KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Huu ndiyo mwonekano wa Barabara kutoka Wilayani Bariadi kwenda Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu, hii Barabara ni hatari Kwa Sasa imekuwa kero kubwa kwetu wananchi.
Barabara imejaa mashimo kuanzia Bariadi hadi Itilima, Kwa Sasa tunasafiri Kwa muda wa saa mbili wakati ni mwendo wa Dakika 30 Kwa gari.
Kwa hali ilivyo mbaya, akibebwa mjamzito akapitishwa kwneye hii Barabara lazima ajifungulie njiani, kama ni mgonjwa mahututi hawezi kufika akiwa hai.
Barabara inakera sana hii, inatesa ukipanda gari, hatujui kama wahusika wanaiona, tumezoea imekuwa ikifanyiwa ukarabati kila inapoharibika lkn Kwa Sasa muda mrefu imefanyiwa.
Tunajiuliza kwani sisi wananchi wa Simiyu hatulipi Kodi kwenye hii inchi? Au huku kwetu hakuna viongozi wa Serikali, au hakuna wahusika ambao ni Tanrods?
Toka kiangazi Barabara imekuwa mbaya sana mpaka Leo masika yameanza haipitiki hata kidogo, wakati ni barabara ya kiuchumi kabisa.
Barabara imeharibika vibaya sana, tunawaomba wahusika kutengeneza, ni barabara muhimu sana lakini inatutesa wananchi.
Kuona matengenezo bofya hapa ~ Barabara ya Bariadi - Itilima Mkoani Simiyu iliyolalamikiwa na Mdau yafanyiwa maboresho