Ushauri wa bure kwa serikali ya awamu hii. Tumbueni hawa Tanroads Biharamulo. Sanjali na hili yaweza kuwa busara kuifunga kabisa barabara ya Rusahunga Benaco na ku i declare impassable kupisha ajali zinazoendelea kutokea kila uchao kabla ya kuleta maafa makubwa zaidi.
Barabara hii ni sehemu ya barabara kuu iendayo nchi jirani za Burundi, Rwanda na Congo. Sehemu kubwa ya Rusahunga hadi Benaco kwa hali iliyo nayo ni aibu kuwa serikali inapata mapato kwa kuitegemea kwani kwa ujumla haipitiki kabisa.
Hivi sasa sehemu ijulikanayo kama ngazi saba hali ni mbaya zaidi. Pana mashimo makubwa katikati ya barabara ambayo pia yame pelekea malori ya mizigo kuanguka na kufanya kupita katika njia hii ni suala la hatari sana.
Ni ajabu kuwa je maeneo haya yana wabunge, wakuu wa wilaya au wakuu wa mikoa? Je viongozi wa serikali hii wa nafasi tofauti wanasafiri katika barabara hii?
Ushauri wa bure kwa serikali. Kabla ya yale ya mv Nyerere na zingine ilikuwa vyema kuwawajibisha Tanroads na labda kuchukua hatua za haraka na dharura mno za kuifunga kabisa barabara hii.
Ni aibu na hali ya kukosa uwajibikaji kwa awaye yoyote kulea uozo wa vipande vya barabara ka hizi.
Ningali napambana ku upload hali halisi ya ajali na mashimo katika barabara hii kama ilivyokuwa leo.
Pathetic!
Pichani ni lori lililopata ajali ngazi saba katika barabara hii lilopelekea uzi huu. Lori hili mara baada ya uzi huu lilitolewa haraka haraka na kuvuta hadi nyakahura mizani. Sababu ya ajali - barabara mbovu.
Pia, soma; Sasa barabara ya Lusahunga – Rusumo yenye urefu wa kilomita 92, kujengwa kwa Bilioni 153

Barabara ya rusahunga Rusumo ni sehemu ya barabara kuu ielekeayo Rwanda. Barabara hii imetelekezwa vilivyo na tanroads na kuwa kupita katika njia hii ni Bomu linalo subiri muda tu.
Yale yale ya MV Nyerere na mengi yenye kufanana na hayo ambayo wananchi tunabakia kutolewa kafara kila uchao. Ni aibu kuwa tanroads wapo na kuwa ati kila mwisho wa mwezi wanapata mishahara na marupurupu yao yote pasi na kukosa.
Kwa uzi huu nitajitahidi kukusanya kuweka ajali zote zinasababishwa na ubovu wa barabara hii labda kwa njia hiyo hawa jamaa wataamka angalau na kunusurika maisha yasiyokuwa na sababu ya kupoteana.
Ushauri wa bure kwenu tanroads: fanyeni matengenezo barabara hii vinginevyo ifungeni kwani haifai kwa matumizi ya binadamu. Kwa hali ilivyo sasa ni janga linalosubiri muda tu.
Katika picha ni hali halisi ya hivi sasa na hizo na ajali za karibuni kuanzia ya jana. Sababu ubovu wa barabara.