Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Ni muda sasa wananchi wa kata ya Sinoni wanaotumia bara bara ya Engo wamekuwa wakilalamika ubovu wa barabara ya Engosengiu kutokea kipande cha makutano ya Reli, mjini hadi kwa mamalaizer kuelekea Nado, chakusikitisha hii ni moja ya bara bara ambayo ipo katika kata za mjini kabisa.
Kipindi cha jioni ambapo abiria ni wengi madereva wengi wa Hiace na Balaji wamekuwa wakikatisha ruti kutokana na ubovu wa barabara na kuelekeza gari kwenye ruti nyingine zenye bara bara ya Lami hivyo basi kuleta usumbufu mkubwa kwa abiria na hivyo kuchelewa kufika majumbani kwao.
Pia abiria Wamekuwa wakilalamika ubovu wa barabara hiyo ndio chanzo cha kuletewa Hiace mbovu kwenye njia yao kutokana na sababu kuwa hakuna tajiri atakaekubali Hiace (vipanya) zake zije ziharibikie huku.
Msimu wa mvua bara bara hiyo ndiyo huzidi kuchimbika na hivyo basi kuwa tabu hadi kwa watembea kwa miguu kutokana na kujazana kwa tope barabarani kwani imekuwa ikiwekewa kifusi tu na hivyo msimu wa mvua kuwa na utelezi pamoja na matope.
Wananchi wamekuwa wakiomba mara nyingi wawekewe Lami lakini hadi sasa hakuna majibu ya lini watawekewa.
I