Kwenye mitandao ya kijamii leo, kumekuwa na habari kuhusu Kampuni ya Mabasi ya Ratco kuingiza barabarani mabasi mapya mawili na kuelezwa sasa mabasi hayo yatakuwa yanapishana nusu saa kuanza safari.
Mchangiaji mmoja alikwenda mbele zaidi akiandika; RATCO AMETOA GARI MBILI LEO KWA KILA NUSU SAA SASA NAHISI AMEENDA KUMKALIA ABOOD KWENYE SHINGO PALE MWEMBE CHAI NA NDY RATCO D 14 ZIMEANZA SAFARI LEO ABOOD ANAPATA UPINZANI MKUBWA KUTOKA KWA HUYU JAMAA SI DAR WALA TANGA.
Katika majibu mahali kwingine, wachangiaji wameandika; Ratco saizi yake ni Abood, lakini siyo mwamba Shabiby Line.
Mwingine akaandika; Sasa wenyeji wa Tanga mmeanza kutia akili. Endeleeni kutembea na makenika kwenye mabasi yenu. Hapa na hapa mnafanya gereji. Shabiby Line kama mamtoni vile.
Mwingine akaandika; Nilipanda Shabiby juzi kuja Tanga kikazi. Daa! Yale magari kiwango. Halafu nauli ni rafiki kwa uchumi wetu kwa sasa. Namba 1 nampa Hemed (Ahmed) Shabiby. 2 nampa Abood. 3 nampa Ratco. 4 nampa BM. Hao wengine waweke vikao kwanza ili wabadilike.
Baadhi ya wachangiaji waliweka taarifa za namba za usajili wa pleti namba ambapo mabasi ya Shabiby Line pekee ndiyo yalionesha hakuna lenye namba D. Yote ni E.
Usajili wa namba kwenye magari Tanzania unakwenda kwa alfabeti. Za kwamba zilikuwa A. Zikafuata B. Zikaja C na kufuatiwa na D. Namba mpya ambazo zipo sokoni kwa sasa ni E. Baadaye zitaingia F, G, H hadi Z.
Nje ya mitandaoni, wakazi wengi wa Tanga wanaofanya shughuli zinazohitaji usafiri wa kufika Dar, wameonesha kufurahishwa kwao na ujio wa mabasi ya kisasa ya Shabiby Line yenye hadhi ya V.V.I.P. Wamesema ukiongeza Abood na BM, Tanga imechangamka sasa.