye ukweli.

Na ruzuku ya umeme ya Tanzania kama ingewafikia walengwa vijijini basi uzalishaji ungeongezeka kama vile wakulima wa Malawi walivyoweza kutumia ruzuku katika katika kilimo. Nyie mnaopata ruzuku ya umeme hili mwangalie vichupa (TV), hampo kwenye mlinganyo wa hesabu za kupata ruzuku (period).

Hao wanaotumia mkaa katika mapishi wanafanya hivyo hili chakula kinukie vizuri na sio kupunguza gharama za matumizi kwani kwenye mlinganyo wa nguvu(enegy) unaonyesha kuwa mkaa ni gharama kubwa kwa nchi. Hivyo hakuna sababu ya kutoa ruzuku hili mtu aangalie TV.

Vile vile mashirika yenye kufanya biashara yana akaunti ya mapato (Receivable) na ya malipo (Payable).Kama shirika la umeme linauza umeme kwa shirika la uzambaji Znz, inachofanya ni kuandika bill katika shirika la Uzambaji Znz na kusubiri mapato katika akaunti ya mapato (Receivable). Na sio kazi ya shirika la umeme kuangalia umeme huo unauzwa vipi huko Zanzibar.

Wateja wa umeme Znz wanalipa kiwango walichopangiwa na wanafanya hivyo. Na kama shirika la usambazaji Znz linakuwa sugu kulipa madeni hili sio swala la muungano ni suala la shirika la kibiashara kushindwa kujiendesha. Kinachotakiwa ni kuchukua hatua za kibiashara na hapo ndipo ubepari ninapoupenda.
 
Bin Maryam! Sasa kwa kuondoa ruzuku kama wanavyoshauri hao wakubwa wetu kutamfikishiaje umeme yule mkulima mdogo mdogo ambaye ndiye asili mia 90 ya watanzania. Au kama ulivyosema awali tuwanawie mikono kwa sababu hata katika miaka 20 inayokuja hawawezi kumudu kulipia huo umeme.

Hao vigogo wa tanzania unaamini kweli wanafanya hivyo kwa kufuata harufu na sio kuikimbia Luku? Hawa vijibosile (ambao kwa hesabu zako ndio wanazo) kuna wakati walikuwa wanafungia simu zao kwenye masunduku kuogopa bill! Wengi wao ni masikini tuu. Tatizo unaangalia hao wachache waliozikomba hela kwa njia wanazojua wao ndio hata upandishe vipi bei wao watamudu tu.

Sikuzungumzia Tanesco kwenye suala la znz bali EWURA ambao ni regulatory authority. Hizo hatua za kibiashara ambazo ungependa Tanesco wachukue ni zipi? Tanesco kuna wakati walijaribu kukatia umeme znz bila mafanikio. Huwezi kuepuka siasa za muungano kwenye hili. Unachokipendekeza ni utopiac. Bahati mbaya kwenye dunia hii tunayoishi ya Tanzania hakitekelezeki bila kubadilisha mfumo mzima wa utawala.

Usisahau pamoja na vijimall(?) kama Shoprite, vijighorofa na mahekalu ya kukufuru yaliyojaa Mbezi Beach Tanzania sio Marekani. Unbridled capitalism hatuiwezi. Wenzetu waliishakubali kuwa kuna watu watachwa kwenye neema wanayoifaidi wengine. Kushindwa kulipia joto mkazi wa kwenye projects Chicago lililiisha kubalika. Akifa, ni collateral damage. Hatuhitaji kwenda huko. Lazima tutafute njia mbadala. Period.
 
Back
Top Bottom