DOKEZO Barabara Kigamboni ni changamoto

DOKEZO Barabara Kigamboni ni changamoto

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joined
May 6, 2024
Posts
77
Reaction score
103
Wahusika.

Hakuna asiyependa maendeleo, lakini kinachofanyika kwenye barabara hii kutoka mzunguko wa kwenda feri hadi Daraja la Mwalimu Nyerere ni kero.

Kama hakukuwa na fedha za kutosha, isingekuwa lazima kufumua kipande hiki kifupi cha barabara. Matokeo yake ni kero kwa watumiaji: magari kuharibika, tope kujaa mvua inyeshapo, na adha kwa watembea kwa miguu. Ni miezi mitatu sasa tangu mlipovuruga njia hii, na ni kero sana kwa watumiaji.

Njia hii sasa inasababisha foleni kubwa, hasa asubuhi na jioni. Tafadhali, kamilisheni kipande hiki kwa haraka ili kupunguza usumbufu huu.
 
Back
Top Bottom