Hizo picha hapo ni kipande kilichopo mbele kidogo ya Kibaigwa kama unaenda Dodoma kwa kutazama inaonekana ujenzi umekamilika ila barabara haijafunguliwa mpaka leo ni zaidi ya miezi miwili tangu mkandarasi atoe vifaa vyake vya ujenzi.
Mkandarasi ameweka mawe kuzuia magari yasipite tunaomba ufatilie ili tujue tatizo ni nini maana rafi road ni mbovu pia na inaharibu magari.
Huu mkoa nao nahisi kuna ajenda ya kuufanya usiwe na barabara za uhakika za lami.Mfano hadi leo wameshindwa kabisa kuiunganisha Mpwapwa na barabara ya lami ya uhakika badala yake lami zimetengenezwa Mpwapwa mjini tu,yule mbunge mzee wa watu Lubereje maskini tangu mwaka 1975 kilio chake ni barabara tu.Job Ndugai yeye alifanikiwa kuweka lami Kongwa center tu..Hii ya Kibaigwa imesuasua hatimaye imeisha na bado inasuasua kufunguliaa tena
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.