Barabara ya 12, Tanga: Inadaiwa Polisi na Zimamoto wamempiga mtu mmoja aliyesaidia kuzima moto

Barabara ya 12, Tanga: Inadaiwa Polisi na Zimamoto wamempiga mtu mmoja aliyesaidia kuzima moto

Mkuu samahani yaani ukae nyumbani kwako askari wakufate wakupe kichapo bila sababu ndio imetokea hivyo au ni tofauti kidogo.
Kwa Askari wetu huu utaratibu ni wa Kawaida sana Mkuu.. Hata kama umelala kitandani na Mkeo, wakiamua wanaweza wakakuamsha na Mateke..

Na wakakupeleka kituoni na wakiamua wanakubambikia kesi kwamba wamekukamata kwenye Tukio la Ujambazi.. Na wataonyesha silaha ambazo watadai wamekukamata nazo..
 
Kwa muktadha wa tukio hilo. Ninachoona ni kuwa huyo muhusika amepigwa kwa kuwa ametoa msaada wa haraka kwa kuokoa mali na uhai wa jirani yake, kwa kuwa ndio mwenye kisima cha maji.

Sasa baada ya wao Zimamoto kuchelewa na kukuta tukio limeisha, wananchi walipoanza kuwapopoa, ndipo wao wakamsaka muhusika ambaye amesababisha wao kuonekana sio weledi.

Ndo wakampiga na kumjeruhi hivyo, hii yote kwa kuwa amefanya kazi nzuri iliyopaswa wafanye wao, na kuwa amewaonesha kuwa wao ni wazembe na kuwatia doa ktk uweledi wa kazi yao.

Wema huponza. [emoji25][emoji25][emoji25]

Hapo zimamoto wachukuliwe hatua kali za kisheria.
 
Acha uongo ww kama Huna cha kuandika kaa kimya mmekalia kuchafua jeshi letu tu .
 
Inasemekana nyumba ya jirani ilikuwa inaungua, na huyu jamaa nyumbani kwao kuna kisima cha maji so akajitolea pamoja na wasamaria wengine kuchota maji na kuzima moto huo, huku wakipiga simu taasisi ya zima moto kwa ajili ya msaada zaidi

Bahati mbaya fire brigade wakachelewa kufika hadi moto umezimwa, kwa hiyo walipofika wananchi wakaanza kuwapopoa kwa mawe, na wao wakaanza kupiga wanachi labda kwa kujihami

Ila kilichowakera wengi ni kwenda kumpiga mtu ambaye hakuwepo kwenye kundi linalorusha mawe na ni mtu ambaye ametoa mchango mkubwa sana wa mali na nguvu zake katika kuuzima moto huo

Inasemekana ameumia sanaa ndani kwa ndani na baadhi ya wakubwa na viongozi waliopo hapo wamempa 30,000/= tsh ili akajitibie huku wakimuomba msamaha

Sasa swali je hii ni haki?

Na inasemekana kuna waliosema watamrudia wamkomeshe yaani maisha yake yapo hatarini
Sijui tumsidieje huyu mtu mwema
Msaada tafadhali wa maoni tu
Kupopoa mawe jeshi la wazima moto ni sawa?
 
Kupopoa mawe jeshi la wazima moto ni sawa?
Si sawa kabisa,
Ila wao kupiga na kisha kutoa fidia ya ths 30,000/= ni sawa?
Usije ukasema walikuwa wanajihami,
Itakuwa ni sawa na waisraeli na wapalestina? Mawe kwa mizinga? 🤣
 
Kwa muktadha wa tukio hilo. Ninachoona ni kuwa huyo muhusika amepigwa kwa kuwa ametoa msaada wa haraka kwa kuokoa mali na uhai wa jirani yake, kwa kuwa ndio mwenye kisima cha maji.

Sasa baada ya wao Zimamoto kuchelewa na kukuta tukio limeisha, wananchi walipoanza kuwapopoa, ndipo wao wakamsaka muhusika ambaye amesababisha wao kuonekana sio weledi.

Ndo wakampiga na kumjeruhi hivyo, hii yote kwa kuwa amefanya kazi nzuri iliyopaswa wafanye wao, na kuwa amewaonesha kuwa wao ni wazembe na kuwatia doa ktk uweledi wa kazi yao.

Wema huponza. [emoji25][emoji25][emoji25]

Hapo zimamoto wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Nakazia
 
Wakati tupo Iyunga Polisi walimuua "MICHAEL SIKUPYA" wakati ndio alikuwa anawasaidia kutuliza mgomo wa wanafunzi.

Hivi vyombo, ovyo saaana!.
 
Back
Top Bottom