Under-Age! Mimi naelewa hii ni www kwa hiyo hakuna kinachonishangaza. Sina haja ya kulumbana juu ya Muungano na mtu yeyote. Kinachonitubua ni pale mnapo dare kusema kuwa hata tukiutaka bure umeme tutapewa kwa vile kuna SIRI ya muungano! Siri gani? Unaamini kweli wengi wa walio bara haswa(wakulima, wavuvi n.k) give a hoot about Muungano? Ni pale wanapopachikwa mizigo isiyo na maana na upande wa pili unawabeza kuwa wao ni wezi, wajinga waliozubaa ndiyo maana wanafanyiwa hivyo. Arguments za Bin Maryam na SiDe ziliniingia ingawa hazikuni'convince'. Wewe na mwenzio Katibu Tarafa ndio mlionifanya nifufue ambayo hayakustahili katika mada hii. Kwa haya nawaachia wengine waendeleze mada kama iko haja.
F. Mchundo:
Miezi michache iliyopita mwakilishi wa World Bank alitembelea Tanzania. Na katika mazungumzo yake alisema serikali ni lazima iache kutoa ruzuku ya umeme.
Sababu zinazotolewa na serikali kutoa ruzuku hizo ni kulenga watumiaji masikini.
Asilimia kumi inayotumia umeme Tanzania sio masikini. Na wale masikini ambao wanalipiwa ruzuku na serikali (90%) hawategemei kutumia umeme kwa zaidi ya miaka 20 inayokuja.
Kwa mtaji huu, mtanzania bara anayeona kuwa anabebeshwa mzigo wa kulipa ruzuku ni lazima aelewe kuwa yeye pia analipiwa ruzuku. Aliyosema mwakilishi wa benki kuu ya dunia yalitolewa kwenye magazeti lakini sikuoni forum yoyote iliyogusia mada hiyo. Na forum azikugusa kwa sababu wachangiaji wengi ni watumiaji wa umeme na ruzuku inawasaidia.
Kumbukumbu zangu za mwisho ni kuwa Zanzibar ilikuwa inanunua umeme kwa dollar kutoka katika shirika lililopo katika jamuhuri ya muungano.
Think about this: Shirika la usambaji Zanzibar linunue umeme kutoka Tanesco kwa dollar alafu liuze umeme kwa kutumia Shillingi ya Tanzania na baadaye libadilishe shillingi ya Tanzania katika dollar na kulipa gharama ya ununuaji wa umeme.
Sasa hivi makampuni mengi ya uzalishaji ya marekani yanapeleka uzalishaji nje ya nchi. Uzalishaji unapelekwa nje ya nchi sio kutafuta malighafi badi kupunguza gharama zinazotokana kulipa wafanyakazi marupurupu makubwa. Gharama ya Infrastructure (mitambo na mambo mengine) na uendeshaji wake sio mkubwa sana.
Hivyo gharama za kuendesha mashirika mengi zipo kwenye Miundo ya mashirika ya umma kama Tanesco ni hasara tupu. Kuna wafanya kazi wengi na ngazi za uongozi zinazoongezea shirika matumizi makubwa. Mameneja wa shirika lazima awe na nyumba Upanga au Osterbay. Na mikoani pia mameneja wanaishi kama wakuu wa mikoa.
Mimi ni mtanganyika ninayeamini siasa za kibepari na masoko huria japokuwa sina pesa. Pamoja na imani zangu hizo bado naona umuhimu wa nchi za kiafrika kuungana. Na hili kuondoa migogoro ya muungano; serikali ziache kufanya umachinga wa kuwa na mashirika ya biashara.
Kwa mfano, pamoja na kuwa na maendeleo ya kiteknologia duniani, shirika la simu Tanzania lilishindwa kusambaza simu. Directory ya simu ya Tanzania nzima ni sawa directory ya wilaya moja iliyopo URUSI (na hapo bado naipendelea Tanzania). Na kama majukumu ya kusambaza simu za mkononi yangekuwa chini ya serikali yetu, uwezekano mkubwa ni kuwa wenye simu hizo ni wangekuwa wachache sana.