KERO Barabara iliyojengwa Keko ni ya kupita gari moja tu, gari likiharibika itakuwaje?

KERO Barabara iliyojengwa Keko ni ya kupita gari moja tu, gari likiharibika itakuwaje?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BrownRange

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2020
Posts
927
Reaction score
1,191
Wakuu habari zenu,

Nimepita maeneo ya Keko, kuanzia chuo cha Diplomasia kwenda Chang'ombe Mataa, kunajengwa barabara, ya mwendokasi. Lakini barabara ya kawaida sijaielewa, kwenda ni gari moja, kurudi ni gari moja. Hivi ikitokea gari limeharibika njiani itakuwaje?

Wanaohusika naomba mlitafakari hili.

Nawasilisha.
 
Bila picha sisi watu wa nanjilinji huku maporini kabisa itakuwa ngumu kuelewa ulichoandika.

Camera ya sim yako haikuwekwa kwa ajili ya kujipiga wew mwenyew, bali pia inaweza kutumika kwa mambo ya msingi kama hayo ili kufikisha ujumbe wako kwa wahusika kirahisi.
 
Ukitaka iwe pana lazima watu wavunjiwe majengo yao...
 
Jiji lenyewe halikuwa well planned for future generations in streets passing roads utadhani the city master planners walikuwa na akili mgando kuwa Watu hawataongezeka baadaye, sasa nani alaumiwe kwa akili yako?
 
naboreka sana na iyo barabara tutateseka sana na foleni hasa malori ya kuingia pale pangan tameco kiwanda cha maji,bado monalisa,bado kwa bakhresa mule na jaffery industries yakiingia na kutoka foleni lazima.
 
Bora kungeachwa Kama zamani, haikuwa na lazima kujenga mwendokasi pale. Cha ajabu mwendokasi ndio umepewa nafasi kubwa
 
Ikikamilika hiyo wale wa Mandela Road na Gongolamboto kuja Ukonga mjiandae kupokea BRT
 
Ikikamilika hiyo wale wa Mandela Road na Gongolamboto kuja Ukonga mjiandae kupokea BRT
Kama zitajengwa Kama pale, Bora wakatae kupokea hiyo BRT. Naona tunabomoa badala ya kujenga. Sasa pale Kuna faida gani Karne hii ya 21. Si Bora watu wabomolewe walipwe, kijengwe kitu Cha maana
 
Kama zitajengwa Kama pale, Bora wakatae kupokea hiyo BRT. Naona tunabomoa badala ya kujenga. Sasa pale Kuna faida gani Karne hii ya 21. Si Bora watu wabomolewe walipwe, kijengwe kitu Cha maana
Na kwa pale keko ukiondoa Veta na yale maghorofa ya zamani ya Nhc kuwalipa fidia upande wa magurumbasi ni watu wachache mno kwa maana pale ddc ni chini ya serikali thru ccm,king palace pia ivo ivo pale sokoni pia chini ya manispaa ambapo mbele yake kuna showroom za fenicha.
 
Walishindwa nn kufanya hivyo, mwishoo kinajengwa, kituko, Kodi yangu inaniuma sana,
 
Back
Top Bottom