KERO Barabara ya Igombe – Kahama (Mwanza) inatupa mateso makubwa Wananchi, Serikali ije kuokoa jahazi

KERO Barabara ya Igombe – Kahama (Mwanza) inatupa mateso makubwa Wananchi, Serikali ije kuokoa jahazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
bb5c9c2f-996c-4100-9b70-07e07cbb38ba.jpg

d5f9df86-9601-4291-a1ed-4ac010352fcd.jpg
Ni Mwendo wa takribani kilomita 16 nilipoianza safari mimi na abiria wenzangu kutoka mjini Mwanza kwenda Igombe, Kata ya Bugogwa, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza.

Tunasafiri kwa dakika kadhaa na kufika stendi ya Igombe, nashuka na kusogea katika maegesho ya pikipiki nakuomba kupelekwa mtaa wa Bujingwa na Kilabela iliyopo katika Kata hiyo.

Nauliza gharama za kunifikisha katika mitaa hiyo. Dereva wa pikipika ananiambia nauli ni elfu tatu, namuuliza ni umbali wa km ngapi ? ananijibu kwa kukadilia ni zaidi ya km 3.

Anasema bei imepanda toka Tsh.1000 hadi Tsh. 3000 kutokana na ubovu wa barabara.

Napanda pikipiki na kuianza safari. Inanishangaza kuona licha ya Kata ya Bugogwa ni maarufu kwa shughuli za uvuvi na kilimo lakini baadhi ya mitaa hali ya barabara inatisha, zinapitika kwa shida.

Tukiwa tunaelekea Mtaa wa Bujingwa nalazimika kumwambia dereva anishushe nitembee kwa miguu kuvuka sehemu korofi. Ni baada ya kutaka kudondoka.
b8050ef9-4c4a-41df-8f03-0129b79bd83b.jpg

97a1130d-f5d0-47ff-9cdb-5a3f83ecf5f5.jpg
Nalazimika kushuka na kutembea kwa miguu maeneo yenye makorongo huku nikizungumza na watumiaji wa barabara. Tukifika penye unafuu napanda pikipiki kisha tunaendelea na safari.

Ubovu wa barabara unawakera wananchi akiwemo mkazi wa Bujingwa Eva Misalaba,‘’ Barabara ni mbovu imejaa makorongo tunapishana na pikipiki kwa tabu. Watoto wanapita kwa hofu kwenda shuleni.

Revocatus Malendeka anasema “Usafiri wa pikipiki ulikuwa Tsh. 1,000 kwenda Bujingwa saizi ni Tsh. 2,000 hadi Tsh.3,000 na ukiwa na mgonjwa nyakati za usiku nauli si chini ya Tsh.10,000 kwenda kituo cha afya Karume.”

Nafika mtaa wa Bujingwa kisha nasogea hadi ilipo ofisi ya serikali ya mtaa wa Bujingwa, kwa bahati nzuri namkuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Shija Habari na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Bujingwa Shaban Nkungu tunasalimiana na kuzungumza.

Ubovu wa barabara ni changamoto kwa wagonjwa wanaosafiri kwenda kupata huduma ya afya. Hali hiyo inasababisha wananchi kuwalaumu viongozi wa serikali za mitaa kuwa wamewachagua lakini wameshindwa kutatua kero zao.

Fares Huzunya ni mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Kilabela anakerwa na ubovu wa barabara ‘’Ukienda hospitali ni shida pikipiki zinapita kwa shida wagonjwa wanahangaika.

"Tukiitisha mikutano Wananchi wanatulaumu viongozi, tunaonekana sisi sio watetezi wao. Wakati mwingine tunakuwa waoga wa kuitisha mikutano maana utawaambia nini wakati wanaona changamoto walizozipigia kelele hazitatuliwi" anasema Fares.

Wananchi wabeba mabegani majeneza yenye miili
Kero ya barabara inaelezwa kujadiliwa kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) lakini bado hakuna utatuzi, huku wananchi wa mtaa wa Bujingwa wakilazimika kubeba mabegani majeneza yenye miili kituo cha afya Karume kilichopo mtaa wa Bugogwa kupeleka nyumbani kwaajili ya maziko.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bujingwa, Shija Habari anasema barabara ni mbovu ina makorongo. Wananchi wanapita kwa shida na kwamba, tangu iharibike kusafirisha marehemu ni shida gari hazipiti.

"Mgonjwa akifariki watu wanalazimika kutembea kwa miguu wakiwa wamebeba mabegani marehemu akiwa ndani ya jeneza.

Mwili hubebwa kwa gari au Bajaji kutoka mochari kituo cha Afya Karume." anasema Shija.

Anaongeza kusema "Wananchi wakifika mtaa wa Kigote, bajaji haiendelei na safari kwenda mtaa wa Bujingwa. Mwili unashushwa chini wananchi wanabeba jeneza mabegani hadi nyumbani kisha makabulini.

“Tangu mwezi wa nne mwaka huu hadi sasa tulipata misiba minne ambayo tulisafirisha majeneza yenye miili kwa kubeba mabegani mwendo wa takribani km 3.’’anasema Mwenyekiti.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kilabela John Mang'ombe anasema '' Gari hazipiti, mgonjwa akiugua kusafirishwa ni mateso. Pia usafirishaji wa vifaa vya ujenzi, mazao toka mashambani na mahitaji mengine kutoka na kwenda Igombe ni shida.

Tunaomba Serikali hijitahidi kuboresha miundombinu. "Serikali itekeleze miradi kwa wakati maana uchaguzi uliopita Chama kilitunadi tukaahidi kutatua changamoto kwenye mitaa ambazo baadhi hazijatatuliwa '' anasema John.

Wataka barabara ya Lami kurahisisha maendeleo
Baadhi ya Wananchi akiwemo Shija Tarima wanaiomba Serikali kujenga barabara ya Igombe - Kahama kwa kiwango cha lami kutokana na kwamba matengenezo ya mara kwa mara katika barabara hiyo yanaigharimu serikali pesa nyingi.

"Ukipita barabara hiyo ya Igombe - Kahama inayofika hadi zilipo ofisi za wilaya ya Ilemela unapita mtaa wa Bugogwa, Igombe B, Kigote, Bujingwa, Kilabela, Igogwe, Ilalila, Kahama kisha Buswelu yalipo makao makuu ya Wilaya ya Ilemela.

"Barabara hiyo ikijengwa kwa kiwango cha lami, nauli kwa usafiri wa haice inaweza kuwa kati ya Tsh. 800- 1,000, Bajaji Tsh. 1,000, Pikipiki Tsh. 3,000 anasema.

Ubovu wa Barabara kuanzia Igombe hadi Igogwe huenda ukakitesa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kuwanadi wagombea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba, 27, mwaka huu kwakuwa kero ya ubovu wa barabara imekuwa mwiba kwa wananchi.

Shaban Nkungu ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Bujingwa anaeleza ubovu wa barabara utakavyowapa ugumu kuwanadi wagombea endapo Serikali haitatengeneza barabara.
 
Mwanza barabara nyingi hata za miji mipya ni mbovuu mnoo viongozi wapuuzi sana
 
Husasani barabara za nyamagana ni aibu nzito.Jichanganyen mtuletee huyo mabula wenu ten
 
Tuache tuijenge kizimkazi nyie pambaneni na hali yenu.
 
Back
Top Bottom