A
Anonymous
Guest
Barabara kuu inayotoka Buzuruga kuelekea Nyasaka hadi kuungana na Airport Road jijini Mwanza ina mashimo mengi ambayo yamekuwepo kwa zaidi ya miezi sita bila kutatuliwa.
Hali hii inasababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara na inaweza kuhatarisha usalama wao. Tunaomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua za haraka kukarabati barabara hiyo ili kurahisisha usafiri na kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.